Umasikini wetu; Matumizi na matanuzi

Rev. Kishoka

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
4,526
1,529
Nimekaa chini na kujiuliza tena, ni jinsi gani kawaida yetu Watanzania kuangalia bajeti yetu kwa kuangalia kuongeza mishahara na kupanda bei kwa bidhaa. Lakini nafikiri mara nyingi huwa tunakaa kimya kujiuliza hivi pesa tunazitumia vipi?

Mnakummbuka Baraza la kwanza la mawaziri la Awamu ya Nne lilikuwa kubwa mno na Wananchi tukahoji ukubwa wake kwa hali zetu masikini, bado tukakebehiwa na kuambiwa ni Baraza ka kukidhi mahitaji ya Mtanzania.

Sasa hivi hapa JF kuna mjadala mwingine kuhusu misafara ya CEO wetu kutalii dunia nzima na swali linarudi pesa tunapata wapi?

Nimepiga mahesabu ya haraka kuangalia uhujumu wa BOT, ATCL, Tanesco (IPTL na RDC) na maeneo mengine yote na nimekuja baini kuwa BOT pekee ni takriban $350,000,000.00 Hii ni sawa na shilingi 420,000,000,000.00 ambayo ni karibu 20% ya fedha za bajeti yetu ya mwaka jana katika fungu la maendeleo.

Ukijumuisha upotevu wa pesa za IPTL na RDC pamoja na gharama za ATCL katika miezi miwili iliyopita, utakuta kuwa pesa tulizopoteza kama Taifa kutokana na Uzembe na Uhujumu ni US $600,000,000.00 ambayo ni Shilingi 720,000,000,000.00 (bilioni 720) ambayo ni 32% ya fedha za bajeti ya maendeleo na ni 11% ya bajeti nzima ya nchi.

Aidha fedha hizi zilizohujumiwa ni 28% ya mapato yanayotokana na misaada ya wafadhili katika bajeti yetu.

Ukiangalia jedwali ninaloambatanisha hapa chini kutoka kwenye hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka huu wa fedha unaoishia Mwezi June, utakuta kuwa makadirio ya mapato yamefanana na makadirio ya matumizi. Sasa najiuliza jee, ni lazima tuzitumbue pesa zote tunazozikusanya?

Lingine la kusikitisha ni matumizi yetu. Inaelekea kana kwamba Tanzania kuna kisima cha kuchota pesa na kutumia kwa kupita kiasi. Je Serikali na Taifa havioni umuhimu wa kubana matumizi na kuanza kupunguza matumizi ya Serikali?

Katika bajeti ya Mama Meghji, anadai 18% ya bajeti ya Serikali ni kwenye mambo ya elimu, na 10% ni kwa masuala ya afya, je matunda gani tunayaona na pesa hizi zinatumika vipi ikiwa bado maradhi na ujinga vinatawala?

Ikiwa Bajeti ya Elimu ilikuwa shilingi 266,000,000,000.00 ambayo ni sawa na 36% ya pesa zilizohujumiwa, na ya afya ni shilingi 370,000,000,000.00 ambayo ni sawa na 51% ya pesa za uhujumu au jumla ya fedha za bajeti ya elimu na afya kwa mwaka 2007 ni 88% ya fedha zilizohujumiwa, je priorities za Taifa letu zimekwenda wapi?

Najiandaa bajeti hii inayokuja kuichambua kwa kuangalia makadirio ya mapato na matumizi na kuangaia kama kweli kuna nia ya dhati kuleta maendeleo.

La mwisho, ukianza kusoma hotuba ya Bajeti ya 2007, inaonyesha kuwa tulitumia takriban 70% ya pesa tulizotenga kwa ajili ya matumizi kwa bajeti ya 2006. Swali je hiyo 30% ambayo ilikuwa ni salio ilikwenda wapi? je kungewezekana ikahamishiwa katika miradi ya maendeleo?

Swali linakuja je kama fedha hizi za uhujumu zingetumika katika miradi ya maendeleo, je safari ya Mtanzania kuendelea ingechelewa kwa miaka mingine 40?

Nawatakia wiki njema.

http://www.tanzania.go.tz/bspeech2007_2008.htm


SPEECH BY THE MINISTER FOR FINANCE
HON. ZAKIA HAMDANI MEGHJI (MP),
INTRODUCING TO THE NATIONAL ASSEMBLY,
THE ESTIMATES OF GOVERNMENT REVENUE
AND EXPENDITURE FOR FINANCIAL YEAR
2007/08 ON 14​
TH JUNE, 2007


SUMMARY
Mr. Speaker,​
the revenue impact of the proposed
measures is as follows:
(billion Shilling)
Value added Tax (VAT) 0.400
Income Tax (1.809)
Excise Duty 34.446
Customs Duty 2.772
Motor Vehicles Fees 60.500
Fuel Levy 109.237
Non Tax Revenues 33.616

Total 239.161

56. Mr. Speaker​
based on the foregoing, the
budget frame for 2007/08 can be summarized as
follows:

Budget Structure​
Resources
A. Domestic Revenue 3,502​
i. Tax Revenue (TRA) 3,237
II. Nontax Revenue 265​
B. Foreign Grants and Loans (incl.
HIPC/MDRI)
2,549
C. Privatization Proceeds 15
Total Resources 6,067 Billion TSh

Expenditure
D. Recurrent Expenditure 3,866​
i. Public Debt/CFS 615
II. Ministries 2,358
iii. Regions 83
iv. Local Government Authorities 810​
E. Development Expenditure 2,201​
i. Demestic Resources 739
ii. Foreign Resources 1 ,462​
Total Expenditure 6,067 Billion TSh

 
Hivi pesa ambazo Chenge anasadikiwa kakutwa nazo "vijisenti" zingeweza saidia vipi Taifa letu? je si zingeweza kusaidia ule mradi wa umeme nyanda za juu ambazo Malima anasema tunahitaji fedha kwa takriban 60%?
 
Matumizi ya serikali ni makubwa sana lakini wafanyakazi wa kawaida hawana share kabisa zaidi ya vijisumni vya mishahara.Ukweli ni kwamba serikali inanunua vitu kwa zaidi ya asilimia 100 ya bei halisi ya hivyo vitu, huo ndiyo ukweli kama mimi muongo katafute listi ya bei za zabuni kwenye wizara na taasisi za serikali.Mchawi wetu ni manunuzi hili ndilo jini linalotunyonya na hapo ndipo kuna chanzo cha ufisadi na mikataba mibovu.
 
Kipesile,

What and where is our government spending its money for? Maana nikiangalia kuhusu kwa haraka haraka kuna mishahara, gharama za uendeshaji kama umeme, simu, maji, majengo, magari, samani, stationary, publications, misafara,makongamano and such. Sasa pesa hizi ni za matumizi.

Pesa za maendeleo mnyumbulishi wake ni nini?

Can anyone give us a complete line by line breakdown of government expenditure in the last year's budget?
 
Wewe Rv.Kishoka uko Tanzania ama wapi! wewe wamjua mswahili, yuko tayari kuwaua watoto njaa ili mradi yeye atumbue huko nje huku mama na watoto wakilia njaa. Kishoka hawa viongozi wetu wameshatusahau, lao moja maslahi yao mbele kisha watanzania next, wewe haushangai viongozi wetu safari za nje ni kila siku? unajua ni kiasi gani hutumika katika safari hizo? Nimeshasema kwa kuwa wao hutumia hata zaidi ya pato la Taifa(collection Tax)mwisho wa siku tunabaki tukiombaomba kwa waisani, faarifa nilizonazo ni kwamba wahisani nao wameanza kugutuka sasa sijui mwaka huu bajeti yetu itatekelezeka kivipi.
 
Wewe Rv.Kishoka uko Tanzania ama wapi! wewe wamjua mswahili, yuko tayari kuwaua watoto njaa ili mradi yeye atumbue huko nje huku mama na watoto wakilia njaa. Kishoka hawa viongozi wetu wameshatusahau, lao moja maslahi yao mbele kisha watanzania next, wewe haushangai viongozi wetu safari za nje ni kila siku? unajua ni kiasi gani hutumika katika safari hizo? Nimeshasema kwa kuwa wao hutumia hata zaidi ya pato la Taifa(collection Tax)mwisho wa siku tunabaki tukiombaomba kwa waisani, faarifa nilizonazo ni kwamba wahisani nao wameanza kugutuka sasa sijui mwaka huu bajeti yetu itatekelezeka kivipi.

Mura,

Sihitaji kuwa Tanzania au Ughaibuni kujua kuwa kama maato yako hayatoshi, basi ni lazima upunguze matumizi, hasa yale yasiyo ya lazima.

Watanzania tumeingiwa na kiwewe cha usanii wa kusema ni lazima kiongozi mkuu atalii dunia kuitangaza nchi. Najiuliza Kagame amefanya nini mpaka nchi yake sasa inaanza kukuwa kiuchumi kuliko Tanzania?

Je Kagame alikwenda kulialia kila kona kusema maafa ya Rwanda tunaomba msaada?

Sisi tuna upungufu mkubwa wa akili ya mambo ya fedha. Tunajua kutumbua, hatujui kuzalisha wala kuweka akiba.

Kiongozi wa shirika na wizara anaona ufahari kutumia pesa zote za bajeti na ni rahisi kuhalalisha matumizi hata yasiyo muhimu, lakini kuimarisha uzalishaji mali ambao utaleta ongezeko la fedha hakuna.

Aidha tunatawaliwa na tamaa na pupa ya kutaka kila kitu sasa hivi, na si kungoja maka tuwe na uwezo kamili. Tunakimbilia kutumia kununua kila tunachoambiwa hii ni fesheni, tunaacha kufikiria ni yapi ya lazima kwa muda huu kwa fedha hizi kiduchu, tunaishia kununua na kutumia kwa gharama ambazo si muhimu, lazima au dharura kwa fedha hizo kiduchu na zingine za kutoka lile kopo la Kimatonya ambalo kila Raisi wetu kalivaa kifuani mwake.
 
Aidha tunatawaliwa na tamaa na pupa ya kutaka kila kitu sasa hivi, na si kungoja mpaka tuwe na uwezo kamili. Tunakimbilia kutumia kununua kila tunachoambiwa hii ni fesheni, tunaacha kufikiria ni yapi ya lazima kwa muda huu kwa fedha hizi kiduchu, tunaishia kununua na kutumia kwa gharama ambazo si muhimu, lazima au dharura kwa fedha hizo kiduchu na zingine za kutoka lile kopo la Kimatonya ambalo kila Raisi wetu kalivaa kifuani mwake.
Rev. hapo ndipo kilipolala kiini cha ufisadi na umasikini wetu, wizarani na idara za Serikali watu wanapigana vikumbo kupika safari hata kama hazina tija kwa Taifa! Safari bado ndefu sana, angalau wakipunguza misaada tutaweza kujipima kama tunachopata kinatosha. Nina hakika Rais atakuwa mkali kwa ufisadi kwani akicheza nchi inamshinda, tofauti na sasa ambapo anasawazisha mabonde ya ufisadi na pesa za misaada, ambazo wakati mwingine unaambiwa zimebaki pasi kuambiwa zinatumika vipi kwenye bajeti inayofuata.
 
Rev Kishoka,
Sisi tuna upungufu mkubwa wa akili ya mambo ya fedha. Tunajua kutumbua, hatujui kuzalisha wala kuweka akiba.
..
Mkuu tatizo kubwa la Mtanzania hasa viongozi wetu ktk bajeti zetu huwa wanakula hata mbegu!..
Tunarudi kule kule kwa Nyani Ngabu!...Ukweli unaouma sana..
 
Rev. Kishoka topic muhimu lakini naona umeunderestimate sana losses zetu.

Naomba uingize twin towers saga, VX purchases, makongamano yasiyoisha, safari za nje za viongozi wote, Tax exemptions, madini yanayoibwa, investor (mafisadi) incentives.

Nadhani total losses zinaaproach $2 billion.
 
Rev. Kishoka topic muhimu lakini naona umeunderestimate sana losses zetu.

Naomba uingize twin towers saga, VX purchases, makongamano yasiyoisha, safari za nje za viongozi wote, Tax exemptions, madini yanayoibwa, investor (mafisadi) incentives.

Nadhani total losses zinaaproach $2 billion.

Moe,

Imebidi nifanye maeleo kwa kutumia makadirio ambayo kila mwananchi anayajua kwa wazi. Sasa ukichanganya no yote haya uliyoyataja, inabidi tujiulize kwa nini tulipokea zile pesa za Kichaka huku uwezo tunao?
 
Kwa maana hiyo Tanzania sio fukara bali inafukarishwa na watu wake hususan viongozi. kuwang'oa madarakani itakuwa panadol ya kutuliza maumivu,tiba kamili itakuja kwa kujenga maadili(values) kwa watanzania wote. Swali ni nani,lini na kwa njia gani hayo yafanyike.
 
Kwa maana hiyo Tanzania sio fukara bali inafukarishwa na watu wake hususan viongozi. kuwang'oa madarakani itakuwa panadol ya kutuliza maumivu,tiba kamili itakuja kwa kujenga maadili(values) kwa watanzania wote. Swali ni nani,lini na kwa njia gani hayo yafanyike.

Dada yangu Waridi,

Tumeaswa na jamaa wa Rai leo eti tuache kulalamika kuhusu ufisadi, tuangalie yale ya msingi yanayojenga Taifa. Sasa kama Ufisadi pekee ni 11% ya bajeti yetu, ni kosa gani kuhoji matumizi ya ile sehemu ya kumi ambayo inaingia mtaroni?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom