samirnasri
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 1,388
- 213
Uzinduzi wa chuo kikuu cha dodoma umefanyika leo katika ukumbi wa chimwaga chuoni hapo. Katika hali isiyo ya kawaida ulinzi uliimarishwa hasa katika ukumbi huo wa chimwaga. Usalama wa taifa walimwagwa kila kona ya chuo hicho. Sio kila mtu aliruhusiwa kuingia kwenye ukumbi huo bali ni watu wachache waliopewa kadi maalumu. Wahadhiri hawakua limited kuingia japo nao walipewa kadi maalumu walizozitumia kuingilia ukumbini. Ukiachilia mbali wageni waalikwa, ni wanafunzi wachache waliruhusiwa kuingia ukumbini kwa kadi maalumu jambo lililosababisha ukumbi huo wenye uwezo wa kuingiza watu takriban elfu tatu kupwaya huku viti vingi vikiwa tupu. KUBWA KULIKO YOTE ni kwamba milango ya kuingilia ukumbini iliwekewa vifaa maalumu vya ukaguzi ambapo kila aliyekua akiingia alikaguliwa na kuonesha kile alichokua nacho. NAJIULIZA ULINZI WOTE HUU WA NINI KWANI TANZANIA TUMEFIKIA MAHALI HAPO..naomba maoni yenu.
Hapo ndipo tulipofika watanzania, ukiona ulinzi kiasi hicho kwa rais wa tanzania, wewe mwananchi wa kawaida unatakiwa kutafakari zaidi, hiyo si dalili tu ya usalama wake uko hatarini bali ni usalama wa nchi hii upo hatarini pia. sasa kama kawa watz tunaamua kuacha kutafakari jambo kwa ukubwa wake na kuachia hisia zetu na chuki kutufanyia maamuzi basi tusubiri saa.
jk wala asiogope tanzania ni nchi ya amani vipi jamani yule mchakachuaji thobias mwesigwa alikuwepo je amekabidhi lile tamko!