Ulishawahi kugombana na mtu halafu baadaye mkapatana na kuwa maswahiba wa karibu sana (best friends)? What happened?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
14,949
2,000
Do you believe in second chances in friendships or romance? Did it ever work out in your life?

Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums. Mimi mdogo wenu (Last Born) Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Eti ndugu zangu Watanzania;

Je, Ulishawahi kugombana na mtu (Ugomvi Mkubwa Kweli) alafu baadae mkaja kupatana naye kisha akawa swahiba wako wa karibu sana (Your Best Friend)? What really happened? Please tell us.

Mimi baada ya kumaliza chuo kikuu mwaka 2009 nilikaa mtaani saaana mpaka kufikia mwaka 2011 nikapata kazi kwenye NGO moja ipo Ifakara Morogoro. Hii kazi niliunganishiwa na classmate wangu.

Makao makuu ya NGO hiyo yapo Dar ila pia wanazo ofisi zao huko Kyela, Mbeya.

Baada ya kuwasili Ifakara nikapokewa na boss wangu huyo anaitwa Emanuel Joseph Mwakapala (Hili sio jina lake halisi)

Sasa kulingana na mkataba pamoja na makubaliano niliyotoka nayo makao makuu huku Dar huyu jamaa alipaswa kuwa ananipa pesa kiasi cha 250,000/= hii ni kwa ajili ya chakula na mawasiliano kila mwezi mbali na mshahara ambao ulikuwa ni mdogo sana kama 150,000/= tu kwa maana I was still under supervision/probation. Kwa wakati huo hii pesa ilikuwa inatosha sana kwa kuishi tena mazingira ya kijijini huku ninasubiria mkataba kamili ambapo mshahara ungeweza kuongezeka maradufu.

Sote tulipangiwa nyumba moja sababu ofisi zilikuwa nje sana ya Ifakara mjini (mwendo wa masaa 2 rough road)

Kwa kuwa bado nilikuwa nipo under probation sikuweza kuingiziwa pesa katika account yangu ya bank. Pesa zote zikawa zinaingia katika account ya huyo jamaa, Emanuel.

Kwa kipindi chote cha miezi sita ya ile probation yangu sikuwahi kupewa ile 250,000/=

Nilichokuwa ninaambulia mimi ni ile 150,000/= tu ambayo ndio hiyo nikawa ninatumia kununulia chakula asubuhi, mchana pamoja na jioni. Na kwa kutumia pesa hiyo hiyo ndio nilikuwa ninanunua sabuni, airtime vouchers pamoja mahitaji mengine madogo madogo huku mzee baba akiwa anabugia pesa yangu kiasi cha 250,000/= kila mwezi.

Niliweza ku-survive kwa miezi 3 tu (I wasn't an Infantry Soldier by then) kisha nikaamua kusepa baada ya kuona maisha ni magumu. Nikarudi Dar kufanya kazi kiwanda cha KTM Mbagala kuna uncle wangu mmoja aliniunganishia.

Sasa Jumapili iliyopita nilipigiwa simu na classmate wangu yule aliyeniunganishia kazi ile ya NGO Ifakara ya kwamba atakuja kunipitia hapa home twende tukamsalimie na kumpa pole Emanuel alipata ajali ya gari akiwa anatokea ofisini Upanga kwenda Mwandege (mkoa wa Pwani) gari yake aligongana na gari nyingine ndogo maeneo ya kiwanda cha Bakhersa.

Mimi nimekataa katakata. Nimemwambia classmate kwamba mtu aliyetaka kuniua mimi kwa njaa kwanini na yeye asife? Kwani akifa mimi nitapungukiwa kitu gani katika maisha yangu? Classmate alikuja na gari mpaka home alinisihi sana twende wote ila nikakataa kuingia katika gari yake nikamwambia nenda mwenyewe.

Ulishawahi kumfanya adui yako mkubwa kuwa rafiki wa karibu? What really happened? Please tell us.

Ninauza Vitabu Vya Kujifunzia Lugha Ya Kijerumani. Ich komme aus der Stadt Dar Es Salaam und verkaufe diese Deutsch-Lernbücher - JamiiForums
 

Kashaulo

JF-Expert Member
Jun 14, 2019
2,802
2,000
Kwenye movies huwa tunaona, maadui wanakuwa marafiki na kuokoana... hata kwenye ndoa kuna ON and OFF nyingi.


Sio lazima uelewe.
 

Mkongwee

JF-Expert Member
Jul 29, 2018
349
1,000
Mwaka 2010 niko mwaka wa kwanzaa chuoni, nliibiwa bum loooote
Jamaa mmoja akawa ananiliwaza liwaza ndio maisha ya chuo nivumiliee,
Kufatilia kumbe mwizi ni yeyeeee, daaaaaaah nilimbadilikia jamaa, maana benki walikua wanamtaka na chuo wanamtaka

Jamaa alimwaga chozi akilia huku akiomba msamaha na akiniahidi atanipa pesa zangu na fidia
Huruma ikanitawala nikamwambia arudishe changu yaishee
Akafanikiwa kurudisha japo kwa awamu

Ajabu sasaaaa toka hapo mpaka leoo jamaa ndio kawa rafiki yangu mkuu, yaani best friend, kwetu wanamjua na kwao wananijua...

Kituko cha pili baada ya kwanza kazi
Siku moja nikaenda ofisi za maji kigoma kulipia bilii, nikakutana na dada mmoja mtumishi wa hiyo ofisi, ni mdada wa kisasaa mzuri, anajua kuvaa,

Dadaa akanivagaa kuniita mie muhuni, moto nlomuwashia hapo hapo ofisini kwaoo alitia huruma,
Ajabu watumishi wenzie hakuna hata alioingilia kumtetea, mwisho wa siku akaniomba yaishe, na yakaisha hapo badooo
Kumcharua nikamwomba namba ya simu akanipa bhanaaa

Huwezi amini akawa wangu kinomaaaa nikimtaka muda wowoteeee anakujaaaa
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom