Ulinzi wa ajabu Central Police kwa ajili ya Mbowe; asafirishwa kwa ndege ya JWTZ kwenda Arusha!

acheni kelele nyie CDM, huyo kiongozi njaa amevunja sheria sasa nyie mlitegemea nini? acha wamfunge tu huyu mpuuzi. Na jaribuni kufanya fujo, safari hii ni cha moto tu.
 
vijana wote wapambanaji msibaki nyuma kwa hili..mavazi yao yasitutishe Mungu wetu atutetee,nipo maeneo haya naona move yote,freedom is coming soon.

8 months pregnant unafanya nini hapo?
Wakikupiga tulalamike nini tena?
ops,mengine ni kujitakia tu
 
Acheni fujo,hazitawafikisha popote zaidi ya kuwaudhi watanzania wengine wanaopenda haki,
Kama kukamatwa kwake ni kinyume cha sheria,hiyo itajulikana mahakamani,
Sidhani kama watu wanaweza kuvunja kituo cha polisi ili kumtoa Mbowe,mtapoteza hata kuungwa mkono na mashirika na taasisi za haki za binadamu.

Arusha walienda kumtoa nani unadhani?
 
Naona Wanataka machafuko hawa!

Machafuko gani wewe, hii ni Tanzania na wengi wenu ni washabiki tu, maneno mengi lakini hakuna waafrica waoga kama wabongo. Tena safari hii hakuna haja ya bunduki, ni fimbo tu.
 
Aswekwe ndani mpaka aelewe maana ya Mahakama ni nini.

Mbona mmeshindwa kuwasweka ndani mafisadi akina Mkapa, Yona, Karamagi, Chenge, Lowassa, Rostam n.k. au mahakama na polisi zipo kuwadhibiti CHADEMA tu na sio watenda maovu toka chama cha magamba!?
 
Mbona mmeshindwa kuwasweka ndani mafisadi akina Mkapa, Yona, Karamagi, Chenge, Lowassa, Rostam n.k. au mahakama na polisi zipo kuwadhibiti CHADEMA tu na sio watenda maovu toka chama cha magamba!?
wanaccm wanaheshimu mahakama, na wote hao wakiitwa mahakamani basi watakwenda. Kwanini wenu nyie wanadharau mahakama?
 
wanaccm wanaheshimu mahakama, na wote hao wakiitwa mahakamani basi watakwenda. Kwanini wenu nyie wanadharau mahakama?

Alinacha hizo! Ufisadi waliofanya hao niliowataja wote walistahili kuwa jela na kufilisiwa mali zao zote walizopata kiharamu lakini kutokana na nchi kutokuwa na utawala wa sheria hadi hii leo wanapeta tu! Polisi na mahakama wako busy kuwadhalilisha Viongozi wa juu wa CHADEMA kila wanapopata nafasi ya kufanya hivyo.
 
WAZIRI MKUU KIVULIWA SERIKALI YA TANZANIA MHESHIMIWA SANA MBOWE ALIPANGA KUTOA BAJETI MBADALA ITAKAYOPUNGUZA UKALI WA MAISHA KWA WATANZANIA WOTE BILA KUJALI DINI CHAMA,KABILA WALA RANGI LAKINI CHAMA CHA MAFISADI (CCM), KWA VILE HAWAPENDI KUONA WATANZANIA WANAMAISHA MAZURI WAMEONA WASHINIKIZE JESHI KIBARAKA CHA CCM WAMKAMATE ILI ASIWEZE KUHUDHURIA BUNGE LA BAJETI. TUMECHOSHWA NA HIKI CHAMA CHA MAFISADI, MAJAMBAZI,. tUFANYEJE ILI KUKIMALIZA JAMANI
 
Alinacha hizo! Ufisadi waliofanya hao niliowataja wote walistahili kuwa jela na kufilisiwa mali zao zote walizopata kiharamu lakini kutokana na nchi kutokuwa na utawala wa sheria hadi hii leo wanapeta tu! Polisi na mahakama wako busy kuwadhalilisha Viongozi wa juu wa CHADEMA kila wanapopata nafasi ya kufanya hivyo.

Mkuu usiumize kichwa na hao maandazi people,
Wamfanye wamfanyavyo Mbowe ni msaada zaidi katika kuijenga CDM,
Kwa mara nyingine busara za CDM zimedhihirika, sababu huo ulinzi uliopo,
Walidhani CDM wangeandamana hadi pale... hivyo polisi wanaogopa UMMA.
Updates zaidi tafadhali... mleta taarifa Bwana Kamende.​
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Machafuko gani wewe, hii ni Tanzania na wengi wenu ni washabiki tu, maneno mengi lakini hakuna waafrica waoga kama wabongo. Tena safari hii hakuna haja ya bunduki, ni fimbo tu.

As you usual from down stairs.
 
hadi sasa sheria imechukua mkondo wake.

na chadema wanavyojinadi kuwa ni waumini wa sheria. kwa hio watulie ili sheria iendelee kufata mkondo wake.

waende mahakamani na kama wanahoja za kutoa watapambana huko mahakamani.

wasijaribu kutuharibia nchi, maana dola kwa nguvu zake zote itasimama kuhakikisha inalinda amani ya nchi, kwa gharama yoyote ile, nchi haitoweza kuacha wale magoi goi kuifanya nchi yetu kama haina sheria za kuiongoza.

poleni sana wanachadema, ila mnatakiwa na nyny kama wapenzi kwa viongozi wenu kuwashauri kufata sheria, na kama wanaona sheria haziko fair watumie bunge na njia halali kurekebisha sheria hizo ili zisomeke ktk wanachoona wao kuwa ni sawa.

Nakupa pole wewe usiyejua mwenye dola ni nani. Pia fikiri kidogo mwisho wa yote mnataka kufanikisha nini?
 
8 months pregnant unafanya nini hapo?
Wakikupiga tulalamike nini tena?
ops,mengine ni kujitakia tu

Mkuu muache Shosti atupe kampani,
Hebu vuta picha enzi zile college, kwenye harakati,
Mnapoandamana na mashosti wapo, gadhabu inazidi!
Nguvu ya kusonga inaongezeka maradufu......
 
Ndugu yangu kuwa kiongozi wa upinzani kuna maana ya kukaidi amri ya mahakama? Fikira yako kuwa kuweko kwa taifa kutategemea viongozi wa siasa peke yake bila ya sheria? unafikiri Mtikila, Lipumba, Mbatia, Mrema na wote wakubwa wa upinzani wafanye wanavyotaka kuvunja sheria hilo litakuwa Taifa la namna gani? After all ni wewe tu unayelalama lakini huu ni mkakati maalum wa CHADEMA kununua umaarufu hivyo hao viongozi wanajaribu sana kutiwa ndani na kwa vile hawapelekwi Ukonga au Segerea wana wasiwasi wa nini?

Usamehewe hujui ulicho kiandika.
 
Hee! Unanishangaza kweli kweli! Mbona serikali ya CCM mara nyingi tu imekuwa ikikaidi amri halali za mahakama? Tena nyingine za mahakma kuu? Au sasa unajifanya hulijui hilo?

Isitoshe serikali hii ya CCM ndiyo mvunjaji mkuu wa utawala bora na haki za binadamu. Nalo hulijui hilo? Wewe ni kipofu? Kiziwi. Husomi magazeti? Husikilizi radio? Hutazami TV?
 
Back
Top Bottom