Ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo katika maisha yako?

nishawahi pindishiwa maneno kosa nilifanya ndio lakini njia ya ufanyaji ikakolezwa! Yani mi hela ndio niliiba ila nikaambiwa ati niliiba kwa kupiga mtu kabali..

Baba wa rafiki yangu nae akasemaga kuna manzi fulani natoka nae kumbe mwanae ndo anatoka nae!,akanikandia mbele ya familia yake aisee nilibisha huku nikiwa very comfortable aibu ikaamia kwake ila sikumwaga mchuzi kumchomesha jamaa yangu..

Kwa hulka niliyonayo ngumu kidogo kunisingizia maana kabla sijajitetea kama Kuna wanaonifahamu wanaweza kunitetea au hata ndani yako tu kunaweza kuanza kunitetea!. Kenzy wa jf ni mtundu ila nje na hapa kenzy ni mpole si kenzy kiberenge au komamanga..

komamanga
 
Nilisingiziwa situmii pombe wakati mezani zipo vitu claasic aisee iliniuma sana
 
Tuliosingiziwa kisha tukafanya kweli tunaweza kuchangia???
 
Nilpanda lift nikakuta inanuka ushuz!!!! Nikakomaa hvo hvo ile floo:: ilofatia wakapanda mademu 3...


Daa waliniangalia jicho baya kuwaambia ukweli nikashindwa!!!

Mweeeh kusingziwa kubaya nyie!!!
(LAPF Tower!!!!!)kijitonyama:
 
Ndugu zangu tunaishi katika dunia ya hatari sana. Chuki, wivu, hasira, uroho, urafi, wizi, kusingiziana imekuwa sehemu ya maisha yetu.

Hakuna kitu kinaumiza moyo kama kusingiziwa jambo la uongo ambalo hujalifanya au kujaribu tu kulifanya. Binafsi nimewahi kusingiziwa jambo la hatari sana, tena na ndugu zangu kama siyo busara ya watu fulani hivi ningepotea kabisa.

Tukio hili sitalisahau maisha yangu yote. Nilijetanga nikaishi maisha yangu. Nilisamehe lakini sitasahau.

Je, wewe ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo?
Na sisi tuliosingiziwa tumejamba kwenye daladala tunaweka reply hapa?
 
Ndugu zangu tunaishi katika dunia ya hatari sana. Chuki, wivu, hasira, uroho, urafi, wizi, kusingiziana imekuwa sehemu ya maisha yetu.

Hakuna kitu kinaumiza moyo kama kusingiziwa jambo la uongo ambalo hujalifanya au kujaribu tu kulifanya. Binafsi nimewahi kusingiziwa jambo la hatari sana, tena na ndugu zangu kama siyo busara ya watu fulani hivi ningepotea kabisa.

Tukio hili sitalisahau maisha yangu yote. Nilijetanga nikaishi maisha yangu. Nilisamehe lakini sitasahau.

Je, wewe ulishawahi kusingiziwa jambo la uongo?
kuna jambo nilisingiziwa baya mno sijawahi kumchukia binadam yeyote lakini huyu dada nimeshindwa kabisa huwa sitamani hata kumuona,,,namchukia.
 
Nilishawahi kusingiziwa wizi.Duh!yani asikudanganye mtu tuhuma kubwa kama hizo,unabaki unaduwaa,maneno huna,hata kujitetea unashindwa,alafu unazidi kuonekana una guilt
 
Nilishawahi kusingiziwa wizi.Duh!yani asikudanganye mtu tuhuma kubwa kama hizo,unabaki unaduwaa,maneno huna,hata kujitetea unashindwa,alafu unazidi kuonekana una guilt
Acha tu mi nilidhalilishwa sana mbele za watu wakati sijawahi kuiba kisa tu nilionekana nafanania kuiba maana kwetu masikini halafu nilikua nmeenda kwenye sherehe kwa ndugu zangu madon ni fedheha kubwa sana ila Mungu alishaga ijibu mpk leo wanaonaga aibu sana mbele yangu japo mi nilishaga samehe
 
Ilikua shule moja mkoani kilimanjaro , niliahamia pale nikiwa form 5 . Nikakaribishwa na jamaa yangu mmoja niliesoma nae o level mkoani dsm. Akanitafutia chaga tukaweka kwenye kitanda nikawa nakaa nae room mmoja, kwenye hiyo room nilikutana na jamaa wengine wawili kutoka dsm,na mmoja kutoka moshi miezi ya badae alikuja kuongezeka mwingine kutoka arusha, basi jamaa wa mule room walikua watu wastory saana. Inafika kipindi unakuta jamaa wamejaa kutoka room nyingine kuja kupiga story mule.

Sasa mimi nilikua na ule ukorofi wa kuchezea chezea umeme nikawa nimetengeneza extension ya kandambili nikaweka waya nikaunga kwenye taa ya room, tukawa tunachaji simu pale. Wakawa wanakuja washkaji kibao kutoka room tofauti kuja kuchaji pale ,

Siku moja akaja jamaa mmoja yeye alikua anatokea mkoa wa dodoma akaja kuchaji ilikua ijumaa mida ya saa mbili usiku, ameweka simu ikamzingua kupitisha moto akaniita nikamsetia ikakawa inapitisha moto mimi nikaenda zangu prepo nikamuacha pale.

Siku ya jumamosi kesho yake tulikua na mechi na shule moja ipo moshi mjini nikawa nimepanga niende kwenye hiyo mechi kama mshabiki,
ile mechi kufikia saa tano usiku ikawa imeahirishwa na mm nilikua nimeshatoa taarifa kwa ndugu zangu wa town kuwa nitaenda walau nikabadilishe hata ladha ya msosi.

Basi jmosi mapema mida ya saa mbili mimi na jamaa yangu mmoja wa mule mule room yeye mwenyeji wa pale pale moshi tukawa tumeondoka.

Sasa asubuhi yule jamaa aliyeiacha simu mule room kuna watu kama watatu akawa amewaambia kuwa amepoteza simu, alipotoka prepo aliipitia pale alipokua anachaji ila hakumbuki aliiweka wapi.

Ilipofuka mida ya saa nne yule jamaa akagundua kuwa mm na jamaa mmoja wa mule room tumeenda town, jamaa akaanza kutangaza kuwa sisi tumemuibia simu na tumeenda kuiuza mjini.

Akamfuata HP na bahati mbaya ile shule ilikua na ubabe wa kipekee, viongizi wananguvu kuliko hata waalimu wakati mwingine katika mfumo wa kiutawa baina yetu, basi ukijumlisha mule room huwa tunaonekana wajanja wajanja wengi wametoka dsm jamaa wakapigia mstari kuwa hiyo simu sisi ndio tumeibeba, karibia viongozi wote jamaa akawamezesha sumu mpka kufikia mchana story ilikua ni kwamba kuna madogo kutoka bweni X room Y wameiba simu wameenda kuiuza mjini.

Wanafunzi wakakaa kikao kutujadili wakafikia hitimisho kuwa tukirudi watuite watuadabishe.


Nikiwa town nikawa napokea simu kutoka kwa washkaji kwamba kuna simu ya mtu imepotea na sisi ndio imegundulika kuwa tumeichukua.

Mimi nikawa nachukulia kawaida sana na wala sikua na hofu kabisa yani sikutilia maanani.

Ebana nikarudi jumapili usiku nakuta shule jina langu limechafuka "mwizi wa simu" daaa.

Pale ndio nikaanza kupata picha ya nini kinaenda kutokea juu yangu, maana mpaka washkaji tuliowaacha mule room nilihisi kabisa na wao wameamini kuwa simu tumeichukua sisi.

INGAWA KI UKWELI SIMU SIKUCHUKUA/HATUKUCHUKUA.

Basi j,tatu HP akaniita ofisini kwake. Jamaa alikua amenizidi umri mbali ki aina alafu alikua na mwili fulani wa kibabe mimi nikisimama nae naonekana kadogo fulani hivi. Basi jamaa akaniambia dogo hapa shuleni yanapotokea maswala ya utovu wa nidham huwa tunamalizana wenyewe wanafunzi na moja ya adhabu ni kupigwa stick , (six stroke) ukiwa umefungwa macho. Ila cha kukusaidia wewe na mwenzako jichangeni mumlipe jamaa hela ya simu yake mambo yaishe.

Mimi nikamwambia siwezi kulipa sababu sijachukua hiyo simu na sitolipa.

Mwenzangu nae alivyoitwa akakaza kuwa hawezi kulipa sababu hajui chochote kuhusu simu wala mambo ya kuchajisha simu mule room.

Mpaka hapo ikaonekan mm ninaechajishia watu simu ndio niliibeba hiyo simu ya jamaa.


Asikwanbie mtu roho iliniuma saaan. Huwa kuna watu walikua wanakuja wanakuomba kwa kukunyenyekea kwa huruma uwachajie, unawachajia. Sababu ilikua ni very risk kuchajishia simu mule room na inamaana tulikua tumejiweka rehani wote .

Mpaka kufikia hapo jumba bovu lote lilikua limeniangukia mm.

Daaa ilikuaga ikifika jioni tunakuaga tumejikusanya vikundi vikundi tunapiga story kusubiria msosi ila kipindi kicho nilikua alone jamaa ambae nilikua naongea nae vizuri ni yule aliyenipokea tuliesoma nae dsm tu. Wengine wote room wakawa hata story wanakaa mbali.

