Umauti Nisiri pekee Anae ijua Mungu

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,400
DID YOU KNOW?

Madaktari wa uingerza walisema atakufa majuz ndani ya masaa 24 lakin hadi Leo yupo hai,,,,
Je wajua nini Allah alisema,, ?

'umauti ni siri pekee anayo ijua yeye kua Wapi na lini na saa ngapii utakufa na kwa sababu ipi'
Tumche mungu kwa kadri ya uwezo wetu Ipo siku tutakutana


df0f3602d01e2134319e749d68408a2d.jpg
 
Nina jirani yangu mama yake ambaye ana cancer madaktari wake walimtabiria kifo tangu September ya 2015. Jamaa akawa anaomba mama apumzike kwa amani ili Xmas ya 2015 wale kwa amani. Mama hakurudisha namba 2015. Mama anaishi mji mwingine ambapo si mbali hivyo kila weekend jamaa na mkewe au yeye tu huenda kumuangalia mama na pia kumsaidia dingi wake kumuuguza mgonjwa.

July mwaka jana akaniambia amechukua likizo ya miezi mitatu kwa kuwa sasa mama yuko jirani na kurudisha namba. Mie nikajisemea tu don't be surprised for you mom to be here this Xmas (2016). Jamaa akaniambia usiseme hivyo it is too much for her and us we're both suffering a lot of course she is the one who is suffering the most. Tunashindwa kufanya lolote lile kwa kuhofia anaweza kufariki wakati wowote.

Kwa hiyo alipochukua likizo August 2016 ya miezi mitatu alijua mama hafiki November 2016. Likizo ya miezi mitatu ikakatika mama bado yuko hai. November madaktari wakaamua kumbadilishia dawa ambayo ikamsaidia mama hali yake kuwa na ahueni pamoja na ugonjwa wake. Last weekend walienda kumuona na kusherehekea miaka 77 tangu azaliwe.

Mimi si daktari lakini hili la Madaktari kutabiri mgonjwa atakufa baada ya muda gani sijui kama linafuata profession ethics zao na linaziweka familia katika wakati mgumu hasa pale kile kipindi kilichodhaniwa mgonjwa atakufa hafi.

Kwa maoni yangu Madaktari waepukane na hii tabia ya kutabiri huyu mgonjwa ataishi kwa miezi mitatu au sita ijayo tu. Mama wa watu walimtabiria kufa September 2015 kishakata karibu miezi 18 sasa. Hali yake si mzima kuna siku ana ahueni na siku anazidiwa zaidi lakini bado yuko hai na si ajabu anaweza kukata miezi 18 mingine na hata zaidi. Mungu mkubwa na yeye tu ndiye ajuaye siri ya umauti.

DID YOU KNOW?

Madaktari wa uingerza walisema atakufa majuz ndani ya masaa 24 lakin hadi Leo yupo hai,,,,
Je wajua nini Allah alisema,, ?

'umauti ni siri pekee anayo ijua yeye kua Wapi na lini na saa ngapii utakufa na kwa sababu ipi'
Tumche mungu kwa kadri ya uwezo wetu Ipo siku tutakutana


df0f3602d01e2134319e749d68408a2d.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom