Ulinzi mlimani city

Mtanzania haswa

JF-Expert Member
Oct 31, 2010
663
99
Ufikapo kwenye geti la kuingilia mlimani city kama una gari unapewa kadi na wale askari geti wa OMEGA NITRO. Kadi hiyo nyuma imeandikwa "Omega Nitro (T) and mlimani holdings accept no liability for damage or losses to vehicles and personal property. Parking is at owner's risk" Sasa kampuni hii ya ulinzi pale mlimani city inalipwa pesa kwa kazi gani, kutoa card? kama si ufisadi mwingine ni nini? NI HAYO TU WADAU
 
Kweli kwa namna hii hatufiki, nafikiri siku akikamatwa mwizi pale akauawa na wananchi wenye hasira labda management ya mlimani city watabalishisha mfumo wao wa ulinzi.
 
Kumbe ndo imeandikwa ivyo yaani abiria chunga mzigo wako imekuwa basi.Kuna haja ya kuwabana wabdili huo upupu mi naacha gari nachoma ndani nkikuta halipo wao hawahusiki sasa si uhuni huo?
 
No, hawa jamaa kamwe hawataweza kuchukua hatua kama tunavyotaka kwa sababu ile centre au huduma zipatikanazo pale wao ndio wanaonekana wako peke yao. Kwa kifupi wateja hawana sehemu nyingine ya kwenda ndio maana wanafanya mchezo huu. Kama kungekuwa na shopping malls nyingi, basi wangelazimika kuwajibika. Labda nitoe mfano; Mie nikienda dukani, customer care ikawa yakipuuzi au nikagundua nimeibiwa, basi duka hilo sikanyagi tena. Na hiyo haiishi hapo na waambie na wengine lililotokea na wao wataamua au kuchukua tahadhari. Vivyohivyo, mlimani city wanaamini watu kwenda pale hawana choice, wataibiwa na kurudi. Kwa sasa hivi nashauri tusemee saana tusichoke, lakini pia kama kuna uwezekano wa kupata huduma sehem ambazo ni salama twende huko tuone kama hawatarekebisha hali hii. Na tukilazimika kwenda pale, basi, tuhakikishe usalama wa mali zetu ni wa hali ya juu sisi wenyewe. Kwa maana wao wanashindwa hata kuweka CCTV kukawa na watu 2-3 wanaoperate na ingekuwa rahisi kuone wizi unapotendeka.
 
Najiuliza hivi kadi wanazotoa ni za nini? Wanasheria tusaidieni.
Kumbe walinzi wanaweza waka conspire kuiba gari! Hatari kweli kweli.
 
Hii sehemu inalalamikiwa miaka nenda rudi ingekua watu wa kusikiliza wangekua wameshajirekebisha hapa cha muhimu ni kubadilisha system nzima ya ulinzi pale ikiwezekana hata kampuni ibadilishwe maana management ya kampuni iliyopo imeshindwa kazi nadhani wanapewa 20%
 
Jamani kwa mara ya kwanza nimebahatika kutoka nje ya nchi yangu hii, nimebahatika kutembelea Malaysia kwa kifupi kama uhuru tulipata nao kipindi kimoja na ilikuwa iko kwenye nchi za dunia ya tatu lakini sasa hawapo tena kwenye dunia ya tatu wan bara bara nzuri ukienda shopping malls zao kama una gari yako hata ukiliacha hadi kesho kutwa utalikuta kama ulivyoliacha, nimebahatika kutembelea karibia shopping malls nyingi tu na ktk sehem ya parking wenzetu wamesambaza CCTV kama njugu (zipo kila kona) Tukirudi hapa kwetu hivi kweli hawa jamaa wanashindwa kuweka hizo CCTV hata kama ni mbili, moja geti ya kuingilia na nyingine geti la kutokea ili endapo kukitokea na issue yeyote ya kiusalama iwe rahisi kutrace hiyo issue.
 
Baada ya miaka miwili mlimani city itaelekea kuwa kama kariakoo, kila abiria chunga mzigo wako/
 
Baada ya miaka miwili mlimani city itaelekea kuwa kama kariakoo, kila abiria chunga mzigo wako/

hali ipoje kwa sasa manake mimi sijawahi kufika huko kifupi ni.miongoni mwa watu mnao waita wa mikoani
 
Back
Top Bottom