Umakini katika madini unaweza kunusuru uchumi na kuimarisha shilingi

Kwa nini umeamua kubadilika?
 
Hebu tuendelee na mjadala huu...na tupende kuwa honest
 
Kumbe Mhe Mnyika naye ni member mwenzetu?
Taratibu mtakuwa watu wazima ....tutawafundisha uzalendo ...napenda msimamo wa vijana ujengwe kutokana na kusoma na kuelewa vilivyo mambo...sio ushabiki wa ajabuajabu.

Kwa upande wa wanasiasa ni vyema wakajitathmini kabla ya kuongea kwani ipo siku tutawauliza na kuwahukumu juu ya yale waliyooyaandika.

Hebu cheki hapo juu mnyika anavyoongelea uharaka kuhusu kubadilishwa kwa mikataba ya madini halafu leo hii chadema wamekuja na msimamo gani!

TAFAKURI::;
 
Wewe inawezekana ni mtu mzima lakini huna akili mkuu, CDM hawapingi mikataba isipokuwa wanataka iwe wazi na siyo kujifungia nyinyi CCM pekee.
 
Wewe inawezekana ni mtu mzima lakini huna akili mkuu, CDM hawapingi mikataba isipokuwa wanataka iwe wazi na siyo kujifungia nyinyi CCM pekee.
Soma hii mada acha kutazama na kushangaa majina ya Members
 

Kwa hali hiyo nilishauri hatua za dharura za Rais na Bunge katika kuongeza uzalishaji na usambazaji hususani wa vyakula katika soko la ndani, kuwezesha wazalishaji wadogo na wa kati katika kilimo na viwanda kuongeza mauzo ya nje na kuharakisha matumizi ya gesi asilia na utekelezaji wa mpango wa dharura wa umeme.Juhudi hizo ziende sambamba na kampeni maalumu ya kuhamasisha watanzania kununua bidhaa za ndani na serikali kutekeleza mkakati wa kupunguza manunuzi yake ya nje kwa bidhaa na huduma ambazo zinapatikana nchini. Kadhalika, kwa upande wangu nilieleza kusudio la kuwasilisha bungeni muswada wa sheria ya udhibiti wa bei ya bidhaa muhimu hususani za chakula ili kukabiliana na ukiritimba katika soko na kuweka mfumo wa kupunguza gharama za maisha kwa watanzania wa kipato cha chini.

Kwa upande mwingine, nilieleza kwamba kwa kuwa mfumuko wa bei unachangiwa pia na matatizo katika mfumo wa bajeti na matumizi ya serikali kutokana na ufisadi, ubadhirifu, matumizi ya anasa, mikopo isiyokuwa na udhibiti, kushuka kwa mapato ya serikali ikiwemo kupungua kwa fedha toka washirika wa kimaendeleo kutokana na matatizo ya kifedha katika ukanda wa ulaya; hivyo hatua za dharura za kibajeti na kimfumo zinahitajika kwa kuhusisha serikali na bunge badala ya kuachia hatua za kisera za fedha za benki kuu pekee.

Wenu katika utumishi wa umma,

John Mnyika
Mbunge wa Ubungo na
Waziri Kivuli wa Nishati na Madini
28/10/2011

[/QUOTE]

CCM ni chama sikivu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…