Ulishawahi kugombana na mtu halafu baadaye mkapatana na kuwa maswahiba wa karibu sana (best friends)? What happened?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,956
2,000
Swali la kizushi:-

Ikiwa kulikuwa na mikataba, pamoja na makubaliano uliyotoka nayo DSM, sasa kwanini usingefanya mawasiliano na makao makuu iliyopo DSM kuwaambia hali halisi?
Mkuu, I was under probation. But the guy was there for 3 years already. Jamaa alikuwa anaaminiwa sana huko headquarters kiasi kwamba chochote atakachosema kuhusu mimi hawezi kupingwa. Alishaanza kunitangaza kuwa mimi ninakiburi huko Dar kwa sababu ninapigania haki yangu
 
eddy king

JF-Expert Member
Apr 1, 2016
512
1,000
Jamaa hakuwahi kuniomba msamaha kwa maovu aliyokuwa ananifanyia. Unaanzaje kumsamehe mtu ambaye hajutii makosa yake?
Sio lazima yeye akuombe wewe msamaha ila unaweza kumsamehe mana pengine yeye hata hajui kama uliumia kiasi cha kumchukia kiasi hicho. Wanasema "Samehe sio kwasababu yake ila ni kwaajili ya maisha yako " mana anayeteseka zaidi ni wewe kuliko yeye .Mana kitendo cha wewe kwenda kumuona Pamoja na mambo aliyokufanyia kitamtesa zaidi ya wewe kutokwenda .

Sent using Jamii Forums mobile app
 
carcinoma

JF-Expert Member
Mar 5, 2017
4,967
2,000
Huwa inatokea mtu unakutana nae ile first impression unatokea kumdiss tu bila sababu lakini siku ukipata nafasi ya kukaa nae unakuja kugundua kwamba ni mtu poa sana. Sema ile first impression mlikutana vibaya tu..

Lakini swala la mtu tulishatibuana halafu tuwe best friends haijawahi kutokea aiseeh.. labda ka unafiki tu ka kuchekeana ili maisha yaende kama mko sehemu ambayo huwezi kumpotezea mazima mfano ni partner wako kwenye mishe mishe.
 
Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,956
2,000
Hata mm sjaelewa na wala sjaona wapi walikua marafiki
emoji849.png
...
Kitendo cha watu wawili na taasisi NGO kwenda kufanya kazi kijijini ndani huuukooo, automatically mnafuwa ni marafiki.

Ningesema niandike kila kitu kama unavyotaka wewe, ingeweza kuchukua masaa hata 5 kusoma. Nimefanya kifupisho alafu umeshindwa kuelewa.

Anyway, sio lazima kila mtu anielewe. Ukishindwa kunielewa wewe basi watanielewa wengine
 
Ninja assasin

JF-Expert Member
Jul 2, 2018
1,502
2,000
Nikiwa jkt kanembwa 2013 kampan ya Chalii koi baada ya doso la ukurutu kukomaa kwelikweli Kuna siku moja tukiwa foleni kusubili msosi mesi saa 8 jua la kigoma likiwa linachoma kisawasawa vipara vya wembe

tukiwa tumekaa chini ya ile ardhi nyekundu mimi nikiwa na plate yangu mkononi nikiwa kama mtu wa tano kutoka mbele Kuna baadhi ya kuruti wakawa wanagombania nafasi ya kuchukua msos pale mbele basi bhana Kuna afande alitoka huko na bonge LA fimbo akachapa mstali wa mbele wale kuruti kujiokoa wakarudi nyuma kwa kasi nikasukumwa na kuanguka chini nikiwa chini nikanyanyua miguu juu kuzuia jamaa wasinilalie wote

Kuna jamaa akafikia kweny ile miguu niliyo nyanyua juu basi kujiokoa nikampush jule jamaa kwa nguvu bahati mbaya kulikuwa na nguzo ya zege pemben kidogo jamaa akaivaa ile nguzo akaumia basi bhana weee nikiwa pale chini jamaa alinirukia kama simba kaona swala nilipigwa makonde ya uso ya maana kama manne mfululizo

Nikiwa bado nipo chini yule mwamba yupo juu nikiwa na plate yangu nilipa jamaa yule plate ya usawa wa jicho moja tuuu mpaka akachanika damu ikaanza kutoka kwa kasi

Akaja afande kwa Jina tulikuwa tunamwita cyborg alikua MP akaanza kutupa doso pale mm ndio nikaonekana mkorofi nikakunjwa kisawasawa basi baada ya doso la maana kukloo kweny maji machafu ya pale mesi kupiga simu kweny kokoto tukafungwa mashati tukaenda kuoga wote kila mmoja anamtuka mwenzake tukamaliza na kufua tukafungana Tena zile Greenvesti za jkt tukarudi ikawa kila sehem tumefungana mashati kwa siku kadhaa

Yule jamaa alikuja kuwa rafk angu mkubwa mnoooo siwez msahau tulifanya mambo mingiii pamoja kila nilipo nae yupo

Kuna siku story inayofuata apo mpaka kupandishwa vyeo na uyo jamaa kuwa majemedari wa kuonja msosi Kwahiyo sisi tukawa tunachukua msos bila foleni ilikuwa hivi kwa ufupi Kuna siku tulipo mdoji afande wa zamu night kali tukaenda kulala kweny maanga/mabweni ya maafande chini ya uvungu wa vitanda vya maafande wenyewe wakiwa juu mida ya saa 11 tunashtuka tunakuna majamaa na kombati za kijani yametuzunguka wamehamisha vitanda yanatusubili tuamke kinacho fuata nazani unajua.............
 
APEFACE

JF-Expert Member
Oct 1, 2016
3,976
2,000
Mi kuna jamaa mmoja tulikuwa nae shule ya bweni huko kilimanjaro...tulikuwa tunalala dorm moja , hatukuwa tunaendana itikadi kabisa...na jamaa kama alikuwa na dharau sana za kishamba (wale jamaa wanaojifanyaga wakishua)...yeye alikuwa anasoma science mimi nilikuwa biashara..kifupi hakuwa rafiki angu kabisa...siku moja asubuhi nimetoka washroom nataka kuingia dorm nashangaa msela anasema nimpe simu yake, kumbe asubuhi ile alikuwa kaibiwa simu sasa ile kutoniona bed kwangu, mana wote tulikuwa tunalala decker za juu karibu karibu,akajua ni mimi ndo nimeenda kuficha, si tukaanza mikono basi tulizibuana hadi dorm leader alipokuja kutuachanisha mana masela huwaga wanashangilia tu...basi ikaisha kihivohivo...sasa baada ya miaka 10 kupita nimekuja kuonana nae mkoa fulani huku kanda ya ziwa, siku naonana nae ilikuwa ni mgahawani nikampa hi tukapeana hii kijujuu..sasa siku niko WORKSHOP kwangu akaja jamaa na pikipiki yake achomewe vijana wangu wakamchomea, akaniuliza vipi nikamwambia hii WORKSHOP ni yangu nikitoka job ndo huwa nazuga hapa...siku nyingine akaja nashangaa tumekuwa marafiki sana mpaka kuna tenda fulani zimetangazwa na Halmashauri tukaenda tukaomba wote...nashangaa sana juu ya hii issue
 
Culture Me

JF-Expert Member
May 24, 2017
9,657
2,000
Nikiwa jkt kanembwa 2013 kampan ya chaii koi baada ya doso la ukurutu kukomaa kwelikweli Kuna siku moja tukiwa foleni kusubili msosi mesi saa 8 jua la kigoma likiwa linachoma kisawasawa vipara vya wembe

tukiwa tumekaa chini ya ile ardhi nyekundu mimi nikiwa na plate yangu mkononi nikiwa kama mtu wa tano kutoka mbele Kuna baadhi ya kuruti wakawa wanagombania nafasi ya kuchukua msos pale mbele basi bhana Kuna afande alitoka huko na bonge LA fimbo akachapa mstali wa mbele wale kuruti kujiokoa wakarudi nyuma kwa kasi nikasukumwa na kuanguka chini nikiwa chini nikanyanyua miguu juu kuzuia jamaa wasinilalie wote

Kuna jamaa akafikia kweny ile miguu niliyo nyanyua juu basi kujiokoa nikampush jule jamaa kwa nguvu bahati mbaya kulikuwa na nguzo ya zege pemben kidogo jamaa akaivaa ile nguzo akaumia basi bhana weee nikiwa pale chini jamaa alinirukia kama simba kaona swala nilipigwa makonde ya uso ya maana kama manne mfululizo

Nikiwa bado nipo chini yule mwamba yupo juu nikiwa na plate yangu nilipa jamaa yule plate ya usawa wa jicho moja tuuu mpaka akachanika damu ikaanza kutoka kwa kasi

Akaja afande kwa Jina tulikuwa tunamwita cyborg alikua MP akaanza kutupa doso pale mm ndio nikaonekana mkorofi nikakunjwa kisawasawa basi baada ya doso la maana kukloo kweny maji machafu ya pale mesi kupiga simu kweny kokoto tukafungwa mashati tukaenda kuoga wote kila mmoja anamtuka mwenzake tukamaliza na kufua tukafungana Tena zile Greenvesti za jkt tukarudi ikawa kila sehem tumefungana mashati kwa siku kadhaa

Yule jamaa alikuja kuwa rafk angu mkubwa mnoooo siwez msahau tulifanya mambo mingiii pamoja kila nilipo nae yupo

Kuna siku story inayofuata apo mpaka kupandishwa vyeo na uyo jamaa kuwa majemedari wa kuonja msosi Kwahiyo sisi tukawa tunachukua msos bila foleni ilikuwa hivi kwa ufupi Kuna siku tulipo mdoji afande wa zamu night kali tukaenda kulala kweny maanga/mabweni ya maafande chini ya uvungu wa vitanda vya maafande wenyewe wakiwa juu mida ya saa 11 tunashtuka tunakuna majamaa na kombati za kijani yametuzunguka wamehamisha vitanda yanatusubili tuamke kinacho fuata nazani unajua.............
Wow interesting story,
Eeenh ikawaje baada ya kukutwa chini ya kitanda na kwanini mliamua kulala chini ya vitanda vyao?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom