Ulinzi na usalama wa tarakishi (computer ) yako | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ulinzi na usalama wa tarakishi (computer ) yako

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Aug 20, 2011.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Kadri ya siku zinavyosonga mbele , tekinologia kukuwa zaidi , kuja kwa programu nyingi na mbalimbali za kutumia katika kompyuta na hata vitu vingine vinavyounganishwa na kompyuta ndio matishio mbalimbali ya usalama dhidi ya tarakishi yako yanazidi kuongezeka toka Nyanja mbalimbali za utendaji wa kazi .
  Mfano zamani watu walikuwa wanaogopa zaidi kubadilishana vifaa vya kuhifadhia taarifa kama floppy disk kwa sababu ya virus baadaye ikaongezeka ujio wa mtandao wa kimataifa unaounganisha tarakishi ulimwenguni ( internet ) napo virus na uhalifu mwingine umetokea huko, kwa sasa hivi watu wanatumia simu zao za mikono kuhifadhi taarifa na vitu vingine virus wanahama toka kwenye simu kuingia kwenye tarakishi au toka kwenye tarakishi kwenda kwenye simu za mikono na vifaa vingine vya mawasiliano .
  Kutokana na visa hivyo hapo juu , kuna njia mbalimbali unaweza kuzitumia kwa ajili ya kuboresha usalama wako unapokuwa kwenye mtandao na tarakishi yako au unapopokea vifaa vya nje kama flashdisk .
  Kitu cha kwanza kujua ni kwamba matishio ya usalama dhidi ya tarakishi yako na vifaa vyake hutegemea na mazingira ya kazi ya kifaa hicho kwa kila siku au mara kwa mara .
  Kwa mfano mtu anayefanyakazi kwenye huduma za sectretarial matishio yake zaidi yapo kwa wale wanaoleta kazi kwa njia ya vifaa vingine kwa ajili ya kuja kufanyiwa kazi na yeye na hapo hapo unakuta kwa muda mrefu hana huduma ya mtandao kwa ajili ya kuboresha programu za tarakishi yake kama antivirus , firewall na program nyingine za kufanya kazi .
  Matokeo yake ni kwa tarakishi hiyo kuvamiwa na virus wapya wanaotolewa kwenye mtandao na kuhamishwa kupitia flashdisk kuja kwenye tarakishi yake mara kwa mara na saa nyingine ni pale anaposhindwa kuboresha baadhi ya program kwa njia ya updates napo program hizo huleta taabu mbeleni .
  Yule ambaye anafanyakazi kwenye ofisi zenye tarakishi nyingi zilizounganishwa kwenye mtandao labda hapo hapo ( LAN ) au wa mbali(WAN )na matishio yake ni tofauti na Yule mchapa karatasi wa steshenari nitaeleza hapa chini .
  Ndani ya ofisi unakuta hakuna maelezo ya matumizi ya tarakishi ( terms of use ) na maelezo mengine kuhusu taratibu za kutembelea mitandao na programu zinazoingizwa kwenye tarakishi hizo haswa zile zilizounganishwa na mtandao kama ni wa LAN au WAN .
  Shida ya kutokuwa na miongozo na maelezo mengine kuhusu matumizi ya tarakishi na mitandao ndani ya maofisi ni kwamba mtu anaweza kuingia na tarakishi yake binafsi iliyoshambuliwa na wadudu kuja kuunganisha na mtandao wa ofisi na kuleta maradhi kwenye mtandao wa ofisi .
  Muda mwingine mtu anaweza kuingia kwenye tovuti za ajabu ajabu akapata madhara huko lakini yeye asione kwa kipindi hicho lakini madhara yakasambaa kwa njia ya mtandao kwenda kwenye tarakishi za wengine kwa njia ya mtandao kwa kujua au kutokujua .
  Mwisho wa siku ni pale mtu kwa kukosa miongozo kuingiza program zake ambazo haziruhusiswi mwenye tarakishi yake na kwa wengine ndani ya mtandao wa ofisi matokeo yake ndani ya mtandao wa ofisi kunaweza kutokea tatizo lilisababishwa na hilo na ni ngumu kulimaliza angalau kwa kipindi kifupi .
  Mtu mwingine ni huyu ambaye hana huduma ya mtandao nyumbani kwake au kazini kwahiyo analazimika kwenda kwenye migahawa ya mtandao yaani internet café , kwa uzoefu wangu internet café nyingi haziko salama na ni rahisi kutoa maradhi humo kwenye café na kuyabeba kwa njia ya flash au kwa mtandao kwenda maeneo mengine kwa urahisi zaidi kuliko sehemu yoyote ile .
  Ndani ya internet café mtu huyu anaweza kuibiwa taarifa zake za benki kama akiombwa kufanya hivyo kutumia tovuti bandia za bidhaa mbalimbali ingawa hii mtu anaweza kufanya hata akiwa kwenye tarakishi yake nyumbani au ofisini au popote pale inategemeanana huduma za ulinzi zilizowekwa kwenye tarakishi hiyo .
  Mtu wa mwisho ni Yule mlinzi wa tarakishi hizi katika shuguli zake za kila siku na mshauri katika maofisi nasehemu zingine za shuguli kama vyuoni na kwa watoa huduma za mitandao ( ISP )wengi wetu sio washauri wazuri tunatanguliza fedha mbele kuliko huduma matokeo yake ni kufuata huduma kwa majina au namba kama 2012 na sio ubora wa program yenyewe kwa kipindi hicho na matishio yaliyokuwemo kwa kipindi hicho .
  Kwa kumalizia naweka vionjo muhimu kwa ulinzi wa tarakishi yako .
  1 – Hakikisha unatumia program unazojua chanzo chake na unapozipata hakikisha leseni zake ni sahihi kwa kudhibitisha usajili wake kwa njia ya mtandao .
  2 – Hakikisha tarakishi yako inaingia kwenye mtandao kwa ajili ya kuboresha program zako haswa Antivirus au Internet Security angalau masaa 3 kila wiki , unapoboresha program hizi unakuwa na uhakika wa ulinzi na usalama na kifaa chako kwa asilimia kubwa .
  3 – Kuwa na program nzuri na za kisasa kwenye tarakishi yako haimaanishi tarakishi yako haiwezi kufa kesho au kifaa katika mashine hiyo hakiweza kufa kesho au saa hiyo hiyo.
  4 – Hakikisha unakuwa na umeme mzuri unaoingia na kutoka ndani ya kifaa chako kwa kuwa na UPS na Stabliser na umeme uko sawa madhara ya kutokuwa na vifaa hivi ni kuharibu vifaa kama powersupply , battery na motherboard au hata kuonguza kabisa .
  5 – Kama unatumia sana mtandao kwenye shuguli zako hakikisha una vitu vinavyoweza kukuonyesha ubora wa kurasa za tovuti unazotembelea au kutafuta mara kwa mara ili unapokumbana na tovuti bandia au yenye madhara basi program hiyo ikupe taarifa mapema .
  Wakati mwingine zinaitwa viongezeo ( addons ) kwenye browser ( kivinjari ) ingawa sio antivirus zote au internet security zenye huduma hizi lakini kwa sasa ni nyingi zina huduma hizo .
  6- Kuna program ndogo ndogo zinazoitwa utilities kwa ajili ya kufanya mambo kadhaa kwenye tarakishi kama kufuta program , kukagua registry na mfumo mzima wa tarakishi na kurekebisha hizi pia ni nzuri sana kwa ajili ya afya ya tarakishi yako .
  7- Wakati mwingine tarakishi yako haswa windows xp na vista zinakuwa na tabia za ajabu ajabu kama kwenda taratibu na kufungua kurasa za mtandao ambazo zinakulazimisha kuangalia mara nyingi hayoni mashambulio ya SPYWARE ni vizuri kuwa na Antispyware ingawa Internet Security nyingi huwa na Antispyware .
  8 – Mwisho kabisa hakikisha program unazoingiza kwenye tarakishi yako zinaendana na tarakishi yako mfano unapotumia Autocad 2011 unatakiwa kuwa na Memory ( RAM) ya angalau GB 3 wewe ukawa na GB 1 ujue utapunguza utendaji wa program yako hata unapofanya update unaweza kujikuta inakuwa taratibu zaidi hii pia iko kwenye Antivirus na Programu nyingine za Kitaaluma .
  9- Hakikisha unazima huduma za wireless au Bluetooth kwenye laptop yako au simu za mikononi haswa unapokuwa sehemu za zenye watu wengi na mikusanyiko ya watu kwa ajili ya usalama zaidi ingawa unaweza kuzitumia kwa tahadhari.
  10 .Funga ( disable) programu zote zinazosaidia watu kushusha program au chochote ( download ) moja kwa moja toka kwenye mitandao mbalimbali ukiacha wazi programu hizi ni rahisi kushusha virus na vitu vingine kwa sekunde kadhaa na kudhuru tarakishi yako .
  Kama umeona unashindwa kukagua vichomekwa kwenye tarakishi yako kama flashdisk kwa njia ya full scan basi weka quick scan kwa ajili ya kukagua kila kifaa kinachochomekwa kwenye tarakishi yako .
  Maelezo haya niliyoyatoa ni zaidi kwa watumiaji wa Operating system za Windows kuanzia xp mpaka 7 ingawa mengine yanafanana haswa kwenye masuala ya umeme .
  Kama una maswali , maoni na maelezo ya nyongeza unaweza kuongezea chini kwenye mada hii nashukuru kwa kusoma mpaka hapa .
  Wasiliana

  Yona f maro 0786 806028 yonamaro@alarmtechtz.com
   
 2. Gurta

  Gurta JF-Expert Member

  #2
  Aug 20, 2011
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 2,246
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Safi sana hii mkuu na matumizi ya kiSwahili yamenifurahisha zaidi, niko mobile ningekupa 'like'
  Zawadi yako hii, floppy disk inaitwa 'diski tepe' kwa kiSwahili
   
 3. IHOLOMELA

  IHOLOMELA JF-Expert Member

  #3
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 830
  Likes Received: 360
  Trophy Points: 80
  Mkuu nimependa ulivyotumia lugha yetu tamu ya kiswahili..nimeamini kuwa kiswahili ni lugha inayokuwa na kupambana na changamoto za mabadiliko ya kitekinolojia.! Kwa ujumla, makala nimeielewa vizuri na yote uliyoyaelezea ni ya msingi kabisa. Hongera na Asante sana
   
 4. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #4
  Aug 20, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,642
  Likes Received: 2,874
  Trophy Points: 280
  Tarakishi au tarakilishi? Nimekuwa nikijua ni tarakilishi
   
 5. M

  Mulugwanza Member

  #5
  Aug 20, 2011
  Joined: Feb 3, 2008
  Messages: 89
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 15
  Asante kwa darasa mzee!
   
 6. Mwendabure

  Mwendabure JF-Expert Member

  #6
  Aug 20, 2011
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,054
  Likes Received: 296
  Trophy Points: 180
  <br />
  <br />
  Nawe pia mkuu umenikuna kwa kumpongeza kwa kiswahili. Zawadi yako hiyo mobile(simu ya mkononi) ni "rununu" asante.
   
 7. saidomr

  saidomr Member

  #7
  Aug 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimejifunza mengi,
   
 8. HT

  HT JF-Expert Member

  #8
  Aug 20, 2011
  Joined: Jul 29, 2011
  Messages: 1,899
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tarakilishi
   
Loading...