Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,054
- 463,971
Mtunzi Nyemo Chilongani SEHEMU YA 01
Sijui nianze kusema nini ili nieleweke, sijui kama ninatakiwa kucheka au kulia kwani kwa kile kilichotokea, ningependa Mungu anisemehe tu.
Kwa jina ninaitwa Steven Edward, mimi ni kijana niliyebahatika kupata msichana mzuri aitwaye Juliet ambaye baadae alikuja kuwa mke wangu niliyempenda sana kabla mambo hayajakwenda kombo.
Kwa Juliet, nilikuwa nimefika, alikuwa mwanamke niliyempenda kuliko wanawake wote duniani, nilimthamini na kumsikiliza kwa kuwa sikuwa na mwingine zaidi yake.
Juliet alikuwa mzuri kila mahali, tukianzia nje mpaka ndani (Nadhani hapo unaelewa namaanisha nini).
Nilidumu na Juliet kwa miaka minne ya ndoa, hakuchuja, bado alikuwa mzuri vilevile, nahisi kwa sababu nilikuwa na fedha hivyo mambo madogomadogo ya make up yalikuwa yakinunuliwa sana.
Nilipoona kwamba kila siku nazidi kulewa kwa mapenzi yake, nikaamua kumnunulia gari la kifahari. Juliet akawa Juliet bwana, mtaani alikuwa akitamba yeye tu. Ana usafiri wa maana, hakanyagi tena ardhini kwa kutembea mwendo mrefu, sasa kwa nini asinione mimi wa thamani?
Ukiachana na gari, nilimnunulia vitu vingi ambavyo alitakiwa kuwa navyo huku nikimfungulia biashara nyingi zilizomfanya kufurahia maisha yake.
Daah! Juliet mke wangu! Hivi ulikosa nini wewe shetani? Au ulitaka nikufanyie nini ili ujue nakupenda?
(Nanyamaza na kuanza kulia kwa pozi, kisha naendelea)
Baada ya kukatika miaka minne ya ndoa yetu huku tukiwa tumepata mtoto wa kike, Magreth, mwaka 2012 ukaingia, siku hiyo ndiyo ilikuwa mwanzo wa majanga yote yaliyosababisha haya yote, ngoja nijaribu kukusimulia, nitakapoishia, naomba mnisamehe kwa kuwa jambo hili linaniuma kupita kawaida.
JANUARI 1
Siku hii ilianzia usiku, nakumbuka siku hiyo nilikuwa na Juliet chumbani kwetu huku tukiwa tumekumbatiana na kupeana mabusu mfululizo. Tulitaka mwaka mpya wa 2012 utukute tukiwa tumekumbatiana namna hiyo.
Kweli bwana, saa ilipogonga na kutuambia kwamba ilikuwa ni saa sita kamili usiku huku siku ikiwa imebadilika, nikammwagia mabusu zaidi.
“Ninakupenda mke wangu,” nilimwambia.
“Ninakupenda pia.”