Umadhubuti wa CCM unategemea upinzani imara

Umadhubuti wa CCM unategemea upinzani imara

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Joined
Jul 17, 2019
Posts
339
Reaction score
677
Udhaifu wa vyama vya upinzani nchini unatutisha CCM wajibu mkubwa sana wa kuwa kiongozi na mhimili mkubwa na wa pekee wa umoja, maendeleo na ustawi wa Watanzania wote, hata wale ambao siyo WanaCCM. Hilo ni jambo la kwanza muhimu la kuzingatia tunapotafakari haya maneno ya Mwalimu Nyerere yanayosema "BILA CCM MADHUBUTI NCHI YETU ITAYUMBA".

Jambo muhimu la pili ni kujiuliza iwapo hali ya kuwa madhubuti ambayo leo tunajivunia, inatokana kweli na CCM yenyewe kuendelea kuwa imara, au ni matokeo tu ya historia na udhaifu wa upinzani? Mfumo wa vyama vingi vya siasa unatoa fursa ya kuwepo uongozi mbadala, sera mbadala, na mikakati mbadala.

Vyama vya upinzani vinapokuwa dhaifu kiasi cha kuonekana na wapiga kura kuwa haviwezi kutoa sera mbadala, mikakati mbadala, na uongozi mbadala, Chama kinachotawala kitaendelea kurejeshewa madarakani, lakini si lazima kwa vile kina mvuto wa dhati, bali kwa vile hakina mbadala wake.

Ni rahisi kujisahau kwa mazingira ya namna hiyo; lakini ni hatari kwa Chama chenyewe na kwa Taifa zima.

Katika kuchambua hali na chanzo na umadhubuti wa CCM, tukione Chama kama mti. Mti madhubuti lazima uwe na vitu Vitatu ambavyo kila kimoja lazima kiwe madhubuti, na hapo ndipo hata tufani ikivuma mti huo unakuwa imara, hauwezi kung'olewa.

Kwanza ni mizizi. Mizizi ni historia yetu, ni urithi wetu, na kwa hiyo ni mwelekeo wa waasisi wetu na mfano waliotuachia. Hakuna mashaka kuwa mizizi ya CCM imezama na imekwenda mbali, na ni imara kweli kweli. Lakini hata mizizi hiyo nayo inastahili kunyweshwa maji na kuwekewa mbolea.

Idadi kubwa zaidi ya Watanzania ni vijana, ambao CCM haiwezi kuendelea kuwa na mvuto kwao kwa kuwasomesha tu historia ya CCM, na mchango wa waasisi wetu. Changamoto walizokumbana nazo wao, hata wakawa maarufu, ni tofauti sana na changamoto za sasa na kesho, ambazo ndizo hasa kipaumbele cha vijana.

Ninarudia. Tunayo mizizi imara, lakini lazima tuienzi, tuinyweshee, tuiwekee mbolea na kuifanya misingi tuliyoachiwa iwe na maana kwa vijana wa leo na kesho. Na hasa lazima viongozi wa leo waonekane wazi kustahili kuwa warithi wa waasisi hao.

Hakuna faida kujivunia urithi wa wazee wetu iwapo hatuigi na kuzingatia vigezo walivyotuwekea vya uadilifu, iwapo hatuwi na Uchungu wa nchi yetu kama wao, na iwapo hatuweki mbele maendeleo ya watu badala ya maendeleo yetu binafsi.

Leo tunaona CCM ni Chama chenye nguvu, lakini tusisahau kwa nini kina nguvu, na inabidi tufanye nini ili kiendelee kuwa na nguvu itokanayo na kukubalika kwa Wananchi, si kwa sababu tu za kihistoria au mabavu.

Hivyo hatua ya kwanza kama tunataka CCM kuwa madhubuti kweli, na si kwa vile tu wapinzani ni dhaifu, lazima turudi kwenye mizizi yetu, tuzingatie kwa vitendo urithi na maadili ya waasisi wetu, tuzidi kuwa Chama Cha wanyonge na kinachotetea wanyonge; si Chama kinachokuwa ngazi ya viongozi peke yao kuachana na unyonge, bali kinachokuwa chimbuko la viongozi wa kuongoza mapambano dhidi ya unyonge wa kila Mtanzania.

Na kisha lazima mizizi hiyo ijielekeze kwenye matatizo ya leo na kesho; isiwe mizizi ya fikra zilizoganda, bali fikra zinazokwenda na wakati. Uadilifu ni sifa nzuri ya kudumu; kinachotakiwa kubadilika SI dhana ya uadilifu, bali uadilifu katika utekelezaji wa sera muafaka katika kila zama.

Eneo la pili katika mfumo wetu wa mti ambalo ni muhimu kwa Chama kuwa imara ni shina. Na kwa mfano huo, shina ni muundo, taasisi na asasi za Chama, pamoja na jumuiya zake. Ni wazi CCM inaonekana madhubuti kwa vile ina muundo wake, na jumuiya zake, unaokifikisha Chama katika pembe zote za nchi yetu. Swali la kujiuzulu ni iwapo muundo huo, na taasisi hizo, ni madhubuti kweli au zinaonekana tu kuwa madhubuti kwa vile wapinzani hawana mfumo na mtandao kama huo?

Shina la mfumo na mtandao huo ni muhimu sana kwa Chama imara. Lakini muhimu pia ni kujua mfumo huo na mtandao huo unafanya nini hasa, na una maana Gani au mvuto gani kwa mwananchi wa kawaida, na hasa vijana wa leo na kesho?! Je, mfumo na mtandao huo ni kielelezo halisi cha sera za Chama na Ilani yake kinachoihubiri? Ninauliza hivyo maana ukweli ni kuwa Wananchi wanatuma kwa kigezo hicho.

Tunaposema CCM ni Chama Cha kijamaa, lazima ujamaa huo, kwa tafsiri yake ya sasa, uonekane wazi kwa Wananchi. Kama kielelezo chetu cha ujamaa ni ushirika, basi katika muundo na mtandao wa Chama lazima ionekane wazi kuwa ushirika ni sera ya CCM, tena kwa vitendo, si kwa maneno tu. Kama kielelezo ni uwezeshaji wa Wananchi kumiliki uchumi wa nchi Yao, hili pia lionekane wazi katika utendaji wa ngazi mbalimbali za uongozi wa Chama katika muundo na mtandao wake. Ionekane wazi kuwa Chama kinaelewa dhana hiyo ya ushirikishwaji, kinaelewa kuwa hiyo ni sera ya CCM, na kwamba kipo tayari kuelezea, kuiteleza na kuitetea.

Kama ujamaa maana yake ni kujali wanyonge, basi ionekane wazi kuwa hiki SI Chama Cha kukumbatia matajiri, bali hasa ni Chama Cha kutetea masilahi ya wanyonge, na kuwawezesha wanyonge kuachana na unyonge wao. Chama chenye historia ya ukombozi na Mapinduzi hakiwezi kuacha leo kuwa mkondo wa wanyonge kufikisha hisia, matatizo na mtazamo wa serikalini.

Ni namna gani muundo na mtandao wa CCM unaweza kutumika kwa masilahi ya wanyonge? Kwa mfano hivi sasa bado kama Taifa tunalumbana juu ya ipi ni Dawa sahihi ya kutibu malaria? 🦟 Tumesahau kuwa tiba sahihi ya malaria ni kuua mbu na kuharibu mazalio Yao. Na hili linawezekana kupitia mtandao wa CCM unaokwenda mpaka kwenye ubalozi. Kila Ubalozi, chini ya uongozi wa CCM na uwezeshaji wa Serikali, wakiamua wanaweza kabisa kumaliza mazalio ya mbu. Tuliwahi kufanya na tulifanikiwa huko nyuma. Tunashindweje leo kuongoza jamii kurudufisha mafanikio tuliyowahi kuyapata huko nyuma chini ya uongozi wa waasisi wetu?

Nimalizie sehemu ya tatu ya mti ambayo inahitaji kuimarishwa ni matawi, majani, maua na matunda ya mti wa Chama Cha Mapinduzi. Haya ndiyo sura, na hata jina la mti. Mwembe unaitwa mwembe kwa sababu unazaa maembe. Mwaridi unaitwa mwaridi kwa kuwa kwa kuwa unatoa maua ya waridi. Kielelezo cha Wema au ubaya wa Chama ni matunda yake, na sehemu muhimu ya matunda hayo ni viongozi wake; na tabia, mwenendo na matendo Yao. Tupende tusipende, viongozi wa CCM hukipa Chama sura, iwe sura nzuri au mbaya. UMADHUBUTI WA CHAMA HAUWEZI KUTOFAUTISHWA NA UMADHUBUTI WA VIONGOZI WA CHAMA.

Mwisho ijapo siyo kwa umuhimu, kila uchaguzi uwe sehemu ya kuimarisha nguvu ya CCM. Tusiendeleze makundi Wala tusikubali kuingia kwenye mtego huo wa upinzani. Tuendelee kujikosoa na kuimarisha uongozi wetu na kurutubisha uadilifu wetu kwa umma wa Tanzania. Hii itasaidia kuwanyima wapinzani hoja Yao ya kudai uongozi mbadala.

CREDIT "BWM", 2002
 
Hivi ni kwa nini CCM wanaiogopa sana CDM mpaka kufikia hatua ya kutumia serikali na vyombo vyake kuifanyia figusu sana...? Mara kesi ya Lembrusi, mara ruzuku ya Judge Mutungi, Mara uhaini, na mambo mengine yote...

Kwa nini ccm wasifuate utashi wa Rais Karume wa Zanzibar? Chadema nao ni Watanzania nao wanastahili kuongoza nchi hii kama nyie ccm au chama chochote- ili Watanzania wenzao nao wawapiwe kama wanatosha au la. Hata kama CCM inapendwa mpaka kububujikwa na machozi, kumbukeni, sote ni watanzania, uongozi wa nchi uwe kwa zamu , sio kila siku nyie tu. Mumechuja- period
 
Ule upinzani uliofichua Escrow na Dowans pamoja na madudu mengine yote sasa umetupwa nje. Santana wanajipakulia kwa Urdu wa kamba zao. Paka Handier Singh nae yuko mezani, mtu akiwa kununua kwa ma billion.

Watanzania wanalishwa habari za Simba na Yanga na Bongo flavour.
 
Unapoona Viongozi wa Chama Tawala na wale wa Serikali wanapopambana kuhakikisha upinzani haukui/hau imariki inaonesha Kuna ufisadi Mkubwa unafanyika na hawataki ufichuliwe
 
Vyama vya upinzani vinapokuwa dhaifu kiasi cha kuonekana na wapiga kura kuwa haviwezi kutoa sera mbadala, mikakati mbadala, na uongozi mbadala, Chama kinachotawala kitaendelea kurejeshewa madarakani, lakini si lazima kwa vile kina mvuto wa dhati, bali kwa vile hakina mbadala wake.

Ni rahisi kujisahau kwa mazingira ya namna hiyo; lakini ni hatari kwa Chama chenyewe na kwa Taifa zima.
Naunga mkono hoja, bila upinzani imara, hakuna CCM imara, hivyo CCM ina wajibu kusaidia Pre GE2025 - Wapinzani wa Tanzania wasaidiwe kuachana na siasa za kufikirika!
P
 
Ccm ni chama legelege na dhaifu kwa sasa, kimehakikisha mpinzani wa kweli CHADEMA kinapigwa pini Ili kupitisha udhaifu wao.
 
Chama kinachotegemea mbeleko ya vyombo vya dola, na hujuma dhidi ya vyama vingine, kisha kupitia hujuma hizo ndio kijione ni imara, chama cha aina hiyo kitakuwa ni cha majizi, wajinga ama vyote kwa pamoja.
 
Back
Top Bottom