Umagufulification wa Rais Samia

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
11,975
48,843
Sasa yule jamaa wa ccm kakamatwa na kufungwa kwa kutoa maoni yake tatizo ni nini je haturuhusiwi kutoa maoni au kumsema Rais!!

Rais lazima atambue anaishi kwa kodi za walala hoi hvyo lazima asemwe ni ujinga kumkamata mtu kisa kamsema Rais !!

Samia Sasa kafikia point ya mwisho ya ule umagufulification ambao ulipigwa kwa nguvu nyingi

Ila kwa vile Samia ni mwanamke wanaharakati wamepigwa kimya kwa sababu alifungulia vile vi NGOS fake vije kumsifia.

Akisemwa watu wanatumia uanamke na dini yake kumkinga

Ila ukweli uchaguzi ujao utachezewa Kama ule wa 2020 kwa sababu magenge ya wezi yote yapo upande wake.

Samia na Magufuli wameshafanana kila kitu tofauti yao ni moja tu Huyu kaongeza na matozo.

Samia ni silent killer anakuua huku anacheka tu!!

Nawaambia 2025 hakuna uchaguzi ni maigizo tu ya uchaguzi

Chadema amasisheni nguvu ya umma Ili 2025 mtafute madiwani na wabunge angalau 45 kwa kutumia nguvu maana 2025 hakutakuwa na uchaguzi bali maigizo tu !!

Niko pale!!
 
Hapatakuwa na UCHAGUZI wowote kabla ya kupatikana Kwa TUME huru ya Uchaguzi na Katiba mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA .

Ameeeeen
 
Wewe ndie umeita jina zuri, "Umagufulification wa Samia" kuna wengine hawauoni huu..

Wao wanawekeza kumsifia Samia kwa kuacha kufanya mabaya baadhi aliyokuwa akiyafanya Magufuli, huku mengine anayofanya sasa wao wako kimya.

Hawa wanataka tupoteze muda kusifia mabaya yaliyopita yasiyofanywa sasa, wakati hata sasa kuna mabaya yanayofanana na yaliyopita, yakiwa ndio yanatuathiri sasa, hatuwezi kuishi kwa kukumbuka past all the time, na kusahau present.
 
Hpa hatuna upinzani WA kweli maana mpaka xx ambao hawalambi asali ni Tundu lisu,John Heche,God bless lema,John pumbalu,waliobaki wanalamba asali nikiwemo na mn
 
Ni bora uchaguzi usubiri katiba mpya kwanza hata ikizidi miaka mitatu
Katiba mpya itapatikana 2024, na Samia ataanza kugombea tena kwa awamu ya miaka kumi kwa katiba mpya, kwaiyo atamaliza 2035, hii mitano ya katiba ya zamani tunaifuta
 
Kwenye meza ya usuluhishi na mazungumzo ya mapatano, ogopa sana mtu mwenye ndimi mbili. Mtu akiwa "prescient, prejudiced, biased & having preconceived ideas" kwa maslahi ya chama chake na cheo, hawezi kwa vyovyote vile kuaminika kuongoza mchakato.

CCM imeonyesha rangi halisi waliyokuwa nao. Hawana dhamira njema juu ya mustakabali mwema wa taifa letu. Wao hufikiri neno "utulivu" lina maana sawa na lile la "amani".

Mfumo huchoka, taasisi huchoka, vyombo vya dola navyo huchoka, na hapo ndipo mwanzo wa mbeleko kuchanika. Siku yaja, nayo i karibu, chama hiki kikongwe kitasambalatika na kutokomea kabisa.
 
Huyo akimtukana Samia matusi ya nguoni, kumtukana mtu yoyote hata kama sio Rais ni kosa na unafungwa
 
Back
Top Bottom