Nilijihisi mpweke saana , nilihisi sitoiweza tena shule. Mbaya zaidi ni nani nimwambie kuwa mm sijaiba hiyo simu aelewe ajue ukweli ndani ya moyo wangu.

Basi baada ya HP kuona kuwa hatuna uelekeo wa kukubali kuwa tumeichukua hiyo simu na tumegoma kulipa, wakapanga ijumaa ya wiki hiyo usiku watuite kwenye bweni moja tukapigwe.


Kiufupi hiyo wiki nilidhoofika sana, sikujua nifanye nini kila ninaepishana nae nilihisi ananichulia mm ni kibaka mzoefu,
Kila wakati movie ya YESU ilikua inanijia akilini, yaani naenda kusulubiwa kwa kitu ambacho sijakifanya.

Ijumaa ikafika usiku tupo prepo jamaa wakakusanyika wote ilikua muda wa prepo, lakini wa class letu hawakuitwa kwenye mkusanyiko huo

Ila baadae walitawanyika bila mimi kuitwa sijui sababu ilikua ni nini lakini nadhan yule mwenzangu nilieenda nae town alikuwepo yeye alika anasoma art mm science, na combination nyingi zilikua za arts kasoro mbili. Na mpaka kufikia nyakat hizo mm na huyo jama zikawa haziapnd kiviile ingawa tulikua room moja.


Basi niliporud room nasikia story za chini chini kuwa kesho yeke yani jmosi ndio naadhibiwa, na sio tena tunaadhibwa mm na jamaa yangu.

Jmos ikafika sikuitwa, basi washkaji mule room wakawa wananitania kuwa mwana una mungu,,,

Wiki ikaisha sina hili wala lile ijumaa mida ya saa mbili HP akanifuata akanipeleka bweni moja hivi nadhan kama sjakosea lilikua linaitwa Lumumba au Nyerere ,
Ebana nikakuta watu wamejaa kibao wamebeba vipande vya chaga za kitandana fimbo lakini wanafunzi wa darasa langu la science hawakuwepo.


State yangu katika kipindi hiki naijua mimi na mungu wangu.


HP akawaambia

Oya tusikilizane yule dogo alieiba simu huyu hapa na kama ilivyo kawaida yetu anatakiwa aadhibiwe,
akawaambia zimeni taaa,


Mungu aitwe mungu siki zotee


Gafla nikamsikia jamaa mmoja akasema HP nina swali, jamaa akasema majuzi tulimsikia aliyeibiwa na leo inabidi kwanza tumsikie huyu dogo aliyeiba anasemaje.


Zikatokea kelele wengine wanasema apigwe banaa, wengine wanasema acheni uonevu.


Basi HP akaniambia hebu sema kama unalakujitetea haraha haraka.

Hapo nimeloaa, ijapokua kilimajaro vijijini ni baridi,

basi mimi nikasema mbona hii kesi mnaipeleka kiuonevu, mbona nilieondoka nae town siku ile hamjamuita na watu wa darasani kwangu hamjawashirikisha.

Watu wakaanza kusema kweli bana wanakuonea,
basi HP akaita yule dogo aliyekua nae yuko wapi, jamaa alikua kwa pembeni kidogo akajitokeza, HP akasema aya jiteteeni.

Mimi nikasema bana siku ya ijumaa qqqqqq alikuja nikamuwekea simu yake chaji nikaondoka nikamuacha na asubuhi yake jmos nikweli nilienda mjini ndio zilikua ratiba zangu si kwamba nilishtukiza sababu kuna baadhi ya watu pia niliwaambia tangu alhamis kuwa jmos nitaenda town.


Mwenzangu nae akaanza kujitetea akasema bana mimi maswala ya simu na kuchaji sijui lolote siwaelewi mnaniltea mambo nisizozojua, jamaa alikua mchaga alikua anaongea kwa hasira.

sasa HP akawa amechukia jinsi jamaa alivyokua anaongea.

Akamwambia dogo usiongee kama unatufokea, dogo akamjibu kuwa,
hivi ndivyo navyoongea na hata nikikufokea wewe sio baba yangu, wewe na mimi wote ni wanafunzi hapa.
Aisee yule HP akawa ame mind hatari. akamwambia, dogo mimi kuwepo hapa shuleni na wewe usidhani tunalingana umri, mimi ninaweza nikawa na watoto wakubwa kukuzid wewe kwahiyo kuwa na adabu .


Yule dogo nae akamjibu akamwambia,

huo ni ujinga wako kaka zangu walio na umri kama wako wanamiliki range wewe upo hapa unapambana na sisi.

Watu wakacheka zikaanza kelele,

HP akapaniki

Akawauliza kwahiyo tunawafanyaje.


Aiise akatokea jamaa mmoja alikua anajiita jeshi la mtu mmoja au nabii SULE.

Akasema sikiliza wewe HP usishinikize vitu ambavyo haviwezekani, anayedaiwa kuibiwa simu siku ya jumamosi alipokua anarudi kutoka maombi ya asubuhi alotuambia kuwa simu alikua nayo na hakumbuki alipoiweka,

na kama sababu ni kwenda mjini jumamos,mbona walienda wengi sio hawa machalii peke yao.
Tatizo lako unapenda kutumia ubabe ubabe.

Yani mimi sikuamini

Umati nzima ukaanza kusema aaaa, majamaa hawana hatia , mnawaonea.

qqqqq muongo yeye amepoteza simu hajaibiwa,

Basi watu wakatawanyika pale,

mimi nikafuatwa na washkaji kadhaa wakanishauri kwamba jamaa amekudhalilisha inabidi akulipe fidia au umfanyie malipizi,,


Kuna wakati ilikua nikiwa nimekaa peke yangu nikawa najiapiza kuwa ni lazima nije nifanye malipizi kwa HP na huyo jamaa aliyenisingizia kuiba simu,,,,,,,,,,,

Basi maisha yakasonga

Ila naamini kwa Tanzania ile shule ilikua inaongoza kwa matukuio ya kibabe shuleni na umafia mtaani kwa kipindi kile kabla ya 2011.

Mungu alinisaidia katika tukio lile sababu matukio mengi ya pale shule huwa yanaishiaga pabaya.

Na kwa upande wangu sijui nilikua na mkosi gani kwa mwaka ule,

sababu nilikutwa na msala mwingine pale moshi mjini ambao siljua chochote kuhusu hiyo issue ila baada ya miezi mitatu aliyenisababishia msala alinitafuta akaniomba msamahaa.




Basi baada ya kumaliza kidato cha sita pale nilipangiwa chuo fulani iringa.

Sijui niite nini hiki kitu,

Yakatokea machaguo ya pili ( second selection) ya watu kwenda vyuo.
Yule jamaa aliyenisingizia kumuibia simu nae akachaguliwa kuja kwenye chuo nilichopo mimi. Hapo nilishakua mwenyeji nadhan kama zaidi ya mwezi na....
Amini usiamini yule jamaa siku hiyo amefika chuo room zilikua zimeisha za ndani na hata nje zinazomilikiwa na chuo, ilibidi watafute mtaani.

Kama bahati, sijui alielekezwa kuwa room fulan kuna wanafunzi mmliosoma shule moja
Basi akaja mule room akanikuta mm na jamaa yangu mmoja wote tulimaliza hiyo shule


Yule jamaa siku zile za mwanzo alikosa pa kulala nilimbeba siku tatu kwenye bed yangu, nilimkumbusha tukio alilowahi kunifanyia akabaki tu kusema tusameheane.

Nikamwambia sisi ni binadamu na sio milima, hivyo tu.

Kuna wakati tukiwa pale iringa nilishapanga namna ya kumfanyia lipizi lakini sikufanya wazo likapotelea juu juu,

Natamani jamaa apate feeling jinsi roho yangu ilivyosononekana kipindi kile,


Muda sasa umepita na naamini mungu alinifidia pale nilipopoteza kwa tukio lile.


NUKTA.
 
Kuna demu baba yake alikuja kunifokea sana mbele za watu akaniambia mwanawe namchukua, mzee alikua na hasira sana kwa jinsi maneno mazito yalivyokua yakimtoka bibi wa mtoto akaingilia kati akawa anamgomba baba wa mtoto kuwa aache kunifokea, mm sijawahi kuwa na mahusiano au ukaribu na huyo mtoto, kulikua kuna mshkaji ndie aliekua anakula sana huyo mtoto ubaya mtoto kadata kwa huyo mshkaji, nilijiskia aibu kubwa sana kinachoniuma zaidi sihusiki na kumchukua huyo mtoto hata kumtania


Mara ya 2 pia kwa mwengine ni story ndefu

Kusingiziwa kubaya maana bora jambo ulitende kuliko kusingiziwa

Na ukiamuacha huyu Dada bila Kumkula?
 
Wema wangu uliniponza kumsaidia mwanadada mmoja ambae aliachika na mumewe nikaja kupakaziwa natembea nae
 
mm nikiwa mdogo niliwah kutakz kujiua nimepigwa sn kwa kusingiziwa afu mama ndio kabisa eti anadai biblia imeandika ucmnyime mtoto mpigo
 
Nimekaa zangu na nyagi ndogo(kischana) mfukoni sina pesa wala kazi kichwani mawazo kibao kodi imekalibia kuisha lijamaa limoja likaanza kuwaambia wenzie huyo dogo hapo ametumwa atupeleleze tumemshtukia lile jamaa lile Mungu alisamehe tu liliniongezea sonona na mji ulikuwa mchungu ghafla ule.
 
Back
Top Bottom