Ulishawahi kujutia kupoteza muda masomoni?

Sijasoma msg content ila Heading tu nimeielewa sana. Nimepoteza sana Muda na nimejifunza, siwez kuwakomalia kiivyo watoto wangu skuli ila ni kuwatengenezea misingi ya kujiajiri na kujitegemea. Wasomi Wa sasa idadi yao kubwa wameajiriwa na walioishia standard seven au form four
 
Wewe tangu mdogo uliambiwa kuwa komaa mwanangu, soma sana utapata maisha mazuri.

Ukaamua kukomaa na shule, ukafunga vioo kwa kuwaona rafiki zako wasio komaa ni "wajinga" ukala kitabu kweli kweli, busy masaa 24 muda wa kukaa na washkaji wakujuze linaloendelea kitaa haukuwa nao, ukajiona "kipanga" wa mtaa, ukakatiza vidato.

Mpaka elimu ya juu, wazazi wakikusifu mwanetu mwenye akili, hana makundi, ukakomaa na kitabu sana, ukiamini kuwa lazima utatoboa kupitia kitabu.

Huu ni mfano wa maisha ya wasomi wengi, wengi wao hatujichanganyi na maisha ya mtaani kujua kinachoendelea katika uhalisia tumekuwa na ndoto fulani hivi tulizozijenga vichwani mwetu ambazo kwenye maisha halisi itatuchukua muda sana kutimia ama zisitimie kabisa, huwa tunawaza tutakapomaliza shule, nyumba na gari ni vitu vya kawaida sana, ila balaa ni pale linapokuja mambo hayo kukosekana.

Maisha ya wasomi yamejikita sana katika kuzingatia shule zaidi kiasi kwamba tunasahau kuchangamana na watu wakatupa maarifa mengine ya kimaisha, kwa kutegemea kupata kazi ila baada ya kukosa kazi pia, mahala pa kushika panakosekana maana hatukuwekeza katika upande mwingine yaani mtaani ambako tunarudi ndipo unakuta uliyemaliza naye form four yeye akaishia hapo, unakuta kajijenga kuzidi wewe.

Hasa pale ambapo course uliyosoma unafahamu kuwa kupata ajira sio leo wala kesho, kujiajiri pia ikawa changamoto.

Vipi ulishawahi kujutia muda uliokaa masomoni? Hebu share experience, utuambie ni kwa nini unajutia.
Safiii.watu hawajiongez
 
Kama mtu ana akili za kijima zilizoezekwa na elimu ya kukariri anaweza kufikiri elimu ni kuajiriwa na akajuta ni kwanini alisoma mara akosapo ajira. Lakini kwa aliyesoma na akaelimika haya mawazo hayawezi kamwe kuwa nayo.
 
Sijasoma msg content ila Heading tu nimeielewa sana. Nimepoteza sana Muda na nimejifunza, siwez kuwakomalia kiivyo watoto wangu skuli ila ni kuwatengenezea misingi ya kujiajiri na kujitegemea. Wasomi Wa sasa idadi yao kubwa wameajiriwa na walioishia standard seven au form four
Mkuu acha story za vijiweni basi .
Nitajie mfano wa hao form four failure na lasaba failure ambao wameajiri wasomi.
Elimu ni muhimu sana wakuu .
Elimu elimu elimu elimu .

Kama mzee Mello angekuw a na mawazo kama ya baadhi ya member humu unadhani angesomesha mtoto wake Maxence mello hadi afikie level ya kutengeneza hii platform.?
Elimu elimu elimu
 
Sometimes huwa najikuta najilaumu kwanini nilisoma kuto huko. Kwanini nisingeishia kidato cha nne nikamuomba mzee mtaji nikafanya biashara.

Basi kuna bro wangu ni mtoto wa mama mkubwa tumesoma wote class moja shule ya msingi ila darasani hakuwa vizuri. Tukamaliza form four pamoja. Yeye hakuendelea akaanza mishe bakta, sasa hivi amejenga nyumba yake kali na ameoa yupo Moshi town hapo.

Mimi mpaka chuo kikuu lakini sijatusua wala mke sina. Huwa najilaumu ila najua sijasoma bure ni milango tu haijafunguka.

Maisha hayana formula wakuu.
 
sijutii sana ila ninampango wa kurudisha vyeti vyangu nirudishiwe ada hata nusu
 
Umeandika vizuri sana mkuu.

Wakati nasoma niliaminishwa kazi ya kuajiriwa ndio yenye utajiri mkubwa zaidi duniani, ila!!!!

Ukweli ni kwamba watu walioajiriwa ndio wanaongoza kwa:
-Madeni
-Stress
-Matumaini yasio na kikomo
-Kutofikiri nje ya ajira
-Jeuri ya kuwa na ajira lakini kipato hakimpi furaha

Wanaosoma kwa ajiri ajira wasome kwa bidii ila kilichomo kwenye ajira ni siri mwajiriwa.
 
Kwa kweli ajira ni mtihani kidogo, bosi anafoka, mshahara hautoshi n.k
 
Back
Top Bottom