Ulishawahi kusingiziwa kitu?

Nilisingiziwa kisawasawa na spicy señorita mmoja kuwa natoka naye na tumeshibana.
She had confessed some feeling about me, before that, but i was like meeh.
Basi mi nikaona sio mbaya tu-spend tha night moja matata, af tu-call it a history.
Long story short, lets just say, THAT NIGHT WAS A MISTAKE aisee.
Kashfa hiyo ilichukua muda mrefu kuisha huku ikiambatana na drama kibao.
I couldnt reverse shit!
But I learned my lesson kwamba some women sio wa kuwachezea feelings. Hands down!
 
mimi kuna mtu alinisingizia mambo mengi tu hiyo ni baada ya kumfuma kwenye tank langu anaiba maji na hapo tulikuwa tumenuniana nikaamua kumshtak kwa mwenye nyumba wacha anishuhudie uongo ambao hata sikuwah kuuona dunia hii kubwa zaid akanisingizia natembea na mumewe jaman wakat huyo kaka hata mazoea nae sina yan nilikasirika nilimbamiza pale pale mbele ya kikao cha watu wanne!!! had leo adabu na heshima @sitakag ujinga mimi usio na maana
 
Kusingiziwa kupoo, mfano mimi navyokusingizia mleta uzi wewe ndio chanzo watu wana chat badala ya kupiga kazi
 
Daah hapoo kwa kumuibia mume tenaa..!! Sema usingempigaa wew ungefanya kweli sasa...
 
Daah! Aisee nilishawahi singiziwa kitu cha ajabu sema nimekisahau ningewambia.
 
Mchumba wa Rafiki yangu alikuwa ananitaka Kimapenzi nilimkatalia na ''kumtolea macho'' kwa hasira........ akaniomba yaishe na nisimueleze yeyote hatarudia tena............Ikafika wakati wanafanya Sendoff yake wakati tunatoa zawadi kwa bibi Harusi Mtarajiwa.......Nilipompa Mkono wa kumpongeza....................Eeeeeeeeeeeebwanaeeeeeeeee aliangua Kilio huku akisema Nimemfinya.........Nilitolewa Nje Mzobemzobe nilivunjiwa heshima siku ileeee sitasahau maishani.............................!!!!!!
 
Daah maskini... sasa umemfinya mpaka akalia!??? Duuh visa hivi
 
Pole
Hakuna kitu kinaumiza kama kusemewa uongo, ingawa wengi husema ukweli unauma, kwangu uongo huniumiza zaidi.
Mmh. Unatabia mbaya wewe. Yaani umesahau kabisa ile njia ya kuja kwangu vibaya hivyo shoga yangu.

Mzima?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…