Pumba. Asante kwa kunipotezea muda na kujaza seva ya JF...Hauna makosa! Hauna mawaa kwa kizungu tunaweza kusema no errors no faults. ...najua utasema kuwa Mungu kasema hakuna mkamilifu!
Kumbuka kasema hakuna mkamilifu la hata mmoja akimaanisha mwanadamu sio roho. Makosa ya kiutendaji,makosa binafsi, makosa ya kukusudia na kutokusudia , habari za bahati mbaya na maneno kama heri ningejua....! Haya yote si ya kiroho ni ya kimwili
Ukisoma habari za jicho la tatu, machale ,ndoto taarifa ufunuo na maono unaona kwa usahihi kabisa ulimwengu wa roho ulivyotutangulia kufahamu yajayo kabla ya nafsi zetu kupata taarifa rasmi
Kila tukio liko preplanned. Hakuna bahati mbaya, ni limitations za ufahamu tu wa kibinadamu ndio umezuiwa kuona haya
Maisha yako na yangu yako kwenye mchoro kamili tangu kuzaliwa mpaka kufa...........
Utazaliwa lini na nani utapitia nini na wapi utakutana na nani! Utakuwa nani, utafanya nini, utaanguka wapi na kusimama wapi! Yote haya hayatokei kwa bahati mbaya
Jee huu ni ubaguzi?
Kwamba mmoja tangu kuzaliwa mpaka kufa yeye ni mafanikio tu?
Kwamba tangu kuzaliwa mpaka kufa ni yeye na matatizo matatizo na yeye?
Kwamba wengine husimama na kushamiri kisha huanguka na kupotea kabisa?
Kwamba wengine hukulia kwenye shida nyingi na matatizo lakini huja kutoboa na kutoka kimaisha?
Ulimwengu wa roho hauyumbishwi...formula zake ziko kama zilivyo michoro yake ni kamili na kamilifu unapojaribu kuisahihisha na ishu za waganga nyota na ngekewa unajitafutia dhahama usiyoiweza
Utafanikiwa kwa kipindi tu lakini asili itakurudisha kwenye shina lako kiroho..pale ulipotakiwa kuwa na hapo ni sawa na kujaribu kunyoosha bati lililopinda na kupondeka
Ulimwengu wa roho hauna modifications! Ishi maisha yako ukijibidiisha na ufanyayo katika mstari sahihi...usijaribu kutoka nje ya mstari kwa kuchanganya ya rohoni na ya kidunia ...hutafika mbali
[emoji115] [emoji115] [emoji125] [emoji125] [emoji125]Bado nauwaza ule msonyo wa juzi alfajiri[emoji24] [emoji24] [emoji24]
Uniletee manyoka yako[emoji125] [emoji125][emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji115] rudi apa
Tena hawa ni Foreman na supervisor ndo walikuwa wakitaka kuniharibia kazi cha ajabu wakajikuta wanapewa makavu na BossMungu hajawahi kushindwa na matendo ya mwanadamu na mambo yake yote! Kwakuwa vyote ni uumbaji wake
Hivi ulimwengu Wa roho ndo ulimwengu gani jamani? Tujuzani jamini sisi wengine hatuamini uwepo Wa munguKama uyasemayo ni kweli basi mafundisho yoyote yanayo amini ktk hukumu ya mwisho si yakweli....[emoji41]
Kama tangu kuzaliwa ramani yako ya maisha imechorwa na huwezi badili lolote ktk ulimwengu wa roho, kwa nini kuwe na hukumu???
Najaribu kuwaza tu!
Leo Mshana nakupinga 100%. Kama kila kitu kimeshapangwa basi kuwa na dini hakuna maana kwa vile dini zinatuambia tutende mema. Hapangekuwa na haja ya ibada wala kufunga iwe Ramadhani au Kwaresima. Dhambi ni tendo analolifanya mtu kwa kudhamiria-yaani kwa UAMUZI WAKE. Unaposema kila kitu kimepangwa una maana hata dhambi mtu anazofanya ambazo anaamua kuzifanya yeye mwenyewe kwa utashi wake ni kitu kilichokuwa kimepangwa? Nonsense. Sema Mungu ametupangia kila mmoja maisha mema (na kumpa kila mtu kipawa fulani cha kumfanikisha maishani), lakini shetani (kupitia binadamu wenzetu) anazuia mafanikio Mungu aliyotupangia. Kwa hivyo, mipango Mungu aliyotupangia kweli ipo (na ni mizuri) lakini sio kwamba eti kama ni uovu basi ni Mungu amemuumba mtu ili awe nao. HAPANA. Mungu amemuumba KILA MTU afanikiwe ila ni shetani tu anayeharibu.
Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.Anachosema mshana jr ni kweli kulingana na bible. Biblia imeelezea predestination/kukusudiwa kimbele. Ndio maana Mungu alisema shukuruni kwa kila jambo. Liwe jema au baya tushukuru tu kwa sababu yeye ndiye kila kitu.
Ukitaka kuangalia pre destination kwenye Maisha yako chunguza hili. Ulipokuwa mtoto mdogo wakati ukikua uliwa na kupanga mambo mengi nanpengine kufikiria ungekuwa nani baadaye. Ungeoa mke yupi, watoto fulani, nyumba fulani etc.
Lakini leo almost mambo sivyo yalivyo salaaleh! Mahali ulipo hukuwahi kupawazia, status uliyonayo hukuwahi kuifikiria kabla, mke, watoto, mali na maisha kwa ujumla siyo yale uliyowazia zamani. Hii inaashiria nini??? PREDESTINATION.
Tangu unakuja Duniani ulishapangiwa njia ya kupita na huwezi kuikwepa. Hapa chini ni mfano wa pre destination unaoongelewa na Biblia:
Waefeso 1:3-5
[3]Atukuzwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo, aliyetubariki kwa baraka zote za rohoni, katika ulimwengu wa roho, ndani yake Kristo;
[4]kama vile alivyotuchagua katika yeye kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili tuwe watakatifu, watu wasio na hatia mbele zake katika pendo.
[5]Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake.
Kwa hiyo ukijiona ni mkristo leo hujifanyi hivyo, bali ulishakusudiwa hilo tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu. Maana yake alikujua na kukuchangua kimbele ili uwe hivyo. Kwakuwa anajua mwisho kabla ya mwanzo ndio maana alikuwekea njia ya wewe kufikia kile alichokukusudia. Hilo ni kweli kabisa
Mshana Jr kabla sijakuumbaMilka Kakete- KABLA SIJAKUUMBA
Dah..... Wahubiri huwa Wanajichanganya sana...... Ukifikiria kwa utulivu utaona dini ni zaka na sadaka tu[emoji87] [emoji87]kwahiyo maisha tayari yapo framed, sisi tunafuata tu kama train kwenye railway!, kwahyo mfano jambazi yeye alipangiwa atazaliwa, ataishi itafika muda ataiba ataua halaf mwisho wa siku motoni, na wengine reli yao imenyooka hadi peponi!?
Kuna baadhi ya makanisa hawafundishi mambo ya kiroho kabisa ila makanisa ya kilokole haya mambo wanajitaidi kwa kweli kufundishaDah..... Wahubiri huwa Wanajichanganya sana...... Ukifikiria kwa utulivu utaona dini ni zaka na sadaka tu[emoji87] [emoji87]
Ujamuelewa vizuri na Mimi nilipoanza kusoma nikabaki nashangaa nimefuatilia reply zake zote anamaanisha kuwa kabla ujazaliwa Mungu anakuwa amekupangia njia yako utayopitia hadi utakapo kufa na njia hii ni njema maana mwishowe tutauona ufalme wa Mungu.Leo Mshana nakupinga 100%. Kama kila kitu kimeshapangwa basi kuwa na dini hakuna maana kwa vile dini zinatuambia tutende mema. Hapangekuwa na haja ya ibada wala kufunga iwe Ramadhani au Kwaresima. Dhambi ni tendo analolifanya mtu kwa kudhamiria-yaani kwa UAMUZI WAKE. Unaposema kila kitu kimepangwa una maana hata dhambi mtu anazofanya ambazo anaamua kuzifanya yeye mwenyewe kwa utashi wake ni kitu kilichokuwa kimepangwa? Nonsense. Sema Mungu ametupangia kila mmoja maisha mema (na kumpa kila mtu kipawa fulani cha kumfanikisha maishani), lakini shetani (kupitia binadamu wenzetu) anazuia mafanikio Mungu aliyotupangia. Kwa hivyo, mipango Mungu aliyotupangia kweli ipo (na ni mizuri) lakini sio kwamba eti kama ni uovu basi ni Mungu amemuumba mtu ili awe nao. HAPANA. Mungu amemuumba KILA MTU afanikiwe ila ni shetani tu anayeharibu.
I don't agree. Where is free will?Kabla sijakuumba katika tumbo nalikujua, na kabla hujatoka tumboni, nalikutakasa; nimekuweka kuwa nabii wa mataifa.
Yeremia 1 : 5