Ulishawahi kupitia changamoto kama hii?

billioner

Member
Feb 11, 2021
79
50
Habari za mda huu Wana JF,

Mimi mdogo wenu katika ujenzi wa Taifa lakini pia ni mgeni katika jukwaa Lini nimeandika ivi kuomba ushauri na kujua ni vipi ww ulikabiliana nalo ili tatizo!

Nipo chuo kikuu kwa Jina (naomba niifadhi) nasomea udaktari/MD lakini ivi juzi Kati Kuna mambo yalitokea kiukwel nimekuwa mtu wa mawazo sana kwasababu

Nimerudia semister chuoni ila tatizo ni kwamba Kuna daktar ambaye kwa kweli alinifelisha kwenye somo La clinical na kunipa 35% makusudi kabisa ila theory nilikuwa na A ya 85% ila sasa kama mnavotambua kwa masomo yetyu ya afya lazima ufaulu kote at least 50% ndo pass marks.

Ila daktar uyo alinifelisha pasina kujua tatizo. Changamoto kubwa I nakuj kweny kurudia somo moja (paedtric), kwanza sikubahatika kupata mkopo wala sponsorship, wazazi ndo wananipa support na kwa wale mliopitia chuoni nadhan ugumu mnaujua.

Kwa sasa nimebakiza mwaka mmoja nitimu masomo angu kwa kwelii chuoni najituma kwenye kusoma ata Kuna wakati silali ata masomo mengine almost masomo yangu yote Nina A na sijawahi kupata C tangu niingie chuoni kabisa yaani.

Sasa nimeamua kurudia ivo kwa kuwa mpini kashika yeye na mm makali lazima niumie. Nikijifanya niko juu au Kuja juu nitaumia mm na still na malengo makubwa.

Kinachonipa matumaini nikuwa principal wa chuo aliona matokea angu nakuzungumzia swala Hilo nakunipa pole ila kaniahidi kuwa atalisimamia next exam clinical isitokee hivo.

Maana kuna uwonevu ndani ake maana walijadiliana wenyewe maana clinical exam kufel ni ngumu sana.

Swali langu ni je ww ulishawahi kukutana na changamoto kama hii na nini mwisho wake ilikuwa je ?

Samahanini lakini kwa uwandishi mpovu, mtanisamehe kwa hilo niwatakie ujenzi mwema ktk Taifa.
 
Sijaelewa, unataka ushauri gani sasa? Naomba unieleweshe nami nitakua tayari kukushauti kwa mtazamo wangu, maana humo humo ndani kuna kufeli mtihani lakini kuna tena changamoto kuwa hujawahi kuwa na mahusiano.
 
Sijaelewa, unataka ushauri gani sasa? Naomba unieleweshe nami nitakua tayari kukushauti kwa mtazamo wangu, maana humo humo ndani kuna kufeli mtihani lakini kuna tena changamoto kuwa hujawahi kuwa na mahusiano....
Kufel na mwisho wake ilikuwa je baada ya kurudia?
 
Wengine tulikutana za zaidi ya hiyo we komaa Tu dogo

Hivi ushawahi wewe kabla ya kuanza kupresent anakuambia nipe hx tu yaani amplification then unamaliza tu anakuambia management zote zile uloandika na anakuongezea mbili hafu anakuuliza nipe zingine 3

Hafu anakuambia umeferi
 
Hebu chunguza mwandiko huenda ndio unakufelisha.

Msomi kama wewe huoni aibu kuandika x, yetyu, ivi?

Huko kuwahudumia wagonjwa herufi moja itasababisha mgonjwa apewe dawa tofauti.

Wasomi kama wewe ndio mnafanya sisi tusiosoma tuone kusoma sio kuelimika.
 
Wengine tulikutana za zaidi ya hiyo we komaa Tu dogo

Hivi ushawahi wewe kabla ya kuanza kupresent anakuambia nipe hx tu yaani amplification then unamaliza tu anakuambia management zote zile uloandika na anakuongezea mbili hafu anakuuliza nipe zingine 3

Hafu anakuambia umeferi
Asante mkuu ushauri wako nimeupenda ntaufanyia kazi
 
Kwa huu mwandiko tatizo si uandishi mbaya au mzuri tatizo unaandika kama mtoto wa form 2 xxxxxx nyingi. Andika upya ndio utapewa ushauri
 
Back
Top Bottom