Umbali kati ya Misri na Israel ni KM 613, lakini wana wa Israel walisafiri kwa miaka 40

Umbali kutoka Misri kwenda Israel ni kilomita 623 tu. Lakini Musa na kundi lake (wana wa Israel) walitumia miaka 40 kutembea hadi kufika nchi ya ahadi.

Huu ni wastani wa kilomita 15 kwa mwaka, sawa na kilomita 1.25 kwa mwezi.

Hii ni sawa na mita 42 tu kwa siku, yani umbali nusu ya uwanja wa mpira.

Hii ni sawa na mita 21 kwa masaa 6(tukichukulia kua siku ilikua ni masaa 12 ya mchana pekee na usiku walikua wanalala)

Ni sawa na mita 10.5 kwa masaa 3(yani urefu wa penalti) kwa masaa 3.

Katika hali ya kawaida na katika historia watu wa kale walikua majabali(giants), ambao unbali wa mita 10.4 ni saww na hatua zake 3.

Nashindwa kuelewa, ina maana walikua wanapiga hatua moja kwa saa moja, kitu ambacho hata konokono tu atavuka huo umbali kwa saa moja.

Hizi hesabu nyie mnazielewa?

Mkuu kwa mujibu wa mahesabu yako umehesabu kana kwamba kuanzia siku wanatoka misri walitembea direct mpaka kanaani, ila ukisoma Biblia utaona kabisa kuna muda mwingi tu ambao walikuw wamepiga kambi;
*Kulikuw na wajawazito na watoto wachanga kweny kundi pamoja na wanaojifungua ambao hawawezi kutembea kwa muda huo kumbuka
*Kulikuw na wagonjwa pia
*Walipigana vita vingi tu njiani kama unajua vita huwa ina cost muda kias gan, kuna wakati ilikuwa inabid watume makachero wakapeleleze nchi za huko mbeleni
* Pia kuna wakati walimchukiza Mungu kabisa kwahy akawaacha wakajikuta wanazunguka mlima mpaka Mungu alipoamua mwenyewe kuwaonesha direction..
Ukisoma mtiririko kweny Biblia nafkir utaona tu
 
Walizungushwa jangwani kwa miaka yote kutokana na sababu kuu mbili na zimelelezwa kwenye hiyo bible
Sababu kuu ni kuabudu miungu mingine wakati wakiwa safarini walimkufuru Mungu aliyewavusha bahari ya shamu

Sababu ya pili kwa vile walikuwa wanaenda kwenye nchi ya ahadi (Kanani) kuna kizazi Mungu hakutaka kiingie kwenye nchi hiyo kumbuka hata Musa hakuingia Kanani alifia jangwani na Mungu akashughulika na mazishi yake
 
Biblia inasema Mungu aliwazungusha jangwani
Pili waliweka makazi ili wazalishe vyakula na haikuwa safari kama ya mbio za mwenge
 
Umbali kutoka Misri kwenda Israel ni kilomita 623 tu. Lakini Musa na kundi lake (wana wa Israel) walitumia miaka 40 kutembea hadi kufika nchi ya ahadi.

Huu ni wastani wa kilomita 15 kwa mwaka, sawa na kilomita 1.25 kwa mwezi.

Hii ni sawa na mita 42 tu kwa siku, yani umbali nusu ya uwanja wa mpira.

Hii ni sawa na mita 21 kwa masaa 6(tukichukulia kua siku ilikua ni masaa 12 ya mchana pekee na usiku walikua wanalala)

Ni sawa na mita 10.5 kwa masaa 3(yani urefu wa penalti) kwa masaa 3.

Katika hali ya kawaida na katika historia watu wa kale walikua majabali(giants), ambao unbali wa mita 10.4 ni saww na hatua zake 3.

Nashindwa kuelewa, ina maana walikua wanapiga hatua moja kwa saa moja, kitu ambacho hata konokono tu atavuka huo umbali kwa saa moja.

Hizi hesabu nyie mnazielewa?
Walikuwa wanaendawastani was kilometer 100 kisha wanakaa hapo kwa miaka kama Saba. Ina maana wanajenga mabanda wanaendeleza maisha.
 
KIOO,
Povu la niini sasa?,

usitake kila mtu awaze,aamini au kuyachukulia mambo kama wewe,

Ishi vile uonavyo ilimradi usimkosee aliyekuumba na kukupa uhai hata leo hii,

hebu onesha mtu hata mmoja aliye tumbukia shimoni kwa kufuata maagizo ya Mungu na watumishi wake.

Ukiongozwa na mihemko utakufa kwa kihoro bure.
 
Ikumbukwe kuwa waisrael walipokuwa misri utumwani miaka 400 walikuwa wapagani kabisa hawamjui Mungu kabisa. Na musa alipokuwa anaomba kibali kwa farao aliagizwa na Mungu kuwa aseme wape watu wangu ruhusa ili wakaniabudu jangwani... Lengo hasa la Mungu ni kuchukua mda mreefu jangwani ili awafundishe imani, wamjue Mungu na namna ya kumwabudu. Walikaa ktk kituo moja kwa mda mrefu sana wakifundishwa kabla ya kuhamia kituo kingine lakini waisrael walikataa matakwa ya Mungu mamilioni wakateketea jangwani. Original waliotoka misri walipona wawili tu ndo walioingia nchi ya ahadi wengine wote ni waliozaliwa njiani ndani ya hiyo miaka 40.... Ukweli ni kuwa Mungu alimpa mwanadamu uhuru wa kuamua, ukiamua kutompenda Mungu lazima upotee. Na ukiamua kumpenda Mungu ni lazima utaishi na utaiona ahadi zake... Wapo waliotumwa kuipeleleza hiyo nchi na walitumia mda mfupi tu wa siku 40 na wakarudi na mkungu moja tu wa mzabibu ambao ulibebwa na wanaume wawili, waisrael wakaona kweli hiyo nchi imebarikiwa mno. Wanaume wachache wakakiuka sharti la Mungu hivo wakaamua waondoke wapitie short cut ili wafike nchi ya ahadi haraka. Mungu akajiondoa kuwalinda hivo walipofika mahali walivamiwa na wenyeji njiani wakauawa.
 
kadagala1 swali la mleta mada mbona linajibika!
Kwanza tuanze na hapa!
slide_4.jpg
 
Nyoka Mwenye Makengeza

Kutoka 13:17

17 Wakati Farao
alipowaachia Waisraeli
waende zao, Mungu
hakuwapitisha katika
nchi ya Wafilisti, ingawa
njia hiyo ilikuwa ya
karibu. Mungu alisema,
“Sipendi watu hawa
wabadilishe nia na
kurudi Misri wakijua
itawabidi kupigana
vita.”

18 Badala yake,
Mungu aliwapitisha
Waisraeli katika njia ya
mzunguko kupitia
jangwani, kuelekea
bahari ya Shamu.
 
Nyoka Mwenye Makengeza nitakujibu kama ifuatavyo
2.jpg

Lengo la Mungu lilikuwa ni kutumia siku Arobaini tu toka Misri mpaka Kanani.

Ila mioyo migumu ya Waisraeli ndiyo ilikuwa kikazwo

Kama utakumbuka hata Musa hakuingia nchi ya ahadi kwa uasi wake kwa Mungu.

Musa na Aaroni waliambiwa na Mungu wauambie mwamba utoe maji,ila wao kwa ukaidi wakaamua kuupiga mwamba fimbo,japo ulitoa maji ila Mungu akaapa awataingia Kanaani.

Waisraeli walitumia miaka miwili kufika mipakani mwa nchi ya Ahadi!
Ukisoma Hesabu 12,utaipata hii habari

Dharau dhidi ya wale Wapelelezi wawili Kalebu na Joshua ndiyo ilimfanya Mungu awahukumu Waisraeli wote walio above 21 yrs old watafia jangwani bila kuiona Kanani,ila watalizungukwa jangwa la Sinai kwa miaka 40 mpaka wote wafe.

Kati ya waisraeli 2,400,000+ waliotoka Misri,ni wawili tu walioiingia Kanani:KALEBU NA JOSHUA TU!
 
Walipewa adhabu njia fupi ilikuwapo ila kulingana na adhabu walio pewa kuna jamii husika haikutakiwa kifika nchi ya ahadi hivyo kwa miaka hiyo wengi walio kusudiwa hawakufika na eneo lenyewe ni kama walizunguka sana
 
Ikumbukwe kuwa waisrael walipokuwa misri utumwani miaka 400 walikuwa wapagani kabisa hawamjui Mungu kabisa. Na musa alipokuwa anaomba kibali kwa farao aliagizwa na Mungu kuwa aseme wape watu wangu ruhusa ili wakaniabudu jangwani... Lengo hasa la Mungu ni kuchukua mda mreefu jangwani ili awafundishe imani, wamjue Mungu na namna ya kumwabudu. Walikaa ktk kituo moja kwa mda mrefu sana wakifundishwa kabla ya kuhamia kituo kingine lakini waisrael walikataa matakwa ya Mungu mamilioni wakateketea jangwani. Original waliotoka misri walipona wawili tu ndo walioingia nchi ya ahadi wengine wote ni waliozaliwa njiani ndani ya hiyo miaka 40.... Ukweli ni kuwa Mungu alimpa mwanadamu uhuru wa kuamua, ukiamua kutompenda Mungu lazima upotee. Na ukiamua kumpenda Mungu ni lazima utaishi na utaiona ahadi zake... Wapo waliotumwa kuipeleleza hiyo nchi na walitumia mda mfupi tu wa siku 40 na wakarudi na mkungu moja tu wa mzabibu ambao ulibebwa na wanaume wawili, waisrael wakaona kweli hiyo nchi imebarikiwa mno. Wanaume wachache wakakiuka sharti la Mungu hivo wakaamua waondoke wapitie short cut ili wafike nchi ya ahadi haraka. Mungu akajiondoa kuwalinda hivo walipofika mahali walivamiwa na wenyeji njiani wakauawa.
Pia maisha tulio nayo sasa yanatukumbusha maisha ya wana wa Israeli kule misri utumwani na ule mpango wa Mungu kuwapeleka nchi ya ahadi kwa hio hapa duniani tunapita na tumeahidiwa kwenda mbinguni kama tukimwamini bwana Yesu kuwa mwokozi wa maisha yetu hadi siku ya mwisho.
 
