Uliyeanza nae hutaendelea nae.

kwa niaba ya mods wa JF napenda kuwashukuruni sana kwa kujadiliana kwa ustaarabu bila mikwaruzano. mkiwezeshwa mnaweza.

asanteni kwa kuipatia hadhi JF.
 
mimi nafikiri hakuna ukweli kwenye mada ila mtu akiamua kuamini hivyo basi atavyunja mahusiano yake ya kwanza kutimiza imani yake
 
kwa niaba ya mods wa JF napenda kuwashukuruni sana kwa kujadiliana kwa ustaarabu bila mikwaruzano. mkiwezeshwa mnaweza.

asanteni kwa kuipatia hadhi JF.

halafu wewe si umeambiwa usimamie pms tu.
Ntakusema kwa mods.
 
it might be true or not swali la kujiuliza na wangapi humu stil wakowameo/wameolewa na wapenzi walianza nao?
 
Inawezeana sana tu mpenzi! hata mimi nimeolewa na mpenzi wangu wa kwanza
 
Hivi ni kweli mtu wako wa kwanza uliyeanza nae mahusiano ya mapenzi huwa hamdumu hadi kufikia ndoa?
Every Rule has an exception....., Ni kweli majority (sio wote) huwa hawadumu mpaka ndoa... Na sababu kubwa ni kutokuwa na uvumilivu ni vigumu kwa watu kukaa wote kwa muda mrefu, bila kuchokana..., sasa wengi huwa wanapata first boyfriend/girlfriend wakiwa lets say 18-20 sasa hawa wakikaa wote sanasana ni miaka mitano au saba by the time linakuja wazo la ndoa they are separated already.., wakati yule anayekuja wakati mume/mke yupo ready kwa ndoa hawakai sana wanawekana ndani.

Now boyfriend/girlfriend ni rahisi kuachana sababu hakuna any obligations sasa kama ndoa zenyewe nyingi hazidumu iweje wapenzi?

kwahiyo probably hata huyo mume wako atakayekuoa kama ungekutana nae 10 years ago uenda mgechokana na yule uliyekutana nae 10 years ago mgekutana mwaka jana huenda angekuoa, and probably 10 years from now kama sio obligation za familia huenda mtaachana (kama sio wavumilivu)..... Its Sad, But True...
 
mmmmmmmhhhh
akili imegoma dear
nipe muda wakufikiria samahaini sana mpendwa..
 
Mara chache sana hutokea either awe ndo kakutana mara ya kwanza na anataka kuoa jumla vinginevyo NGUMU
 
Inawezeana sana tu mpenzi! hata mimi nimeolewa na mpenzi wangu wa kwanza

Sawa dada lakini ulishatoka nje ya ndoa mara kadhaa, unakumbuka kisa na mkasa wako uliotusimulia humu JF (samahani kama nimekuchanganya na member mwingine).

Ndio maana msimamo wangu ni kuwa heri kuoa asiye bikira ambaye ameshaonja za aina tofauti kabla ya kuamua kutulia, licha ya kwamba nayo si guarantee ya uaminifu.
 
Dah!! Niko kwenye uhusiano wa mapenzi na huyu wa kwangu kwa muda wa miaka 10 sasa sijui tutaoana nikipata jibu nitarudi
 
Dah!! Niko kwenye uhusiano wa mapenzi na huyu wa kwangu kwa muda wa miaka 10 sasa sijui tutaoana nikipata jibu nitarudi

haya, mi nitasubiri feedback, wewe ni wa kwanza kwake au yeye wa kwanza kwako?
 
Ni kweli majority (sio wote) huwa hawadumu mpaka ndoa... Na sababu kubwa ni kutokuwa na uvumilivu ni vigumu kwa watu kukaa wote kwa muda mrefu, bila kuchokana

inawezekana kweli ila nashindwa kuelewa inakuwaje unamchoka binadamu mwenzio!
Kwanini hatuwachoki wazazi au ndugu zetu tunawachoka wapenzi wetu! Watu ambao ni wa karibu na tunaweza kushare kila kitu. Nini sababu hapo?
 
halaf wewe mbona hauhuzurii lab. siku hizi au ushapata kipedeshee kinakugaia hela za cafe? ,nikikukosesha razi utafeli ujue. kaz kwako.

tatizo siku hizi xperiments zinakushinda. Hadi mimi ndio nikufundishe. Lol!
Nitakuja leo tufanye revision.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom