Ulimwengu wa Bernardo Mukassa katika nyimbo za Kikatoliki (RC) Tanzania

Naunga mkono hoja.... ukiangalia videos ndio utaona changes kubwa zaidi muda si mrefu wataaanza kuvaa tight na baadae vichupi kwenye vidz
 
Sure. Japo mabadiriko ya tabia nchi hayazuiliki nadhani ndio tatizo
 
kwa wale wanaopenda kwaya za kikatoliki, Bernad Mukassa si mgeni kwao, yeye ni mwalimu wa kwaya ya Mt. Kizito makuburi, ni mtunzi alijizolea sifa nyingi kwa utunzi wake wa nyimbo. hata ukichukua albam za kwaya nyingi huwezi kukosa wimbo wa Mukasa, licha ya kuwa mtunzi bora ila kwa upande wangu mimi naona MUKASA, na wenzake kama VICTOR MURISHIWA, E.L MKUDE, E.F JISSU, MANOTA na watunzi wengine wanaochipukia wanaanza kuharibu ladha ya muziki wa kikatoliki kwa kuingiza vionjo na free organ za ajabu ajabu, kwa mfano wimbo uitwao KIDOLE JUU ngoma zake zimechukuliwa kutoka kwenye wimbo wa kihindi uitwao GOLOGOLO na nyimbo nyingine nyingi ambazo MKUDE amekuwa akicheza KINANDA amekuwa akiiba free organ za nyimbo za dunia.Nyimbo za watunzi hawa nyingi zimekuwa ni za kasi yaani 6/16, badala ya nyimbo za kutafakarisha ambazo zilikuwa zikitungwa na JOHN MGANDU, DEO KALOLELA, MARCUS MTINGA,A.NGURUMO, J.MAKOYE, SEVERIN SWILLA na wengine ambapo nyimbo nyingi zilikuwa na mwendo wa 4/4, 2/4,3/4 na 3/8. vilevile watunzi hawa wamezidisha nyimbo mpya kila siku kanisani kama inawezekana nyimbo za kuuzia albam zisipigwe kanisani.
tunataka ile ladha ya kikatoliki irejeee
Umemsahau F Mwarabu, Lukando, F Nyundo na wengine wengi.
 
Uyo baba sinaneno kabisa hicho no kipaji haaishii huko katoliki tu pia ni mwalimu anaye pokea mialiko kwaya zingine na anafundisha
 
nashukuru ndugu yangu nitasali huko siku moja. i really miss that...hiyo atmosphere huwa inanipeleka straight mbinguni. niko dar lakini naomba nijulishe mavurunza ni maeneo gani hasa.. nitashukuru kwa taarifa.
IPO kimara suka. Upande wa kushoto kama unatokea mbezi
 
Kwa sasa watunzi wa nyimbo za Katoliki ambao wamekuwa wakiniinjilisha vilivyo kupitia nyimbo zao; ni wengi!

Ila kwa uchache ni David Wasonga, Beatus Idama, Ben Nturama, F. E. Nyanza, Isaack Mwita, Ansbert Ngurumo (ingawa siku hizi hasikiki tena baada ya kukimbilia uhamishoni), Ernest Ogeda, Didas Kidesu (yuko Kanisa la mshindo huyu pale Iringa mjini), na wengineo wengi!

Hakika hawa pamoja na wenzao wengi kwa sasa ndiyo hazina ya Kanisa. Maana wanajitahidi kutunga nyimbo zinazifanana na za watunzi wa zamani kama John Mgandu, nk.
 
kwa wale wanaopenda kwaya za kikatoliki, Bernad Mukassa si mgeni kwao, yeye ni mwalimu wa kwaya ya Mt. Kizito makuburi, ni mtunzi alijizolea sifa nyingi kwa utunzi wake wa nyimbo. hata ukichukua albam za kwaya nyingi huwezi kukosa wimbo wa Mukasa, licha ya kuwa mtunzi bora ila kwa upande wangu mimi naona MUKASA, na wenzake kama VICTOR MURISHIWA, E.L MKUDE, E.F JISSU, MANOTA na watunzi wengine wanaochipukia wanaanza kuharibu ladha ya muziki wa kikatoliki kwa kuingiza vionjo na free organ za ajabu ajabu, kwa mfano wimbo uitwao KIDOLE JUU ngoma zake zimechukuliwa kutoka kwenye wimbo wa kihindi uitwao GOLOGOLO na nyimbo nyingine nyingi ambazo MKUDE amekuwa akicheza KINANDA amekuwa akiiba free organ za nyimbo za dunia.Nyimbo za watunzi hawa nyingi zimekuwa ni za kasi yaani 6/16, badala ya nyimbo za kutafakarisha ambazo zilikuwa zikitungwa na JOHN MGANDU, DEO KALOLELA, MARCUS MTINGA,A.NGURUMO, J.MAKOYE, SEVERIN SWILLA na wengine ambapo nyimbo nyingi zilikuwa na mwendo wa 4/4, 2/4,3/4 na 3/8. vilevile watunzi hawa wamezidisha nyimbo mpya kila siku kanisani kama inawezekana nyimbo za kuuzia albam zisipigwe kanisani.
tunataka ile ladha ya kikatoliki irejeee
Aisee... Kumbe nilishakupa like toka wakati huo? Maana hata sikumbuki kumbe nilishasoma huu uzi. Ni kweli kuna nyimbo nyingi za kiliturujia zinapotea. Tena zile ambazo zikiimbwa kanisa zima linapokea
 
Kuna hii kwaya ya mtakatifu joseph
Bakhita
Parokia ya chuo kikuu cha mzumbe (mbeya)

Walikuwa wanaimba vizuri sana sijui walipotelea wapi wale vijana
 
Back
Top Bottom