Ulinzi wa ajabu Central Police kwa ajili ya Mbowe; asafirishwa kwa ndege ya JWTZ kwenda Arusha!

Guys kama kuna mawasiliano yoyote huko alipo,mwambieni asikubali kula chakula chao hata kidogo.maana hatuwezi jua.

Hili la kweli kabisa kama waliweza kumkolimba Kolimba kwa kutoa kauli kwamba, "CCM imekosa muelekeo" basi pia wanaweza kumdhuru Mbowe.
 
Huu ni mwanzo tu, habari zilizopatikana kutoka kwa under cover zinaeleza kitakacho fuatia kwa Chadema ni Tsunami kuliko iliyotokea Japani ,Let wait and see .

Wewe umetumwa kuwatisha watu hapa? Kwa taarifa yako mbinu ya kuwatumia polisi na mahakama kujaribu kuuzima upinzani ni mbinu iliyopitwa na wakati na hasa enzi hizi za za utandawazi!!! Mbinu hii ilikuwa poa wakati ule wa Mrema kwani alimalizwa nguvu kwa kesi kibao mahakamani na kuripoti polisi. Kwa kipindi hiki, mbinu hii haitwasaidia CCM mbali ya kuchochea hasira za wananchi na kujichimbia kaburi zaidi.

Fungua macho uone what will happen next!!!!

Tiba
 
Kajifunze kusoma na kuandika kwanza,"gurupu"ndio kitu gani?
huu ndio mwisho wa magamba na watu wake.
 
Hili la kweli kabisa kama waliweza kumkolimba Kolimba kwa kutoa kauli kwamba, "CCM imekosa muelekeo" basi pia wanaweza kumdhuru Mbowe.

Kabisa mkuu hawa jamaa now hawawezi kuaminika kabisa,maana ingekuwa ihari yao wangefanya moja tu ili ijulikane lakini ndio hivyo macho ya watu yanawaangalia,so kama chakula apewe na watu wake basi na sio zaidi.....
 
wanaturahisishia kaz ya kung'oa utawala wa kidhalimu,kibabe,siku si nyingi sana kutoka sasa,yatatimia,vitabu vitaandikwa upya uhuru wa kweri wa tanzania ulipatikana kwa revolution.
 
Jamani naomba niulize si ni jana tu wametoa tamko na Mbowe akasema hawezi kuishi huku amekaa ni heri kufa huku amesimama.... sasa kawaje baada ya masaa machache hivi Kageuka kuwa Marehemu Saadam Husein???

Let, somebody who knows the truth tell us the truth..... Kuna tatizo lolote hapo au ilikuwaje mpaka Mbowe kageuka kuwa jiwe la chumvi?
 
Mods stop chakachuaring this topic,just because we have a different views on sensitive issues,it doesn't mean we can't post a comment or at least see what others ARE SAYIN'!
We have to go through a lot of sh*t before posting a comment,..why?
OKAY!! BACK TO THE TOPIC!!
 
CDM wangefanya nini mkuu wangu maanake sheria yenyewe imewekwa kuwalinda viongozi wetu na Mbowe kama Mbunge anatakiwa kupewa heshima hiyo. Kama taratibu hizo zitakiukwa na chombo chochote cha usalama hatuwezi kuhalalisha tukio hili sababu nyingine ambazo hazipo ktk vifungu vya sheria.
Hakuna sheria inayokataza mbunge kukamatwa....kwa heshima,mbunge hakamatwi bungeni au bustani ya bunge,barazani,njiani kwenda au kutoka.Akifika crib,kama weekend hamna kikao cha bunge anaweza kung'ang'aniwa..Kwanza hata akiwa bungeni na bi makinda akasema go ahead,wanamrukia!!...acheni kuchakachua sheria wandungu!.
 
