Umasikini ndio Ugonjwa Mbaya kuliko yote Duniani

Sure, hata watoto wa masikini hujiona dhaifu mbele ya watoto wa tajiri.pia mke wa masikini anaweza kuwa na hasira zisizo na sababu kwa mke wa tajiri, ni shida tupu, ni sawa na kusema one crisis leads to another ni mnyororo wa matatizo kwa kwenda mbele, tutafuteni hizi hela enyi watu japo juhudi haishindi kudra.


100%
 
You have a point grandma! Naona watu wanapambanua "umasikini" kwa maana ya kuwa na kipato duni. Umasikini ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kufanya jambo fulani bila msaada wa mtu mwingine,ile hali ya kuonewa huruma,hali ya kula dagaa chukuchuku ,kuvaa nguo za jerojero, utaitaje umasikini wakati umejinunulia mwenyewe?
Labda mleta mada na wanaoshabikia neno "masikini" au "umasikini" wanashindwa kuelewa kuwa hakuna binaadam ambae kwa vipindi fulani vya maisha yake anakuwa ni masikini wa kuonewa huruma na kusaidiwa hata awe na utajiri wa kupindukia.

Tafakari.

Mtazamo wa kudhani kuwa umasikini ni ugonjwa ni mtazamo duni na ni mtazamo wa watu wasio na fikra hata ya kuvalia nguo.

Jifikirie ulivyokuwa ukichambishwa ulipojinyea ulikuwa tajiri au masikini?

Jee, unafikiri hali kama hiyo haiwezi kukuta tuna hata ukiwa na Mali?

Muwe mnafikiri kabla hamjaleta utumbo. Umasikini ni sifa ya kuhurumiwa na si kuwa masikini hawezi kuwa na utajiri au akili zilizo bora kabisa.

Mtazame huyu alikuwa ni mwana sayansi wa kiwango cha juu duniani lakini kwa hali yake alipoishia si alikuwa masikini tu huyu wa kuhurumiwa?...

 
.
IMG_20190711_155630.jpeg
 
Umetoa uzi na kuhakikisha unanyamazisha hadi maskini tusitoe povu..anyway njia za kutusaidia kupata mitaji mtutajie pia, njia za kupambana na umaskini katika mazingira yoyote yale hadi kuushinda na je, inachukua mda gani kupambana na umaskini hadi kuushinda?? povu ruksa!
 
Thabo Mbeki kilichomuondoa na alipingwa sana alipozungumzia Aids sio tatizo kubwa kama linavyozungumziwa tatizo ni Elimu na umasikini kwa watu weusi na alitaka uwepo mfuko maalumu kwa ajili ya kuboresha Elimu ya watu weusi kama ilivyo kwa shule za watu weupe alipingwa sana akibezwa kuwa ilikua kauli ya kibaguzi leo hii SA umasikini umetamaraki sana kwa kweli...
 
NYONGEZA.
Ukiwa maskini halafu mkawa kwenye jumuiya kisha simu ya mtu ikawa haionekani... unaanza kupoteza amani.. unahisi jamaa wanakuhisi wewe ndo umechukua. hivyo unalazimika kuongoza katika kuitafuta mpaka ipatikane.ama sivyo utaacha impression wewe ndo umeichukua.

ukiwa maskini hata uikitokea mmekaa watu wengi halafu mmoja akatoa gesi chafu.. watu wanakutizama wewe wanaamini wewe ndo umeharibu hali ya hewa.eneo hilo. yaani kila kitu kibaya kinahusishwa na maskini na kila kizuri kinahusishwa na utajiri.
Aisee! Nimecheka sana mkuu 🤣🤣🤣.
Uko sahihi!
 
Thabo Mbeki kilichomuondoa na alipingwa sana alipozungumzia Aids sio tatizo kubwa kama linavyozungumziwa tatizo ni Elimu na umasikini kwa watu weusi na alitaka uwepo mfuko maalumu kwa ajili ya kuboresha Elimu ya watu weusi kama ilivyo kwa shule za watu weupe alipingwa sana akibezwa kuwa ilikua kauli ya kibaguzi leo hii SA umasikini umetamaraki sana kwa kweli...
Mkuu elimu bora ni kitu muhimu sana maishani.
 
