Ulizaa na mke/kimada wa mtu, unampataje mwanao?

Ulizaa na mke/kimada wa mtu, unampataje mwanao?

Upo katika mahusiano na kimada wa mtu, baada ya miezi kadhaa unaona kitumbo kimetutumka lakini yeye hakwambii lolote kuhusu hicho kitumbo, na wewe kwakuwa unajua ana mtu wake maalum unaamua kukauka tu, siku zinaendelea kusonga mtoto anazaliwa, wakati huo wewe tayari ulishahama maeneo yale umeenda kutafuta maisha sehemu nyingine.

Mtoto akiwa na umri wa miaka miwili, watu wako wa karibu wanakwambia unafanana sana na mtoto wa aliyekuwa hawara yako, unapanga safari ukamuone huyo mtoto kweli kwa macho yako unaona mtoto anafanana na wewe lakini zaidi anafanana sana na Mama yako, unaamua kumtafuta Ex wako na kumuuliza kuhusu mtoto, anakwambia mtoto sio wako, wakati huo tayari umeshaambiwa kuwa Kuna mgogoro mkubwa kati ya Ex wako na mtu wake kuhusiana na huyo mtoto. Je unaweza ukachukua hatua zozote za kisheria dhidi ya huyu Ex ili akupe haki yako ambaye ni mtoto?
[/QUOTE
Visa vya namna hii viko vingi sanaa sikuiz hii hata mm ilishanitokea kuna demu nliwahi deti nae tena mara moja tu tukapotezana kuja kuonana anasema ana mimba yangu namm sina hiana nkakubali nkajapotea tena nkarud keshajifungua nkawa namuhudumia na mwanae sikutilia maanani sanaa maana nlikuwa naishi mkoa wa mbali so hata kurudi huko aliko ambako ndo home ni mara moja kwa mwaka au baada ya miaka miwili mtoto kafikisha miaka mitatu zikaanza zagaa tetesi huko kuwa yule mtoto sio wangu ana babaake tena kitaa hapohapo mamaangu akamtuma braza angu afatilie hilo swala maana mm sipo niko mbali braza akampata mpaka huyo jamaa inaesemekana ndo baba wakaongea japo mwanzo hakutaka kutoa ushirikiano ila baadae akafunguka yote kuwa mtoto ni wake ila aligombana na huyo demu baada ya yeye kubroke braza akanipigia kunambia alichogundua ila akasema yule mtoto alivyomwangalia na huyo jamaa basi huuliz mara mbili ukabd nitafute namba ya jamaa nkaipata kupitia kwa sister angu nkaongea nae bahati nzur yeye ananijua ila mm simfahamu nadhan sababu sikai sanaa kule tangu nasoma mpaka saiv nshakuwa mtu mzima akanipa mkanda mzima nkaemda FB kumchek jamaa baada ya kupata jina lake aisee kiukweli ni copy na mtoto nkampigia remu kumuuliza anaruka kimanga nkamwambia sasa kuanzia leo huyo mtoto hatapata huduma yangu yyte labda mpaka pale ntakapojiridhisha kwa DNA demu akaanza kujifanya kunitishia nkamwambia pimbi wewe nenda kshitaki hata mbinguni sio polisi tu ila huna chchte cha kunifanya baadae nkamlima tofali basi. Huko mkoani sijarud mwaka wa pili huu.
 
Achana na hiyo makitu bana,katafute mke uoe,achana na wake za watu bana.

Nani kakwambia kakwambia kwamba mbegu zako zimeisha hutazaa tena.
Hakuwa mke wa mtu mkuu alikuwa kimada tu, Kwahiyo niache mbegu yangu ipotee kwasababu nina mbegu zingine ?
 
Hakuwa mke wa mtu mkuu alikuwa kimada tu, Kwahiyo niache mbegu yangu ipotee kwasababu nina mbegu zingine ?
Ahaa kumbe hakuwa mke Wa mtu dai chako mkuu.
Anaweza akaja kuwa maarufu kama mondi.
Ila mtoa mada katoa mfano mzuri halo juu kuwa mwanamke anaweza akakunyima mwanao kisa tu anakuchukia akampa mwingine ambaye sio mwanae kisa tu anampenda.
 
Duuuuu!!! pole sana ,je ungekuwa unaishi na huyo mwanamke una ukagundua mtoto sio wako ,ungeruhusu aende kwa baba yake?
 
Alikuwa kimada sio mke,hata wazazi wake mwanamke wanadai hawajui kama binti yao ana mume
Sasa Kama jamaa ake alikuwa namhudumia sababu anajua mtoto ni wake na wewe hukujali wakati ana mimba leo mtoto ana miaka 2 mate yanakutoka je wakikupa mtoto akasema ni wako utamuhudumia mama na mtoto???? Au ndo kutaka mtoto tu mama abaki na shida zakee... Kama huwezi kumuhudumia mama yake tuliza kalio chini fanye maisha yako mengine huyo mama anaishi kupitia huyo mtoto wewe ulikojoa ukaondoka usigeuke nyuma.
 
Sasa Kama jamaa ake alikuwa namhudumia sababu anajua mtoto ni wake na wewe hukujali wakati ana mimba leo mtoto ana miaka 2 mate yanakutoka je wakikupa mtoto akasema ni wako utamuhudumia mama na mtoto???? Au ndo kutaka mtoto tu mama abaki na shida zakee... Kama huwezi kumuhudumia mama yake tuliza kalio chini fanye maisha yako mengine huyo mama anaishi kupitia huyo mtoto wewe ulikojoa ukaondoka usigeuke nyuma.
Ningemjali vipi akiwa na mimba hali ya kuwa hakuwahi kuniambia kuwa mimba ni yangu na wala hawajawahi kuniambia mtoto ni wangu mpaka leo hii?
Ndio nitamtunza mtoto Ila mama yake noo aendelee kuwa kimada wa jamaa
 
Nenda kajenge nyumba kwenye kiwanja kisicho chako kisha ulizia utaratibu wa kisheria.
 
Back
Top Bottom