Umaarufu wa Mwanahalisi umeishia wapi?

mpayukaji

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
940
349
Siku za nyuma, ilikuwa haipiti muda bila kusoma habari za gazeti la Mwanahalisi kwenye JF. Hata hivyo, siku hizi halisikiki ukiachia mbali kuibuka utata juu ya ithibati yake. Je kulikoni Mwanahalisi au ni yale ya kila kipaacho hutua? Wapo wanaodai limeishatumbukia kwenye mifuko ya mafisadi kama magazeti ya Uhuru, Mzalendo, Tazama, Mtanzania, Rai hata Raia Mwema. Je hii ni kweli?
 
Hili gazeti la Udaku wa Kisiasa nilishaacha kulisoma longtime...
 
Frankly, Mwanahalisi ya sasa sio ile ya kipindi kile...SWOT analysis should be carried out within itself.
 
Mwanahalisi ni moja ya magazeti ya udaku ya Tanzania na linamilikiwa na mtu ambaye hadi leo hajui ni nani aliyemwagia tindikali.
 
Ukitaka kufahamu kuhusu mwanahalisi fanya utafiti juu ya nakala za gazeti hili zinavyouzwa kama kiwango chake kimeshuka basi tujadiliane lakini kama zimeongezeka tujadili pia.

''NO RESEARCH NO RIGHT TO SPEAK"
 
ukitaka kufahamu kuhusu mwanahalisi fanya utafiti juu ya nakala za gazeti hili zinavyouzwa kama kiwango chake kimeshuka basi tujadiliane lakini kama zimeongezeka tujadili pia.

''no research no right to speak"

hata magazeti ya kiu na risasi yanauzwa sana....!lakini nani wanaoyanunua?
 
ha wapi! Mimi nina nakala zote kwa miaka mingi sasa,halipiti ata nikiwa kwetu kule byelanyange.
 
hebu tuache ushabiki tuwe wakweli,ilifikia watu kutoa takrima kwa muuzaji ili akutunzie mwanahalisi lakini sasa hivi linapigwa na jua hadi linakutana na toleo la mbele bado unahitaji utafiti?penye ukweli tuseme.
 
mwaNAHALISI HALINA MPINZANI TANZANIA ANAYEBISHA MWAKA HUU NI WAKE KWA KUSUTWA KWA UMBEYA.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom