Interest
JF-Expert Member
- Apr 11, 2015
- 3,434
- 7,096
Nimetazama makala iliyoandaliwa na Citizen TV ya Kenya kwa Dkt. Reginald Mengi. Nikajisikia vizuri na vibaya kwa wakati mmoja.. Mixed feelings.. Excited and Disappointed.
Media zetu zinafocus kwenye mambo ya siasa tu ambako nako hakuna jipya.. Hivi tunakosa ubunifu mdogo kama huu kweli? Hii makala imefanywa poa sana na kwa kiwango cha kuvutia. Mzee Mengi is very simple and cooperative... Makala imefanyikia nyumbani kwake kiroho safi..
Mimi ni mdau wa Media.. Naumia sana nikiona Tanzania hatufanyi vizuri eneo hili wakati tuna rasilimali za kutosha sana.. Isitoshe watanzania ni watazamaji wazuri wa vitu vya kwao.. Huu ni mtaji tosha..
Tuna watu mashuhuri kibao ambao watu wangependa kuwafuatilia story zao kwa mtindo huu wa makala..
Youngest Billionaire wa Afrika, Mohammed Dewji MO anatokea Tanzania na kwa bahati nzuri jamaa yuko very humble and accessible.. Mpaka leo sijaona content yoyote iliyofanywa na media zetu kwa mtu kama Maxence Melo ambaye mchango wake umetambuliwa mpaka na Rais Buhari wa Nigeria hivi majuzi.. Tunao akina Flaviana Matata wanafanya mambo makubwa huko duniani, Mbwana Samatta na wengine lukuki.. Hizi ni hela ujue?
Wakenya wanatuzidi maarifa sehemu ndogo ndogo kama hizi.. Kwenye burudani Tanzania inaongoza Afrika Mashariki kama sio Afrika kwa ujumla.. Sio filamu na muziki pekee.. Kila idara ya burudani tuko vizuri kwa kiasi kikubwa.. Hizi ni hela ambazo media zinashindwa kuzifikia.. Hatuna maarifa?
Siamini kama media zetu zimeishiwa ubunifu wa kutengeneza contents wakati kuna soko la kutosha tu.. Najua kabisa tuna wabunifu hawashindwi kuandaa makala za namna hii.. Tatizo liko wapi?!
Natoa wito kwa Media zibadili namna ya kufikiri.. Biashara haipo kwenye kufanya news coverage and reporting pekee.. Content kama hizi zinaongeza viewership na zinalipa sana..