Bollo Yang
JF-Expert Member
- Aug 10, 2009
- 440
- 50
Haijawahi tokea Central kukawa na ulinzi kama huu.
Kituo kikuu kimezingirwa na askari wa kutuliza ghasia wengi sana ambao wote wamejitanda vizuri sare za kivita na bunduki mikononi mwao. Hakuna ruhusa ya mtu yoyote kuingia ndani ya kituo.
Viongozi wa CHADEMA wamehoji kuhusu namna Mbowe atakavyosafirishwa kwenda Arusha wakajibiwa kuwa hilo ni juu ya jeshi. Watamsafirisha kwa usafiri wa jeshi kwa saa wanayotaka wao.
Inaonekana kuwa watamsafirisha usiku huu huu ama alfajiri sana kesho. Kuna wasiwasi kuwa watamchoma sindano ili apoteze fahamu hadi atakapofikishwa Arusha.
Lolote litakalotokea sisi tunaamini kuwa saa ya Mungu ya kuikomboa Tanzania imefika.
============
UPDATED:
Wakuu,
Dakika tano zilizopita (Juni 6, 2011) saa 1:35 ndege ya jeshi iliyombeba Freeman Mbowe imetua Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro International Airport. (KIA)
Sasa ndo wanapanga msafara kwa ajili ya kumsafirisha kwenda Arusha Mjini.
Hyperbole