Haya mambo ni ya kiimani zaidi na sijui kama unataka malumbano ya kiimani au lah ila kumbuka Mussa alikuwa anawaongoza watu waliotoka utumwani na tunaambiwa utumwa usioelezeka so lazima wengine walikuwa na afya zisizokuwa nzuri,majeruhi waliokuwa wakiumia kwenye kazi za wamisri,walikuwepo walemavu nk na kipindi hiko hakukuwa na technology kama sasa kwamba mlemavu atapewa wheelchair au majeruhi atachukuliwa kwenye ambulance ilibidi aondoke nao wote kumbuka haukuachwa hata ukwato wa mnyama wa wana wa Israel...pia Mungu ili kuwaimarisha imani zao aliwapa mitihani kama kukosa maji na chakula,na ilibidi Musa kupanda juu mlimani kupokea maaigizo kutoka kwa Mungu kwamba afanyeje wapate mahitaji{sio kwamba Mungu hakujua wanachokihitaji alijua sana}pia ilifika mahali Musa alipanda mlimani akakaa kwa kitambo kidogo kushuka chini akawakuta Waisrael wamejitengenezea miungu wa kuchonga so unaweza kuona jinsi gani kulikuwa na mambo mengi.kingine walipita jangwani inawezekana walikuwa wanatembea usiku tu kuogopa kuumia na jua na walikuwa na wanyama wao hivyo pia ukorofi wa wanyama unaweza kuwa uliwachelewesha!
 
Hiki kitabu ni kitabu cha hovyo kabisa kuwahi kutokea juu ya ardhi.

Kuna makosa mengi mno ila ukishakuwa kondoo unatakiwa tu kuinamisha kichwa chini na mchungaji anakupeleka shimoni.

Hovyo kabisa. Pumbaaaaf.
Umemaliza kubwabwaja?
 
Wewe ilimradi Musa alifika kanaani basi.
mambo ya kilometa jometri mstatili na mraba, hayana maana yoyote, acha kujigeuza calculeta mkuu
Musa hakufika kanani, alioneshwa tu akaiona kwa mbaaaaali kisha malaika mtoa roho akamfikia
 
Ukisoma biblia utaelewa kwanini ilikua miaka arobaini...umesahau kwamba walikua na kambi nyingi , sikukuu, ibada na mapokeo ya amri kumi na mengi..hiyo kambi wanaweza wakakaa hata miaka 3, walipigana vita wakiwa safarini...na ukumbuke waliizunguka kukwepa kupita ktk nchi za maadui zao na namna ya kukabiliana na wakanaani..soma biblia yote yapo utaelewa
 
Haya mambo ni ya kiimani zaidi na sijui kama unataka malumbano ya kiimani au lah ila kumbuka Mussa alikuwa anawaongoza watu waliotoka utumwani na tunaambiwa utumwa usioelezeka so lazima wengine walikuwa na afya zisizokuwa nzuri,majeruhi waliokuwa wakiumia kwenye kazi za wamisri,walikuwepo walemavu nk na kipindi hiko hakukuwa na technology kama sasa kwamba mlemavu atapewa wheelchair au majeruhi atachukuliwa kwenye ambulance ilibidi aondoke nao wote kumbuka haukuachwa hata ukwato wa mnyama wa wana wa Israel...pia Mungu ili kuwaimarisha imani zao aliwapa mitihani kama kukosa maji na chakula,na ilibidi Musa kupanda juu mlimani kupokea maaigizo kutoka kwa Mungu kwamba afanyeje wapate mahitaji{sio kwamba Mungu hakujua wanachokihitaji alijua sana}pia ilifika mahali Musa alipanda mlimani akakaa kwa kitambo kidogo kushuka chini akawakuta Waisrael wamejitengenezea miungu wa kuchonga so unaweza kuona jinsi gani kulikuwa na mambo mengi.kingine walipita jangwani inawezekana walikuwa wanatembea usiku tu kuogopa kuumia na jua na walikuwa na wanyama wao hivyo pia ukorofi wa wanyama unaweza kuwa uliwachelewesha!
Ni kweli yale maisha yana aksi maisha ya leo mitihani mingi na migumu tunakutana nayo hii yote ni kuimarisha imani zetu.
 
Back
Top Bottom