Uliwahi kuisikia hii...!?

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
16,726
2,000
Nimo safarini...kiuchovu cha safari kimenisababisha ni uchape usingizi kidogo...ghafla na shtushwa na vicheko vikubwa vikubwa kutoka kwa abiria wote ndani ya chombo hicho cha usafiri.

Watu wako hoi kwa kicheko wakiwa wameshikiria mbavu zao...nami namuuliza jirani yangu kwenye kiti...kulikoni?

Huku bado anaendelea kicheka anasema" Una..unamuona yule kijana aliyesimama ameshikilia bidhaa mkononi?"
Nami namjibu "Ndiyo"

Jirani anaongeza" Yule kijana anasema anauza sabuni za kisasa kabisa kuwahi kuuzwa hapa dunia, sabuni hizi zinasifa kuu moja, ambayo ni kuwa SABUNI HIZI ZINAONGEZA HAMU YA KUOGA"

Pale pale nilivunja mbavu yangu moja kwa kicheko, na mbavu ya pili iliteguka, zilizobaki zilipata msituko....!!!

Ndiyo maana ninakuulizeni uliwahi kulisikia hili la sabuni kuongeza hamu ya kuoga?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom