Ulizaa na mke/kimada wa mtu, unampataje mwanao?

Ulizaa na mke/kimada wa mtu, unampataje mwanao?

Buzi Maarufu

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2019
Posts
422
Reaction score
330
Upo katika mahusiano na kimada wa mtu, baada ya miezi kadhaa unaona kitumbo kimetutumka lakini yeye hakwambii lolote kuhusu hicho kitumbo, na wewe kwakuwa unajua ana mtu wake maalum unaamua kukauka tu, siku zinaendelea kusonga mtoto anazaliwa, wakati huo wewe tayari ulishahama maeneo yale umeenda kutafuta maisha sehemu nyingine.

Mtoto akiwa na umri wa miaka miwili, watu wako wa karibu wanakwambia unafanana sana na mtoto wa aliyekuwa hawara yako, unapanga safari ukamuone huyo mtoto kweli kwa macho yako unaona mtoto anafanana na wewe lakini zaidi anafanana sana na Mama yako, unaamua kumtafuta Ex wako na kumuuliza kuhusu mtoto, anakwambia mtoto sio wako, wakati huo tayari umeshaambiwa kuwa Kuna mgogoro mkubwa kati ya Ex wako na mtu wake kuhusiana na huyo mtoto. Je unaweza ukachukua hatua zozote za kisheria dhidi ya huyu Ex ili akupe haki yako ambaye ni mtoto?
 
Yaani kwa uzinzi wako unataka kuvunja ndoa za watu?Kwa hiyo unataka mtoto ambae hujalea?Unaelewa kuwa Baba halisi na wa ukweli ni yule alielea mtoto na wala siyo yule aliekula starehe za ngono?Mimi ningekuwa ni huyo mume wa huyo mwanamke ningeiwinda hiyo tigo yako mchana kwa usiku!
 
kuna siri inayofichwaga milele juu ya mtoto? Kama sio mama ake jua jamaa zake au zako watakuja kumlopokea siku moja tu
Hata wakimropokea bado atatakiwa akapate ukweli kutoka kwa mama yake,na Kama mama ataamua kukomaa ndio basi tena
 
Pale ulipoamua kukauka wakati huyo Hawara ana mimba ndipo ulipoharibu
 
Huyo jamaa:
1.Amelea mtoto wako hadi kafikisha umri huo alionao sasa hivi.
2.Umemla mke wake.

Haya utayalipa vipi?
1:Nitatoa gharama za malezi ( Kama Sheria inaruhusu)
2:Hakuwa mkewe alikuwa hawara
 
Ukizaaa na mke wa mtu huwezi kumpata huyo mtoto kisheria ila baba wa mtoto anaweza kumkana inaruhusiwa ndani ya sheria..

Kwa kimada sheria haijasema maana hawataambuliki ko huyo ni wako moja kwa moja
 
Back
Top Bottom