Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Kila wakati na kila kiongozi mpya akiingia madarakani, inakuwa kama vile Tanzania ndiyo imezaliwa jana na yeye ndiye kiongozi wetu wa kwanza anayetokana na watanzania.
Mwalimu Juliusi Nyerere alipoingia tu madarakani, pamoja na mambo mengi sana aliyoyafanya na kuyajengea dhana, nadharia, na mipango mkakati, lakini aliwataja aliowaona kwamba ni maadui wa Tanganyika baadae Tanzania. Mwalimu alisema kuwa maadui wetu ni watatu, UJINGA, MARADHI NA UMASKINI.
Mwalimu baada ya hapo alikaa madarakani miaka 23 kabla ya kumkabidhi Mzee Ally Hassan Mwinyi. Mwinyi alipoingia tu alikabidhiwa "Ufagio wa Chuma" na wazee wa Dar es salaam ili afagie uozo uliokuwapo serikalini. Hapo tena utaona ni kama vile Mwinyi alipokea serikali iliyojaa uozo hadi kuhitaji kuwa na "ufagio wa chuma" ili kuufagia.
Mzee Mwinyi naye alipoondoka na kuingia Benjamini Mkapa, alikuja na kauli mbiu ya "Uwazi na Ukweli" kama vile kuonesha watangulizi wake hawakujali sana kuendesha mambo yao kwa uwazi na ukweli. Ni kama vile watangulizi wake kuna mambo walikuwa wanawaficha watanzania.
Alipoingia Kikwete na kupokea uongozi toka kwa Mkapa, yeye akaja na kauli mbiu ya "Kasi mpya, Nguvu mpya, Ari Mpya" kama vile aliingia na kuona kwamba wale waliotangulia kasi yao ilikuwa ndogo, nguvu dhaifu na wasiokuwa na hari. Waziri Mkuu wake Edward Lowassa akawa na msemo wake kwamba wanataka kuondoa tabia ya "Business as usual" serikalini.
Sasa tunaye Rais Magufuli ambaye ana kauli mbiu "hapa Kazi tu" ambayo kwa kweli mwanzoni mwa utawala wake ilishabikiwa sana na wafuasi wa CCM.
Lakini leo miaka 59 Tangu Tanganyika kupata Uhuru wake toka kwa Waingereza na miaka 53 Tangu mapinduzi ya Zanzibar lakini bado nchi yetu (Zetu?) ni Maskini. Kila mara ukiwasikiliza baadhi ya viongozi wetu ni kama vile tuko hivi tulivyo kwa kuwa "wakoloni" walitunyonya sana na "Mabeberu" wanatugandamiza tusisonge mbele kimaendeleo.
Hivi ni kweli kushindwa kwetu kupambana vizuri na wale maadui aliwaosema Mwalimu wa UJINGA, MARADHI na UMASKINI kunatokana na wazungu.Wazungu wanatuziaje kufanya mambo yetu ya kimaendeleo?