Umeni-bariki
NDUGU WAPO SHULENI NA KAZINI!

BAADA ya baba kufariki dunia, mama alibaki kuhangaika kufanya kazi ngumu, ikiwemo vibarua ili kulea watoto wake mapacha. Wa kiume Kulwa na Dotto wa kike.

Siku moja Kulwa alimuuliza mama: "Mbona tangu baba afariki ndugu hawatutembelei? Wanakwenda kwa baba mdogo na shangazi peke yake." Mama akajibu: "Ndio maana naamka pwee kwenda vibaruani ili niwaletee ndugu wengi na marafiki."

Siku nyingine Dotto aliuliza: "Mbona shangazi, baba mdogo na watoto wao hawatutembelei? Sisi ndio tunaenda kwao. Na tukienda hawatuchangamkii." Mama akajibu: "Ndio maana nakurupuka asubuhi kwenda vibaruani ili nanyi muwe mnatembelewa na mchangamkiwe."

Siku nyingine Kulwa alihoji: "Mbona ulisema unaenda vibaruani kutuletea ndugu na marafiki, watutembelee na kutuchangamkia lakini hatuwaoni?" Mama akajibu: "Nafanya vibarua nawapeleke shule. Huko mtapata ndugu na marafiki wa kuwatembelea."

Wakiwa sekondari bweni, likizo walirejea na marafiki. Dotto akasema: "Mama kweli shuleni kuna marafiki. Huyu ni rafiki yangu na yule ni rafiki wa Kulwa. Likizo hii wametumbelea. Likizo nyingine Kulwa atamtembelea rafiki yake na mimi nitaenda kwa rafiki yangu. Tumepata watu wa kututembelea."

Jioni mama aliwaita wanaye pembeni akawaambia: "Sikumaanisha hao marafiki mliokuja nao. Nataka huko shuleni msome kwa bidii na mtaona ndugu na marafiki wengi wa kuwatembelea." Walisoma na kuhitimu shahada za uongozi wa biashara.

Mama akawaambia: "Sasa karibia wale ndugu na marafiki wa kuwatembelea wataanza kufurika, fanyene kazi sasa." Kulwa na Dotto walifungua kampuni yao. Biashara zikawaendea vizuri. Wakaajiri mamia ya watu. Wakajenga nyumba kubwa tatu kwenye kiwanja cha heka mbili. Moja ya mama, Kulwa yake na Dotto pia. Wakazungushia uzio mmoja.

Siku moja jioni baada ya chakula cha jioni, Dotto aliuliza: "Mama kumbe tuna ndugu kijiji cha Mshinyole? Wamenipigia simu wanakuja kututembelea wiki ijayo." Dotto akasema: "Baba mdogo na shangazi walikuja ofisini leo, wanataka tufanye kikao cha ukoo, wanasema sisi watoto tunakua vibaya, hatuna ukaribu wa kindugu."

Mama akacheka, akasema: "Anzeni sasa kupokea ndugu. Fungueni milango mtembelewe. Msingeyashinda maisha msingetambulika. Baba mdogo wenu na shangazi yenu walikuwa wapi kuwakusanya kipindi kile? Sababu mlikuwa hamvutii. Baada ya kusoma na kufanikiwa kimaisha, tayari mnavutia. Jibu mnalo sasa, muwaambie na wajukuu zangu kama sitawaona kuwa ndugu na marafiki huja kwa wingi baada ya kufaulu shuleni na kufanikiwa kimaisha."

Basi sawa! Tuwaabie watoto wetu kuwa ndugu na marafiki wengi watawafuata kama watafaulu shuleni. Tusemezane kwamba tupige kazi tuyashinde maisha, ndugu na marafiki mbona ni wengi tu!

Ndimi Luqman MALOTO
 
Back
Top Bottom