Umaarufu!

shylock

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
604
1,000
Nikiwa form 1. Nilikutwa napiga chabo nyumbani kwa mwalimu. Mpaka kamaliza kaondoka 0-level nilijulikana kama mzee wa chabo
 

Kingsharon92

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
6,706
2,000
Nilikuwa bize na harakati zangu sipendi mazoea yakifala.

Wenzangu wakiwa mstarini Mimi Niko jikoni.. wakiwa wanasali Mimi Niko kwenye bustani ya shule.....

muda wa prepo mi ndio naoga .......

wakilala Mimi ndio nazurura kila chumba na kupiga chabo hosteli za mademu...

Daily Mimi ni mtu wa adhabu za mashambani manake class siiuwahi paelewa. Adhabu yenyewe kulima dakika 20 nimeshamaliza nakuwa na ticket ya kutoenda class.....

Nilikuwa na dili na mpishi wa skuli kwenye biashara ya mazao ya shule na bangi (kwa wateja wangu) niliwahi kamatwa ila niliitoka kesi kibabilon....

Nilikuwa sioni umuhimu wa ratiba manake Kama Ni class nilikuwa vizuri. Na nimemaliza na Division One Tena nzuri tuuu..

tukipewa kazi ya shamba ndio dakika mbili nimeshamaliza nawadere watoto wa mama.......

Cjawahi kuwa msafi kupindukia ule usarobaro wa O-level hata siku moja kwanza mashati nilikuwa naiba daily ya watoto wa mama, nikikuta nguo imefuliwa ikakauka ndio naitupia mwilini ikichafuka narudisha nilipotoa.....

Nilikuwa nakula sio utani aisee Yani mademu wakienda kumwaga msosi si unajua Toto za kishua Mimi natia nanga msosi. Kama wote kwangu.....

Ila nilikuwa mkimya watu wananijua ila Sasa kuanza kunisemesha ndio msala kwaiyo sikuwa na marafiki wa shule na hata Sasa (wale sijui best friend wa kufatana kila mahali)


Nilianza kupunguza udismainda baada ya kwenda advance...ila swala la kufata ratiba za watu zisizo muhimu siwezi hata siku moja

Sent using Jamii Forums mobile app
Uko wapi kwa sasa kwa tabia zako hizo unaweza kutufaa kazini
 

NYEKUNDU YA BIBI

JF-Expert Member
Oct 27, 2017
1,979
2,000
Kila mtu humu anasema alikua haingii darasani then anakua wakwanza
wazazi siku hizi hekima Hamna ndo maana vijana tunaitana wenyewe mzee baba tumewavua vyeo kisa huu uchuro wenu
acheni uongo nakujikweza kweza
kipumbavu nyie ndo mtakua waganga mkirudi maeneo mliyozaliwa
wazazi waongo duuuuh sijui mmesahau siku hizi watoto wamekua wajanja wanawachora tu na ujinga ujinga wenu

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Barn

JF-Expert Member
Feb 28, 2017
2,077
2,000
Msafi smart kemia na biolojia vililala hapa hadi nikawa naitwa mkemia pia nilikua naimba tulikua na group tukajiita black tigers nikapewa ukilanja mkuu O-level..

Wengi walinifahamu Mimi siwafahamu..


Advance umaarufu ulikua sababu ya kuimba na kuigalagaza sana biology
 

smaki

JF-Expert Member
Jan 23, 2019
1,113
2,000
Siku moja wakuu heeee!

Nilitoroka Shule katikati ya vipindi, baada ya kujichokea kusoma soma darasani all days of the week, hivo nikaamua kwenda zangu down town(Bukoba mjini), ili nipate ku spend some money of telegram money order, na kubadilisha mazingira kidogo. sasa nikiwa don town, kama kawaida nikaanza kula mitaa.

Mara ninywe soda dukani kwa mangi, mara chai ya maziwa kwa matoke pia vibaragara nk, ilimradi tu niko busy sehemu tofauti na niliyoizoea, ghafla bin vuuu!, Discipline master huyu hapa, uso kwa uso, nikawa sina jinsi ya kumkwepa kirahisi! duuu! nikajikaza , vichocheo vya kumbukumbu ya adhabu za kung'oa visiki na hamsa ishirini vikapenya haraka kwenye Medulla oblongata yangu, pyuuu,aaa!. up to this point there is no easy escaping route rather than pure deceiving tech. so bila kuchelewa wala kupepesa macho. Yaani direct eye contact baba mzazi.

Nikamuwahi kwa salaam ya kujipendekeza kama namjua vile, (sikutumia kabisa salamu ya shikamoo) na kujitambulisha kiaina kwamba nina mdogo wangu pale shuleni kwako, nikamuuliza kwa kumtaja jina kama anamjua, pia ana endelea vipi na shule kwa sasa , si akanijibu hajambo ana endelea uzuri!.

Basi ok! nikamwambia ampe salam zangu, pia nimem-miss sana, zaidi nikampa hela kidogo akampatie huyo mdogo wangu na hela nyingine kama bakhshishi yake as a teacher, alifurahi akanishukuru na kusema ''tuko pamoja mzazi''. akatokomea zake huyooo!,

Bila ajizi, nikaenda kunyoa para-zungu haraka bila kuchelewa hela si ninazo!. nikapandisha Shuleni, there after nikabadili nguo nikajichanganya haraka na wanafunzi wenzangu.

Asubuhi Teacher kanifuata, Tea breack time, hapo sasa nawaza sijui atastukia issue jamaa, but nikakauka kama simjui vile, Si kaniita kwa mkwara, (ndo alivyo kuwa mtu wa mikwarax2 sana). ''wewe Samaki! kuja hapa'',

Daaaa! hapo nika jiandaa ki saikolojia kubisha kama akinistukia.

Hamadi! anaanza kunipa salaamu kutoka kwa kaka yangu, na kumsifia alivo mstaarabu halafu tuna fanana ile mbaya na kuongezea utani Mama yako hajaiba nje, Finally akanikabidhi fedha taslim kadhaa nilizompa, kuonyesha si mchoyo wa fadhila nami nikamkatia kidogo, akashukuru akawa rafiki zaidi ya pale, maisha yakasonga.

na mwalimu akawa rafiki mkubwa,kupita maelezo. lakini sasa mwishowe huyu mwalimu sasa .............
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom