Ha ha haaa...Lizzy...nakusoma nakusoma...kumbe umeanza mdomo zamanieeeee
Loh,kweli mlikua watoto maana...!
Mi nilisutwa sekondari tena huo umbea uliniangukia tu jamani.
Kuna dada alikua anahisiwa mjamzito mi sikujua. Watu wakateta wakakatisha ghafla mi sikumjua anayesemwa kumbe anakuja na kaskia.
Badae tupo wawili akaniuliza mi nikasimulia kilichosemwa bila kujua namsema yeye.
Loh,kutoka pale akaenda kusema niliyomwambia,wakaja nikawekwa kati,najitetea watu wanazidisha kelele tu. Nikalia....lol
na nikaonekana mbea hasa
Loh,kweli mlikua watoto maana...!
Mi nilisutwa sekondari tena huo umbea uliniangukia tu jamani.
Kuna dada alikua anahisiwa mjamzito mi sikujua. Watu wakateta wakakatisha ghafla mi sikumjua anayesemwa kumbe anakuja na kaskia.
Badae tupo wawili akaniuliza mi nikasimulia kilichosemwa bila kujua namsema yeye.
Loh,kutoka pale akaenda kusema niliyomwambia,wakaja nikawekwa kati,najitetea watu wanazidisha kelele tu. Nikalia....lol
na nikaonekana mbea hasa
Yeahh hayo maneno ni ya kuyaogopa sana kwakweli.Heheh pole lizzy! Mie nilishawa wahi kusutwa na mama yangu tu ktk maisha kwa kumuongopea kwa baba! Ila tangu hapo alinifunda kutokutumia maneno alisema, anasema, atasema! Ila nimesuta wengi!
Da Prety ivi umbea umeshaacha au bado unaendelea nao maana mkao wako huo...umbea! umbea tu!
Heheh pole lizzy! Mie nilishawa wahi kusutwa na mama yangu tu ktk maisha kwa kumuongopea kwa baba! Ila tangu hapo alinifunda kutokutumia maneno alisema, anasema, atasema! Ila nimesuta wengi!
Ushawahi kuwa mmbea? Ulishasutwa?
Mi niliwahi zamani kidogo wakati nikiwa darasa la nne nadhani, na nilivunja urafiki na my 'then' best friend kwa huo umbea na hapo hapo nikakoma.
Kulikua na msichana mmoja darasani kwetu, mkubwa kuliko wasichana wote. Hata kukua(vunja ungo) alikua wa kwanza, yani darasa la nne tayari alikua ameshalipuka kila kona ya mwili, alafu alikua anapenda kweli kukunja sketi yake ya shule iwe fupi na kufunguo vifungo vya shati wakati wengine tulikua tunafunga mpaka karibu na shingoni. Zaidi ya hapo alikua hamaind kabisa kushikwa shikwa na wavulana na wenyewe wakawa wanajua na walikua wanamshika haswa.
Sasa bwana huyo msichana alikua na mdogo wake mdogo sana, maneno yakazuka kwamba yule sio mdogo wake ni mtoto wake kutokana na story zilizokua zinasikika kuhusu yeye na wanaume. Mimi baada ya kuambiwa na msichana mmoja jirani yangu kesho yake wakati wa kwenda shule nikamnong'oneza rafiki yangu. Siku moja hata sikumbuki kilitokea nini si akaenda kumwambia mhusika na wasichana wengine bana. Loh likanijia jopo bana. Basi kunipiga hawawezi, kwenda kushtaki kwa walimu hawawezi wakaishia kuongea tu. Baadae nikawaelezea kwamba mi niliambiwa na sikuongeza chochote, ila nikamwambia huyo msichana mwenyewe samahani kwa kumwambia mtu mwingine basi yakaisha.
Ila kwanzia siku hiyo yule rafiki yangu ubesti uliisha tukawa tunaongea kawaida tu. Since then maneno ya "nimesikia, akasema" hua nayaogopa kweli. Kusutwa noma!!!
Mh. Lizzy karibu kwenye kampuni ( km hupo)...
ha ha ha, pole
i can imagine...
Sijui nilie sasa hivi for u
ila kwa sasa hata nikisutwa siogopi