Nadhani kukamatwa kwa Mbowe ambaye ni kiongozi wa upinzani bungeni, na mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani nchini kwa kesi ya kisiasa ni swala la kuangaliwa kwa makini. Maandamano yanayofanywa na CHADEMA na mwitikio wa watu, hali ya maisha ya watanzani kuzidi kuwa mbaya, na CCM kuonekana kuharibika taswira yake mbele ya umma ni mambo ambayo yeyote anayefikiria atashawishika kuamini kuwa kukamatwa na kushtakiwa mara kwa mara kwa viongozi wa cdm na sasa kukamatwa kwa Mbowe kunaweza kuwa na ajenda ya kuzima na kudhoofisha kasi ya mabadiliko nchini.

Kwa msingi huu ni vyema wanasheria wa cdm, viongozi, na wafuatiliaji wa mambo mtuhabarishe kila hatua kuhusu kile kinachoendelea juu ya Mbowe, na viongozi wengine. Nadhani anayefuata kukamatwa sasa ni Dr. Slaa. Tafadhalini tujulisheni, Mbowe anasafirishwaje na lini, na usalama wake unahakikishwaje?
Ndugu yangu kuwa kiongozi wa upinzani kuna maana ya kukaidi amri ya mahakama? Fikira yako kuwa kuweko kwa taifa kutategemea viongozi wa siasa peke yake bila ya sheria? unafikiri Mtikila, Lipumba, Mbatia, Mrema na wote wakubwa wa upinzani wafanye wanavyotaka kuvunja sheria hilo litakuwa Taifa la namna gani? After all ni wewe tu unayelalama lakini huu ni mkakati maalum wa CHADEMA kununua umaarufu hivyo hao viongozi wanajaribu sana kutiwa ndani na kwa vile hawapelekwi Ukonga au Segerea wana wasiwasi wa nini?
 
ndugu yangu kuwa kiongozi wa upinzani kuna maana ya kukaidi amri ya mahakama? Fikira yako kuwa kuweko kwa taifa kutategemea viongozi wa siasa peke yake bila ya sheria? Unafikiri mtikila, lipumba, mbatia, mrema na wote wakubwa wa upinzani wafanye wanavyotaka kuvunja sheria hilo litakuwa taifa la namna gani? After all ni wewe tu unayelalama lakini huu ni mkakati maalum wa chadema kununua umaarufu hivyo hao viongozi wanajaribu sana kutiwa ndani na kwa vile hawapelekwi ukonga au segerea wana wasiwasi wa nini?

kibwengo hiki!
 
Nguvu za jakaya na serikali yake ni nguvu za soda tu, hawaendi popope zaidi ya kufa na kukizika chama chao, ccm kwel sikio la kufa duh! Poleni wanaccm mnaotegemea makubwa!
 
hakuna haki huko majaji anachagua KIKWETE na anaweza kuwatimua kama hakitaka, ni kama mtu unavyoweza kukatiza mkataba kama wa shamba boy wako, na ili ni tatizo la kikatiba hapa yawezekana huyo hakimu ni TV watu wana change channel wanavyotaka huko LUMUMBA ccm headquater, unadhani kuzomewa mchezo, MUKAMA kazomewa kwao.
hakuna haki mahakama za tanzania ni wanyonge kubondwa tu.
mahakimu wanahukumu kwa kusikiliza serikali inataka nini katika kesi, hakuna common sense
mimi sijasoma sheria lakini kuna kesi nyingi ningekuwa hakimu mzuri moja ni hii maana hakini za binadamu ni kitu cha kisheria ni issue ya kuji update tu.
ndio maana mimi naona kufanyakazi serikali ni kuwa kama mke wa mtu. ni kutumika tu na ukileta kujua wanaku kolimba
Ni mahakama gani iliyompa ubunge Kabourou?....Majaji wengi duniani huchaguliwa na rais na kupitishwa na mabunge,
Karibu asilimia 90% ya majaji duniani wanateuliwa na marais wao,kuhusu hili la Arusha wewe niambie ungekuwa hakimu ungeamuaje hili suala?...mshtakiwa wala mdhamini hakuja kortini,wewe unataka hakimu apete?...why?
 
hakuna haki huko majaji anachagua KIKWETE na anaweza kuwatimua kama hakitaka,.
hakuna haki mahakama za tanzania ni wanyonge kubondwa tu.
mahakimu wanahukumu kwa kusikiliza serikali inataka nini katika kesi, hakuna common sense

