mwita ke mwita
JF-Expert Member
- Aug 13, 2010
- 7,848
- 3,483
kwa wale wanaopenda kwaya za kikatoliki, Bernad Mukassa si mgeni kwao, yeye ni mwalimu wa kwaya ya Mt. Kizito makuburi, ni mtunzi alijizolea sifa nyingi kwa utunzi wake wa nyimbo. hata ukichukua albam za kwaya nyingi huwezi kukosa wimbo wa Mukasa, licha ya kuwa mtunzi bora ila kwa upande wangu mimi naona MUKASA, na wenzake kama VICTOR MURISHIWA, E.L MKUDE, E.F JISSU, MANOTA na watunzi wengine wanaochipukia wanaanza kuharibu ladha ya muziki wa kikatoliki kwa kuingiza vionjo na free organ za ajabu ajabu, kwa mfano wimbo uitwao KIDOLE JUU ngoma zake zimechukuliwa kutoka kwenye wimbo wa kihindi uitwao GOLOGOLO na nyimbo nyingine nyingi ambazo MKUDE amekuwa akicheza KINANDA amekuwa akiiba free organ za nyimbo za dunia.Nyimbo za watunzi hawa nyingi zimekuwa ni za kasi yaani 6/16, badala ya nyimbo za kutafakarisha ambazo zilikuwa zikitungwa na JOHN MGANDU, DEO KALOLELA, MARCUS MTINGA,A.NGURUMO, J.MAKOYE, SEVERIN SWILLA na wengine ambapo nyimbo nyingi zilikuwa na mwendo wa 4/4, 2/4,3/4 na 3/8. vilevile watunzi hawa wamezidisha nyimbo mpya kila siku kanisani kama inawezekana nyimbo za kuuzia albam zisipigwe kanisani.
tunataka ile ladha ya kikatoliki irejeee
tunataka ile ladha ya kikatoliki irejeee