Ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo katika maisha yako?

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,226
2,000
Ndugu zangu tunaishi katika dunia ya hatari sana. Chuki, wivu, hasira, uroho, urafi, wizi, kusingiziana imekuwa sehemu ya maisha yetu.

Hakuna kitu kinaumiza moyo kama kusingiziwa jambo la uongo ambalo hujalifanya au kujaribu tu kulifanya. Binafsi nimewahi kusingiziwa jambo la hatari sana, tena na ndugu zangu kama siyo busara ya watu fulani hivi ningepotea kabisa.

Tukio hili sitalisahau maisha yangu yote. Nilijetanga nikaishi maisha yangu. Nilisamehe lakini sitasahau.

Je, wewe ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo?
 
Mwifwa

JF-Expert Member
Apr 3, 2017
38,853
2,000
Nilisingiziwa nimekata mtama(mmea) nikala muwa na mama mdogo, bi mkubwa alipopata taarifa alinishushia kichapo. Ilikuwa utotoni(around 8yrs).

Unyayo uliangaliwa wakazani ni mimi wakati haikuwa mimi na sikujua alikuwa nani. Kitendo hicho cha kusingiziwa sijawahi kukisahau hadi leo na huwa nasikitika sana kwa kosa ambalo sikulifanya.

Yapo mengi ila hili ni miongoni.
 
Pole Sana.
 
STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
6,752
2,000
Kuna demu baba yake alikuja kunifokea sana mbele za watu akaniambia mwanawe namchukua, mzee alikua na hasira sana kwa jinsi maneno mazito yalivyokua yakimtoka bibi wa mtoto akaingilia kati akawa anamgomba baba wa mtoto kuwa aache kunifokea, mm sijawahi kuwa na mahusiano au ukaribu na huyo mtoto, kulikua kuna mshkaji ndie aliekua anakula sana huyo mtoto ubaya mtoto kadata kwa huyo mshkaji, nilijiskia aibu kubwa sana kinachoniuma zaidi sihusiki na kumchukua huyo mtoto hata kumtania

Mara ya 2 pia kwa mwengine ni story ndefu

Kusingiziwa kubaya maana bora jambo ulitende kuliko kusingiziwa
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
45,462
2,000
Nilisingiziwa nimekata mtama(mmea) nikala muwa na mama mdogo, bi mkubwa alipopata taarifa alinishushia kichapo. Ilikuwa utotoni(around 8yrs).

Unyayo uliangaliwa wakazani ni mimi wakati haikuwa mimi na sikujua alikuwa nani. Kitendo hicho cha kusingiziwa sijawahi kukisahau hadi leo na huwa nasikitika sana kwa kosa ambalo sikulifanya.

Yapo mengi ila hili ni miongoni.
Ulikula mboko za standard geji πŸ˜…
 
Extrovert

JF-Expert Member
Feb 29, 2016
45,462
2,000
Ndio mkuu.

Mara nyingi wazazi hawajiridhishi na kosa, wanatoa adhabu wakizani wanadanganywa endapo akianza kujitetea. Athari yake endapo mtoto asiposahau hiyo adhabu inakuwa ni jambo jingine jipya
Heheheheh lazma upotezee tu
 
Santos06

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
2,149
2,000
Ndugu zangu tunaishi katika dunia ya hatari sana. Chuki, wivu, hasira, uroho, urafi, wizi, kusingiziana imekuwa sehemu ya maisha yetu.

Hakuna kitu kinaumiza moyo kama kusingiziwa jambo la uongo ambalo hujalifanya au kujaribu tu kulifanya. Binafsi nimewahi kusingiziwa jambo la hatari sana, tena na ndugu zangu kama siyo busara ya watu fulani hivi ningepotea kabisa.

Tukio hili sitalisahau maisha yangu yote . Nilijetanga nikaishi maisha yangu. Nilisamehe lakini sitasahau.

Je wewe ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo?
Ndio maisha
 
danielhipoliti

JF-Expert Member
Jun 8, 2015
677
1,000
Nipo form one, dawati la mbele kbsa teacher (Madam pisi kali) wa English anafundisha nipo na mwanangu J akajamba teacher kauliza ni nani jamaa kaninyooshea kidole

Teacher anasema hata ufanani dah niliona soo sna alaf nina tabia flani ya upole enzi izo
 
The Monk

Platinum Member
Oct 12, 2012
16,891
2,000
Kuna jambo unaweza ukasingiziwa ukajikuta unakosa kabisa cha kufanya.
Kuna watu wanaweza kukusingizia jambo ukabaki unajiuliza maswali yasiyo na majibu.

Nikakumbuka kuna jamaa aliniambia silaha wametengenezewa binadam, sio wanyama. Tokea siku hiyo, naenenda na watu kwa step za kunyata na umakini wa hali ya juu sana. Nimeshakua Bepari, ujamaa hakuna tena, bora lawama.
 
KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
19,143
2,000
nishawahi pindishiwa maneno kosa nilifanya ndio lakini njia ya ufanyaji ikakolezwa! Yani mi hela ndio niliiba ila nikaambiwa ati niliiba kwa kupiga mtu kabali..πŸ˜‚

Baba wa rafiki yangu nae akasemaga kuna manzi fulani natoka nae kumbe mwanae ndo anatoka nae!,akanikandia mbele ya familia yake aisee nilibisha huku nikiwa very comfortable aibu ikaamia kwake ila sikumwaga mchuzi kumchomesha jamaa yangu..

Kwa hulka niliyonayo ngumu kidogo kunisingizia maana kabla sijajitetea kama Kuna wanaonifahamu wanaweza kunitetea au hata ndani yako tu kunaweza kuanza kunitetea!. Kenzy wa jf ni mtundu ila nje na hapa kenzy ni mpole si kenzy kiberenge au komamanga..🀣
 
Minah

JF-Expert Member
Dec 23, 2018
740
1,000
Kuna Mschana alinisingizia nimemtukana matusi WhatsApp!! Eti alinitumia msg kunisalimia mimi nikamtukana matusi.. Yaani hadi Leo roho inaniuma sana, Hao walionipa Habari hizi huwa nawaambiaga wamuombe Screenshots za ushahidi km kweli katukanwa! ila mpk Leo Kimyaa.
 
The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,226
2,000
nishawahi pindishiwa maneno kosa nilifanya ndio lakini njia ya ufanyaji ikakolezwa! Yani mi hela ndio niliiba ila nikaambiwa ati niliiba kwa kupiga mtu kabali..

Baba wa rafiki yangu nae akasemaga kuna manzi fulani natoka nae kumbe mwanae ndo anatoka nae!,akanikandia mbele ya familia yake aisee nilibisha huku nikiwa very comfortable aibu ikaamia kwake ila sikumwaga mchuzi kumchomesha jamaa yangu..

Kwa hulka niliyonayo ngumu kidogo kunisingizia maana kabla sijajitetea kama Kuna wanaonifahamu wanaweza kunitetea au hata ndani yako tu kunaweza kuanza kunitetea!. Kenzy wa jf ni mtundu ila nje na hapa kenzy ni mpole si kenzy kiberenge au komamanga..
Haaaaa,haaaaaa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom