Ulishughulika vipi na kisa cha namna hii?

Mkuu, huyo demu hakupendi, sikiliza maneno ya rafiki yako. Just kula mzigo then move on. Huyo demu anajifanya kukutafuta kipindi hiki kwasababu mapenzi aliyoinvest miaka hiyo yaliishia shimoni. Believe me, atakusumbua sana ukimpa moyo wako.

Kwasasa hana cha kufanya kwasababu hana mtu wa maana anayempenda kwa dhati thats why amekutafuta wewe bwege mtozeni wake. Akipata anayempenda kwa dhati hatofikilia hata kwa dakika kukuacha!

Hayo yalitaka nitokea mie though kwangu mie ni tofauti kidogo. Maana mie alinikubalia, bahati mbaya yeye alifeli na mie nilifaulu. Nimpenda sana and so sikujali ufaulu wake. Niliendelea n advance yeye akaenda veta. Alianza leta usumbufu wa kutopokea simu na kujibu hovyohovyo. Nikaamua kumsahau. Kaja nitafuta nikiwa naingia chuo mwaka wa kwanza, mixer anapiga simu mpka kuniuliza kama nimekula, offcourse moyo ulitaka niendelee naye pale tulipoishia but akili ikakataa.

Nimemaliza chuo ikabidi nimchane live tu kuwa siwezi kuwa naye maana alishapoteza chance yake kipindi kile nipo shule, afterall alishazalishwa na jamaa haeleweki kama atamuoa.

Take care chief.
 
Changamoto yangu kaka ni Je, tutaishi kwa upendo maana sijui kama kweli kaja kunikubali kwa moyo mkunjufu au la !!!
Kakukubali bahati mbaya..
Maana am sure she wasn't single mlivoonana Makumbusho.
Ila umetokea wa ahueni ya alienae mda huo. Si ajabu pia anapima kwanza kuona ka bado unamshobokea ka mwanzo. Akicomfirm tuu umo basi gwaride litaanza(kukutesa)
 
Form 5, alikuwa bado ana akili za kitoto...na kwa kuwa unataka mke basi mpe nafasi, mkaribishe, mtoke muende sehemu iliyotulia ya wazi (siyo kwako wala lodge) umsikilize, mdadisi na pia ujaribu kuuliza kwa waliosoma udsm tabia zake n.k...sikushauri kumla bila kujua historia yake tangu mlivyomaliza form 6. Sikushauri kabisa kumla kama ataanza kujirahiisha ili umtie siku ya kwanza kukutana.

Kuhusu kuliwa sana hiyo ni kawaida, kwa wanafunzi wa chuo, wakimaliza chuo wanakuwa wamechapika kweli kweli hasa kama alikuwa ni slay queen, ila siyo wote.

Mahusiano ya shule na chuo kwa asilimia kubwa hayana clarity in terms of future, things don't work out, you move on...haina makombo. Ila onyo usimle bila kumfahamu vizuri
 
Ushari mzuri
 
Prisca alikuwa sahihi kukukataa akiwa kidato cha tano na sita.
Kwa sasa acha awe rafiki kwanza, kama kuna masahibu yoyote yametokea utajua tu.
Si sahihi kumhukumu mtu mzima kwa makosa aliyofanya akiwa mtoto.

Awe rafiki kwa sasa.

Kama utaona kuna sababu ya kuanzisha mahusiano basi kila la kheri
 
mchunguze kwanza historia yakr ana kazi? sasa hiv ana maon gan kuhusu maisha?
vip amedhoofu labda?
mchek kwanza na ummulize kipind kile ilikuwaje kuwaje.
usichape kabla ya ndoa shaur yako.mchuma janga utakula na wa kwenu
 
[emoji817] [emoji817]
 
