Elections 2010 Umaarufu wa Kikwete Mkoa wa Mbeya utatetereka?

Sifa za Mwakipesile ni hizi:
1. Akipewa majungu na mtu wake wa karibu huyaamini moja kwa moja bila maswali. Mtu yeyote atakayemwambia vinginevyo hakubaliani naye hata kidogo!
2. Kinyongo huwa hakiishi milele kwa mzee huyu! Ukipishana naye kidogo tu ndio imetoka hiyo! Amejaa visasi mzee huyu!
3. Ni mtu wa kujiongezea maadui kila uchao! Kwa mfano kama wewe ni rafiki wa adui yake maana yake na wewe ni adui yake, yaani umepita bila kupingwa kuwa adui yake!
4. Ni mtu wa makundi, sio wa kuunganisha watu ili kutafuta maendeleo! Ukiamua kupeleka maendeleo Mkoani Mbeya kama ni adui wa Mwakipesile yeye anahesabu kuwa hayo si maendeleo!
5. Mtu wake wa karibu akikosea humkingia kifua kwa gharama yoyote! Watu wa Mwakipesile kwake yeye Mwakipesile ni wateule, huwa hawafanyi makosa! Kosa kwa Mwakipesile ni kuwa kinyume naye, basi!
6. n.k.......
Huyo ndiye Mwakipesile, kipenzi cha JK, ambaye ni adui (yaani JK na Mwakipesile) wa maendeleo na umoja wa watu wa Mkoa wa Mbeya!

Bahati mbaya sifa hizo ni typical kwa asilimia ndogo ya watu kutoka Kyela, mbaya zaidi wengi wa hao huwa viongozi wa kati. Wanapojitokeza wenye sifa tofauti na hizo ni kweli kabisa huonekana maadui. Ndio maana Mwakyembe anakutana na adha kibao. Wapo wengi sana wapenda maendeleo kutoka Kyela, tena wakikusudia kufanya kitu sio wepesi kukata tamaa. Bahati mbaya sana mbegu mbaya hiyo ina nguvu kubwa sana ya ushawishi kwa watu wa kawaida kwani mbinu wanazotumia kutambuliwa katika jamii ni chafu na huenezwa kupitia vibaraka wachafu katika mazingira machafu. Kidogo kidogo Kyela itapata kikosikazi cha maendeleo ya kweli. Kunabadilika sana Kyela sasa hivi. Kuna haja ya wanakyela kizazi kipya kuunganisha nguvu na kuibadili dunia ya Kyela kwa kufagia mawazo ya aina ya Mwakipesile na wenzake.
 
Mkuu vipi aisee.........yaani unamsikitikia JK kupoteza umaarufu!!!..............yaani una matumaini kwamba JK atabadilika na kuleta maisha bora kwa kila mmoja wetu.............duh
Ha ha mkuu!
Hajamaliza zile safari na mi nataka aupate urais ili arekebishe uozo uliotengenezwa na mtandao wake.Give a man enough rope

to hang himself
 
............."ubusisya" ndio unaowamaliza nyie shemeji zangu..............hahahaha
 
Back
Top Bottom