Labda tujikumbushe hii speech aliyoitoa JK siku ya sheria duniani naweka link hapo chini. Ni siku hiyo hiyo aliyasema haya (casually not written in speech) kwa watu hawa hawa nanukuu " Nawaambieni kabisa atakayepingana na mimi atapata shida sana" Ofcourse he never explained kupingana na yeye how, when, on what? but the message was clear. Viongozi wa vyombo hivi sio kwamba ni wajinga sana but most of them ni fear yakupoteza maisha, kazi au wapendwa wao. Nikumbushe tu kuwa tume inayopendekeza majina ya majaji ilipendekeza majina nakuyapeleka kwa JK na jopo lake kuyapitia, lakini kati ya majina yaliyopelekwa only 40% ndio walipitishwa, 60% yalikuja majina mapya yamependekezwa na kupitishwa huko huko kwa mkuu. Hakuna member wa tume aliyejua yale majina yalipelekwa saa ngapi na nani na yalipatikana kwa kigezo kipi. That being said 60% ya majina yaliyopendekezwa na kupitishwa hayakujulikana yalikotoka. Sasa niambie kama wewe umebebwa kwenye nafasi ambayo unajua huku deserve utafanya tofauti na bosi wako? Now check hii movie ilivyo. Raisi akasema kwenye mazungumzo yake na hao viongozi siku ya sheria duniani "watu wananilalamikia kwanini hawakupendekezwa; mimi nawaambia sijaletewa majina, mimi sio ninayependekeza majina". Hapo akawa anaelekeza lawama kwenye tume ili watu wawaone wabaya. Yaani huyu mtu kwakweli ni sumu kwa nchi yetu, anaruka kabisa asubuhi kweupee. Napata wasiwasi kuwa anaweza akawa anatengeneza mtandao mzuri wakumuokoa yeye na wenzie pale kesi zitakapoanza kuwaandama. Na anajua wazi no one was recording him that day sana sana Ikulu watatoa speech aliyoiongea ambayo hakuweka hiyo mikwala yake in writings. He knows exactly nani yuko kwa interest zake na ambao hawako kwa interest zake lazima awape vitisho. Naamini katika vyombo hivi kunawanaopingana naye (hasa wale wazee waliokuwepo toka zamani) lakini hawaonyeshi. Lakini hawa waliongia kwa fasta fasta tuandike tumeumia labda waamue kujitoa muhanga.

Ikulu Mawasiliano: HOTUBA YA MHE. RAIS - SIKU YA SHERIA NCHINI
 
Ni mahakama gani iliyompa ubunge Kabourou?....Majaji wengi duniani huchaguliwa na rais na kupitishwa na mabunge,
Karibu asilimia 90% ya majaji duniani wanateuliwa na marais wao,kuhusu hili la Arusha wewe niambie ungekuwa hakimu ungeamuaje hili suala?...mshtakiwa wala mdhamini hakuja kortini,wewe unataka hakimu apete?...why?

Ni kweli na hii ni baada yakupendekezwa na tume. Tume inapitia majina, inaangalia uzoefu watu wake, kesi walizokwishakuamua, sifa zao i.e. uwajibikaji, kama anakesi zozote alishatuhumiwa kupokea rushwa etc. Yale majina ndio yanapelekwa kwa raisi kwaajili ya kupitishwa au kukataliwa. Kitu ambacho sielewi kwanini majina yanayopelekwa kwa raisi wetu huwa wanakatwa yanachomekwa yale ambayo hayajapitiwa na tume??? Kama raisi anaona kuna mtu/watu wameachwa kwa haki inakua na ugumu gani ku-raise that issue ili liangaliwe labda kuna kitu/tuhuma zinazowakabili hao watu ndio maana wameachwa au pia labda ni uzoefu mdogo? Hii mambo yukufanya vitu under the rug ndio kunakoleta wasiwasi nakutoaminiana.
 
Back
Top Bottom