Umaskini mbaya sana!

Umaskini mbaya sana!

Dr Jeremiahs

Member
Joined
Sep 4, 2020
Posts
39
Reaction score
314
UMASKINI MBAYA SANA!

Umaskini mbaya! Unaumiza, Unaogopesha, Unatisha

Umaskini unafanya Tufanye kazi ngumu za kuchosha, Kwa mishahara midogo isiyolingana na thamani ya kazi tunazofanya na Tunaridhika nayo.

Sifa zote za kupata ajira tunazo lakini umaskini unafanya tukose “Ajira” sababu hatuna cha kuhonga, zaidi ya Taaluma zetu na mioyo safi. Labda ndio maana ya lile neno “Mwenye nacho Huongezewa” (Hii ni kutokana na ukweli kwamba ajira nyingi zama hizi ni ama za kunununua, au uwe na connections)

Umaskini unafanya wale tuwapendao wanaolewa na wengine, na tunakubali Tu sababu hatuna uwezo wa kuwahudumia wao na familia zao ambazo tuko hali moja kiuchumi.

Biashara nyingi zinakufa kwa kukosa pesa ya kuziba pengo pale inapotokea hasara kubwa au tukio la kumaliza pesa {Misiba, ajali, Magonjwa, kuibiwa n.k)

Umaskini unafanya wenye Pesa ndio waonekane wana mapenzi ya kweli. Pesa imekuwa muhimili mkubwa wa mahusiano.

Umaskini unafanya tuamini wanawake wenye mapenzi ya kweli ni wale wasioomba pesa na wale wanaoomba Pesa wapo kimaslahi Zaidi na hawana mapenzi ya kweli.

Umaskini unafanya tuonekane hatuna thamani kwenye familia/ukoo. Hata tukitoa mawazo au ushauri kwenye vikao hamna anayesikiliza. Wanaopewa kipaumbele na kusikilizwa ni wale waliojijenga kiuchumi na wanaotegemewa na familia.

Umaskini umeua ndoto zetu kwa sababu wazazi walikosa uwezo wa kutusomesha hadi kufikia na kuziishi ndoto zetu. Kuna madaktari bingwa /wanasheria/walimu na wengine wengi ambao hawajafika kule walitamani kufika kwa kukosa Ada.

Umaskini unafanya tunapoteza wapendwa wetu kwa kukosa pesa za kumudu matatibabu

Umaskini unatufanya tuamini waliofanikiwa wanatumia njia zisizohali kufata mafanikio. Si ajabu ata wewe siku ukifanikiwa ukapewa Title ya “Freemason”

Na ikiwa kweli una nia ya kuua umaskini basi anza na ule umaskini wa fikra maana huo ndio chanzo cha kushindwa kufikia ile level ya financial Freedom hasa kwa kuanza na zile fikra za kujustify umaskini. Kama vile;
“Kuamini kwamba Waliofanikiwa wengi wamepitia njia zisizo halali, au pengine wamerithi kutoka kwa wazazi wao

“Fikra za kuilaumu Serikali kuwa haina mfumo bora wa elimu na kutotoa ajira za kutosha kwa wahitimu”
“Fikra za kusubiri wakati wa Mungu ufike, au ile kwamba kama Mungu amekupangia uwe maskini basi utakuwa maskini milele” na nyingine nyingi.

My Ndugu, kama usipoamka na kubadili aina hii ya Mindset basi nakuhakikishia umaskini wa kudumu.

Kama jinsi ambavyo kuwa na pesa nyingi sio gurantee ya kuwa na furaha kwenye Maisha, ndivyo ambavyo umaskini haujawahi kuwa chanzo cha furaha tangu kuubwa kwa ulimwengu. And the point sio kuwa Tajiri, bali ni kuwa na FINANCIL FREEDOM.

Kwa kumalizia Tu niseme kwamba kama kuna mtu atakukwaza ukwazika basi hizo hasira zimamishie kwenye umaskini, kama mpenzi wako atakusaliti ukaumia haswa basi huo uchungu uhamishie kwenye umaskini, kama kuna Boss/workmate au jirani yako utamchukia sana iyo chuki ihamishie kwenye umaskini UTAKUJA NIELEWA BAADAE.

“Poverty is not an accident, like salvery… it’s man-made… and can be removed by actions on man” ---NELSON MANDELA.

#Jeremiahs
 
Umeongea ukwel mtazamo kwenye maisha una nguvu sana katika kukupa amani ya moyo na nguvu ya kupambana💪.
 
Back
Top Bottom