Umakini katika Kuadhibu watoto wetu

Umakini katika Kuadhibu watoto wetu

AFRIKAN GUY

Member
Joined
Jun 26, 2015
Posts
67
Reaction score
74
Nilikua natumia muda kufikiria namna gani ni mwadhibu mwanangu kulingana na kosa alilotenda, kiasi kwamba mpaka nahairisha kumwadhibu au nasahau.

Nimelelewa na mzazi ambaye anapiga balaa, yaani anatandika kinouma. kiasi kwamba ninamuogopa mpaka leo.

Lakini katika kusoma soma kwangu nikapata kaexposure kidogo kakusoma mambo kadhaa kuhusu adhabu kwa watoto, nikagundua mimi ni mwathirika wa Mtu aliepata adhabu ilizopitiliza utotoni.

So naogopa sana mwanangu awe kama mimi. kwasababu kuna gharama kubwa anazolipia na alizilipia mzazi wangu kwasabab ya namna alivonilea. mimi nililipa gharama za kutumbukia kwenye mabalaa lkn sikuweza kumwambia mzee, mzee alipitia na anapitia gharama za kukosa ukaribu na mimi, ukaribu ambao hauwezi kuja ghafla kama anavyotaka yeye. (though najitahidi lkn yeye hajabadilika)

Kwahiyo mimi nimeamua nitakua na urafiki mkubwa na mwanangu, kwasababu ataweza kuniambia lolote hata kama akitumbukia kwenye mabalaa atanambia kirahisi.

Na kuhusu adhabu nitajitahidi nisimtukane wala nisimdhalilishe, nikifanya hivyo nitamwomba msamaha. na akifanya makosa yyte nitajitahidi:
  • ajue makosa yake na nimweleze kwanini hilo ni kosa.
  • Kumwekea Muda wa Kutulia ili afikilie makosa aliofanya.
  • Kumwondolea Privilege endapo atakosa.
Nitampa adhabu lakini nitajitahidi asihisi kama namchukia. nataka aendele kujua kua nampenda na nataka awe mtu bora.
 
nilikua natumia muda kufikiria namna gani ni mwadhibu mwanangu kulingana na kosa alilotenda, kiasi kwamba mpaka nahairisha kumwadhibu au nasahau.

Nimelelewa na mzazi ambaye anapiga balaa, yaani anatandika kinouma. kiasi kwamba ninamuogopa mpaka leo.

lakini katika kusoma soma kwangu nikapata kaexposure kidogo kakusoma mambo kadhaa kuhusu adhabu kwa watoto, nikagundua mimi ni mwathirika wa Mtu aliepata adhabu ilizopitiliza utotoni.

so naogopa sana mwanangu awe kama mimi. kwasababu kuna gharama kubwa anazolipia na alizilipia mzazi wangu kwasabab ya namna alivonilea. mimi nililipa gharama za kutumbukia kwenye mabalaa lkn sikuweza kumwambia mzee, mzee alipitia na anapitia gharama za kukosa ukaribu na mimi, ukaribu ambao hauwezi kuja ghafla kama anavyotaka yeye. (though najitahidi lkn yeye hajabadilika)

kwahio mimi nimeamua nitakua na urafiki mkubwa na mwanangu, kwasababu ataweza kuniambia lolote hata kama akitumbukia kwenye mabalaa atanambia kirahisi.
na kuhusu adhabu nitajitahidi nisimtukane wala nisimdhalilishe, nikifanya hivyo nitamwomba msamaha. na akifanya makosa yyte nitajitahidi:
  • ajue makosa yake na nimweleze kwanini hilo ni kosa.
  • Kumwekea Muda wa Kutulia ili afikilie makosa aliofanya.
  • Kumwondolea Privilege endapo atakosa.
nitampa adhabu lakini nitajitahidi asihisi kama namchukia. nataka aendele kujua kua nampenda na nataka awe mtu bora.
Jambo zuri sana aisee
 
Lakini Tambua mtoto umleavyo ndivyo
hio methali ina maana kwamba tabia, mienendo, na maisha ya baadaye ya mtoto hutegemea malezi anayopata utotoni. Ikiwa mtoto atalelewa kwa maadili mema, upendo, na nidhamu, kuna uwezekano mkubwa kwamba atakua mtu mwema na mwenye maadili. Vilevile, mtoto akilelewa kwa njia mbaya, kuna hatari ya kuendeleza tabia hizo mbaya hadi ukubwani.
 
Malezi ni pamoja na mijeledi.huwezi kusema unamlea mtoto Kwa kumwambia Kwa upole Hadi anakuwa mtu mzima
 
Malezi ni pamoja na mijeledi.huwezi kusema unamlea mtoto Kwa kumwambia Kwa upole Hadi anakuwa mtu mzima
Viboko muhimu, lkin vilingane na kosa na vifwatane na maelekezo. na visiendeshwe kwa hasira bali viendeshwe kwa lengo kuu la kumfanya mtoto awe mtu bora.
 
Back
Top Bottom