Ulishawahi kujutia kupoteza muda masomoni?

Deva

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
1,237
Reaction score
1,819
Wewe tangu mdogo uliambiwa kuwa komaa mwanangu, soma sana utapata maisha mazuri.

Ukaamua kukomaa na shule, ukafunga vioo kwa kuwaona rafiki zako wasio komaa ni "wajinga" ukala kitabu kweli kweli, busy masaa 24 muda wa kukaa na washkaji wakujuze linaloendelea kitaa haukuwa nao, ukajiona "kipanga" wa mtaa, ukakatiza vidato.

Mpaka elimu ya juu, wazazi wakikusifu mwanetu mwenye akili, hana makundi, ukakomaa na kitabu sana, ukiamini kuwa lazima utatoboa kupitia kitabu.

Huu ni mfano wa maisha ya wasomi wengi, wengi wao hatujichanganyi na maisha ya mtaani kujua kinachoendelea katika uhalisia tumekuwa na ndoto fulani hivi tulizozijenga vichwani mwetu ambazo kwenye maisha halisi itatuchukua muda sana kutimia ama zisitimie kabisa, huwa tunawaza tutakapomaliza shule, nyumba na gari ni vitu vya kawaida sana, ila balaa ni pale linapokuja mambo hayo kukosekana.

Maisha ya wasomi yamejikita sana katika kuzingatia shule zaidi kiasi kwamba tunasahau kuchangamana na watu wakatupa maarifa mengine ya kimaisha, kwa kutegemea kupata kazi ila baada ya kukosa kazi pia, mahala pa kushika panakosekana maana hatukuwekeza katika upande mwingine yaani mtaani ambako tunarudi ndipo unakuta uliyemaliza naye form four yeye akaishia hapo, unakuta kajijenga kuzidi wewe.

Hasa pale ambapo course uliyosoma unafahamu kuwa kupata ajira sio leo wala kesho, kujiajiri pia ikawa changamoto.

Vipi ulishawahi kujutia muda uliokaa masomoni? Hebu share experience, utuambie ni kwa nini unajutia.
 
Sikuwahi maana masomo niliyafanya nikiwa na malengo, nikiwa naendeleza shughuli za pembeni
 
hauhitaji PHD kujua dira ya maisha.ila elimu ni cha kwanza ktk maisha
 
m najutia___ elim ni muhim but shida inakuja unavomaliza degree umekaa miaka zaid ya 15 shule af unakosa ajira unaanza kupasua kokoto same na mtu ambaye hakwend kbisa scul
 
Elimu ya kidato cha 4 tu ingenitosha kabisa.

Najuta kwa muda niliopoteza, maarifa niliyopata yananifanya nione maisha hayawezekani nje ya ajira
Hiki ulichonena ni hisia zinazotupata wasomi wengi.

Sijui kusoma sana huwa kunatupunguzia uwezo wa kufikiri? yaani hata sielewi, maana wasomi wengi tumekaa kiwoga woga sana.
 
Zama zinabadilika hivyo sisi nasi pia hatuna budi kubadili fikra na mitazamo yetu kuhusu Elimu.
Elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya mwanadamu,inamfanya ajitambue na kuziona fursa za kujikomboa kiuchumi ambazo asiye na elimu ni ngumu sana kuziona!...hili ndio kusudi kuu la Elimu na si vinginevyo!
Chukua mfano huu; mtu mwenye Elimu na asiye na Elimu ni mfano wa watu wawili watembeao gizani kwa nyakati tofauti tofauti huku mmoja wao akiwa na torch (Elimu) na mwingine akiwa hana torch(hana Elimu)
Hivyo basi yule asiye na torch ni rahisi sana kujikwaa na kukengeuka njia aendayo kuliko yule atembeaye gizani na torch...
Mark my words..kwa mtu mwenye Elimu kufanikiwa huwa ni suala la MUDA tu wakati kwa asiye na Elimu suala la kufanikiwa ni la KUFA na KUPONA!!
 
Wewe tangu mdogo uliambiwa kuwa komaa mwanangu, soma sana utapata maisha mazuri.

Ukaamua kukomaa na shule, ukafunga vioo kwa kuwaona rafiki zako wasio komaa ni "wajinga" ukala kitabu kweli kweli, busy masaa 24 muda wa kukaa na washkaji wakujuze linaloendelea kitaa haukuwa nao, ukajiona "kipanga" wa mtaa, ukakatiza vidato.

Mpaka elimu ya juu, wazazi wakikusifu mwanetu mwenye akili, hana makundi, ukakomaa na kitabu sana, ukiamini kuwa lazima utatoboa kupitia kitabu.

Huu ni mfano wa maisha ya wasomi wengi, wengi wao hatujichanganyi na maisha ya mtaani kujua kinachoendelea katika uhalisia tumekuwa na ndoto fulani hivi tulizozijenga vichwani mwetu ambazo kwenye maisha halisi itatuchukua muda sana kutimia ama zisitimie kabisa, huwa tunawaza tutakapomaliza shule, nyumba na gari ni vitu vya kawaida sana, ila balaa ni pale linapokuja mambo hayo kukosekana.

Maisha ya wasomi yamejikita sana katika kuzingatia shule zaidi kiasi kwamba tunasahau kuchangamana na watu wakatupa maarifa mengine ya kimaisha, kwa kutegemea kupata kazi ila baada ya kukosa kazi pia, mahala pa kushika panakosekana maana hatukuwekeza katika upande mwingine yaani mtaani ambako tunarudi ndipo unakuta uliyemaliza naye form four yeye akaishia hapo, unakuta kajijenga kuzidi wewe.

Hasa pale ambapo course uliyosoma unafahamu kuwa kupata ajira sio leo wala kesho, kujiajiri pia ikawa changamoto.

Vipi ulishawahi kujutia muda uliokaa masomoni? Hebu share experience, utuambie ni kwa nini unajutia.
Kusema kweli wanachuo wengi hawana ideas na maisha halis ya mtaani, kwa ambao wapo chuo wanajua hili,ukimaliza chuo ndo akili inakukaa sawa

Elimu ya mtaani haihitaji madesa kama uliyosoma chuo,
 
Zama zinabadilika hivyo sisi nasi pia hatuna budi kubadili fikra na mitazamo yetu kuhusu Elimu.
Elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya mwanadamu,inamfanya ajitambue na kuziona fursa za kujikomboa kiuchumi ambazo asiye na elimu ni ngumu sana kuziona!...hili ndio kusudi kuu la Elimu na si vinginevyo!
Chukua mfano huu; mtu mwenye Elimu na asiye na Elimu ni mfano wa watu wawili watembeao gizani kwa nyakati tofauti tofauti huku mmoja wao akiwa na torch (Elimu) na mwingine akiwa hana torch(hana Elimu)
Hivyo basi yule asiye na torch ni rahisi sana kujikwaa na kukengeuka njia aendayo kuliko yule atembeaye gizani na torch...
Mark my words..kwa mtu mwenye Elimu kufanikiwa huwa ni suala la MUDA tu wakati kwa asiye na Elimu suala la kufanikiwa ni la KUFA na KUPONA!!
Umenena vizuri kabisa mkuu kuwa elimu inamfanya binadamu ajitambue na kuziona fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi, swali langu je? Ni mfumo huu wa elimu wa Tanzania? Hakika sio huu, huu umejaa "Illusion"(Imani ya mambo ambayo hayapo) yaani unafundisha mambo kinadharia sana.

Msemo wako ni kinyume chake kwa nchi hii ya Tanzania, idadi ya watu wanaozichungulia fursa katika uhalisia wasiosoma wamewapiku wasomi ambao kutwa ni bahasha za kaki, kwa sababu tayari wameshaaminishwa hivyo, graduate ni muoga kupita kiasi.

Mfumo wa elimu ndio inapaswa ubadilike.
 
mtu aliyesoma na asiyesoma wana tofauti kubwa sana......kuanzia life style,namna ya kuargue, mwonekano na mengine mengi.......kwa kifupi elimu inaweza kum-shape mtu

sijutii kusoma aisee thou nimejiajiri......
 
Sijawahi na sitowahi kujutia. Kusoma ni Biashara kama Biashara nyingine Kuna wakati tunapitia profit and loses, kwangu kawaida mzee
 
Hongera kwa kujiajiri, kuja wenzio hata hilo pia ni mtihani mkubwa.
 
Sijawahi na sitowahi kujutia. Kusoma ni Biashara kama Biashara nyingine Kuna wakati tunapitia profit and loses, kwangu kawaida mzee
Wewe una mtazamo sahihi, sio kila tukifanyacho kitaleta mrejesho tunaotaka.

Tujifunze tu kutokuwa dissappointed
 
Wengi wetu tumekalia lawama tu hatuna uvumilivu hata kidogo asee
 
Umenena vizuri kabisa mkuu kuwa elimu inamfanya binadamu ajitambue na kuziona fursa zilizopo kujikomboa kiuchumi, swali langu je? Ni mfumo huu wa elimu wa Tanzania? Hakika sio huu, huu umejaa "Illusion"(Imani ya mambo ambayo hayapo) yaani unafundisha mambo kinadharia sana.

Msemo wako ni kinyume chake kwa nchi hii ya Tanzania, idadi ya watu wanaozichungulia fursa katika uhalisia wasiosoma wamewapiku wasomi ambao kutwa ni bahasha za kaki, kwa sababu tayari wameshaaminishwa hivyo, graduate ni muoga kupita kiasi.

Mfumo wa elimu ndio inapaswa ubadilike.
Yap,,ni kweli mfumo wetu wa Elimu ya darasani haujafit vizuri kumuandaa mhitimu kupambana na mazingira yake kwa vitendo.
Lakini huu sio muda wa kulaumiana wala kumtafuta mchawi ni nani! Ni lazima tupandikize "Flexibility" katika akili ya wanafunzi wa zama hizi kuliko kuendelea kuwaaminisha kuwa Ufunguo pekee wa maisha yao ni Ajira!
Wazazi wafikirie nje zaidi ya box la watoto wao kusoma ili waajiriwe pekee huku wakifatilia kwa ukaribu ni ujuzi (skills) gani watoto wao wanao ambao ukiendelezwa unaweza kumsaidia mtoto huyo kujiajiri!
 
Back
Top Bottom