Uliye nae sasa ndio wa ndoto yako?

Uliye nae sasa ndio wa ndoto yako?

flulanga

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2016
Posts
4,861
Reaction score
6,442
Habari wanajukwaa pendwa,

Mimi kwa mara ya kwanza naleta mada tuijadili sote, ila kama haitakuwa ngeni humu jukwaani mtaniwia radhi.

Mliopo kwenye ndoa au kwenye mahusiano ya mda mrefu, embu tuambizane huyo uliyenae ndiye aliyekuwa ndoto yako toka ulipoanza kujitambua au upo nae kwasababu amejitokeza/alijitokeza kipindi ambacho wewe ulihitaji kuingia kwenye mahusiano au ulikuwa nashida fulani kwahiyo ukaona umkubalie ili akusaidie shida zako au ulikuwa mpweke ndio akajitokeza akawa mfariji wako kwamda huo naukajikuta umezamia.

Hapa naongelea labda ulitaka boy/girl mwenye muonekano fulani, kiwango fulani cha elimu, kipato, kazi afanyayo, na dini yake ila kwa bahati mbaya ukajikuta upo na mtu ambaye hana kile kitu ulichokipa kipaumbele katika kichwa chako ila ndio hivyo upo nae, embu tuambizane.

Mimi binafsi nilihitaji sana nipate wadini yangu ila kwa bahati mbaya toka nimeanza kudoo sijawahi kumpata wadini yangu, nipo na mahusiano na wadini tofauti na yangu japokuwa amekubali kubadili dini ila najiona bado sijapata kile nikitakacho labda wangebadili dini familia yao yote ila ndio hivyo ishapenda.
 
Thank God nilie naye hakika ni chaguo langu .Yaani vitu vyooote nilikuwa namuomba Mungu anijalie mwanaume mwenye hizo sifa ndo Mungu amenipatia.kwa hakika nafurahia sana maisha ya ndoa.He is the best husband and best father to my kid.
 
Asilimia 90% ya wanaume huoa wanawake wa ndoto zao(kwa kuwa wao ndio hutongoza) asilimia 10%tu ya wanawake ndio huolewa na wanaume wa ndoto zao kwa kuwa hawana uwezo wa kutongoza wanaume wanaowapenda.
 
Nikueleze ndugu yangu hakuna ndoto kwenye kuoa au kuolewa. Katika uumbaji Mungu kufanya fumbo katika mambo matatu: kuzaliwa, kuoa/kuolewa na kifo. Huwezi kuwa na ndoto eti ni namna gani utakavyozaliwa, wapi na utazaliwa na nani. Pia huwezi kuwa na ndoto eti utamuoa nani, utaolea wapi na uta oa kivipi au utaolewa na nani na wapi halikadhalika kifo. Hivi vitu jua kwamba vipo katika maisha lakini you can't create a vision and mission about it ever because all are unpredictable and you can't measure . Unaweza ukawa na vision namna nyumba unayoitaka, gari, au kuwa Kiongozi au Rais.
 
Huwa inakuwa ngumu sana kumpata yule unayemtaka kwa sifa zote.
Ukibahatika utapata mwenye nyingi kati ya sifa unazozitaka ila nyingine hana.
Mwingine anazo chache sana katika unazozihitaji.
Cha msingi mimi nadhani ukimpata mtu ukaridhika naye jinsi alivyo inatosha.
Unawza ukapata mwenye kila sifa ila changamoto inakuja kwenye tabia zake
Mimi nikiridhika na niliyenaye inatosha
 
Habari wanajukwaa pendwa,

Mimi kwa mara ya kwanza naleta mada tuijadili sote, ila kama haitakuwa ngeni humu jukwaani mtaniwia radhi.

Mliopo kwenye ndoa au kwenye mahusiano ya mda mrefu, embu tuambizane huyo uliyenae ndiye aliyekuwa ndoto yako toka ulipoanza kujitambua au upo nae kwasababu amejitokeza/alijitokeza kipindi ambacho wewe ulihitaji kuingia kwenye mahusiano au ulikuwa nashida fulani kwahiyo ukaona umkubalie ili akusaidie shida zako au ulikuwa mpweke ndio akajitokeza akawa mfariji wako kwamda huo naukajikuta umezamia.

Hapa naongelea labda ulitaka boy/girl mwenye muonekano fulani, kiwango fulani cha elimu, kipato, kazi afanyayo, na dini yake ila kwa bahati mbaya ukajikuta upo na mtu ambaye hana kile kitu ulichokipa kipaumbele katika kichwa chako ila ndio hivyo upo nae, embu tuambizane.

Mimi binafsi nilihitaji sana nipate wadini yangu ila kwa bahati mbaya toka nimeanza kudoo sijawahi kumpata wadini yangu, nipo na mahusiano na wadini tofauti na yangu japokuwa amekubali kubadili dini ila najiona bado sijapata kile nikitakacho labda wangebadili dini familia yao yote ila ndio hivyo ishapenda.
wewe ni dini gani na umedoo na wangapi? maana wengine tushamaliza dini zote hadi freemason
 
Back
Top Bottom