Hili suala lipo""" Nami nilishawah kataliwa sana kipindi cha nyuma huko"" 2014 hiv!!! Nilimpenda mno jacky!!!
Nakumbuka niliwah kumbembeleza day 1 hivi""" mchana mpka nilipiga magoti na machoz!! (Stend ya mabas ilikua)

Kisa alikua ki"chuo flan hiv! Afu mi msela wa mtaan!! Yaan sio type yake
Kmmk!!!!!!! Kimaelezo kutoka kwake""

Mkono wangu wa kushoto nilichora jina eruf! Ya kwanz ya Jina lake" kwa kutumia wembe"""" damu iliruka aswaa"" ajabu sasa"" wala akustuka zaid ya kusema nitolee uchuro wako hapa""""

Jack"" huyu alisababisha nionekane fala kwa ndugu zangu wote"" [emoji26] baada ya kugoma kula kwa siku 2 mpka nguvu zikaniisha"""

Mkuu nilipambana mnooooo......
Kusaka life kwa hasira"
Japo sina elimu kubwa...naishukulu serikali iliniona"" nikala shavu upande mmoja hivi;;;;;

Nilikutana nae 2019 hapo Nov""""alinitunuku nilimla na"kumuacha mkuu"" japo analia lia sana kweny social net!!!......to be cont.....
 
Bila shaka yupo wa moyo wako ambaye unamfuatilia kabla hujaonana na 'Prisca' hiyo juzi. Kama kweli yupo basi shikilia na endelea kufuatilia ujiridhishe ukiwa na nafasi na uhuru wa kufanya maamuzi sahihi.

Prisca wa stendi ya Makumbusho siyo yule wa kipindi mko shule. Kumbuka alikukataa wewe pamoja na vitu vingine ni kwamba alishakuwa na uliyemtaja kuwa ni monitor wenu na si kwamba alikukataa kutokana na kuhofia kuharibu 'shule'. Baada ya monitor ni mdosi gani alishikilia chombo hadi sasa apate wazo la ghafla kukukumbuka? Hala hala mti na macho kaka. Na kuna uwezkano mkubwa maamuzi utakayo chukua hivi sasa ambapo hata nafsi yako inagoma si tu kukubaliana na hali halisi unayoiona bali hata kuamini kinachojiri basi maamuzi hayo yanaweza kubeba majuto kwa siku za usoni maana haukujiandaa na hili kipindi hiki. Hujui kabeba nini SIRINI mwake/mwilini mwake ambacho anataka kukitua kwako.

Naamini ingekuwa anakupenda kweli asingesubiri mapenzi hayo ayaoneshe kwa tukio la ghafla hapo stendini bali angefanya namna yoyote kukupata kwani kwa vile nyie mlifahamiana mkiwa shule ni kwamba mna mtandao wa 'classmates' kwa hiyo hata asingeshindwa kupata mawasiliano yako. Je, msingekutana hapo stendini ingekuwaje?

Pamoja na haya yote tunayoyaandika kuchangia kwenye mada yako wewe ndiwe pekee MUAMUZI WA MWISHO. Ila ukumbuke kuwa kosa moja goli.

Asante
 
Kwani wewe mleta mada, ujawahi kuwakataa mademu waliokupenda ila baadae ukagundua wako fire kinyama
 
Hiyo haraka ya Prisca ina walakini mwingi mno.

Nenda naye taratibu inaonesha ana stress sana na mahusiano aliyonayo au aliyowahi kupitia.

Muda unaofikiri upo salama ndiyo huwa wa hatari zaidi.
 
Afate huu ushauri
 
Kwa niaba ya rafiki yangu danny napenda kuwashukuruni nyote kwa ushauri wenu naahidi tutaufanyia kazi na mambo yataenda sawia mi ni kishoro mshikaji wake mtoa maada. Hatuhitaji tena ushauri imetosha. asanteni sana
Asante kwa kumuwakilisha. Yule jamaa (Kishoro) hanaga muda wa mitandao. Anasemaga mitandao inaweza vunja ndoa yake😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…