Umaskini tulio nao ni wa makusudi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Umaskini tulio nao ni wa makusudi!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kiby, Jul 30, 2010.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Jul 30, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Inawezekana umasikini watanzania wengi walio nao ni mpango mahsusi wa watawala. Ndio nasema watawala na sii viongozi.
  Fikiria kwa mfano watanzania wangejengewa mazingira bora ya ya kuwezesha kila familia kuwa na chakula bora, matibabu, maji, umeme, elimu na mengineyo yaliyo huduma kwa jamii achilia mbali maendeleo,
  Wale wanaonunua uongozi kwa kutegemea ufukara wa raia kama mtaji wao wangepata wapi wateja?
  Wanaodanganya kujenga miradi mbali mbali ya kijamii ikiwa watachaguliwa kana kwamba pesa zinatoka mifukoni mwao, nani angewapa usikivu kama raia wangepewa elimu?
  Ni wazi kabisa kuufuta ujinga, umaskini, njaa na utegemezi ni mwanzo wa kuiondoa serikali ya watawala wa ccm madarakani, jambo ambalo hawako tayari kulifanya.
  Hata hivyo tukubali kuwa chini ya kongwa hili la kupewa kipande cha kanga, kitochi, simu, asali, elfu kumi, hamsini nk, kabla ya kupiga kura milele? Jibu ni hapana!! Tushikamane sote kama jamaa moja keweza kuleta kutoka kwa pili. Kutoka kwa kwanza ni pale tulipojikomboa na ukoloni wa weupe, ambapo sasa tuna wajibu wa kuhimiza kutoka kwa pili kwa kujikomboa na ukoloni wa hawa weusi wa ccm walio jamaa moja nasi.
   
Loading...