TANZIA Mwl. Samson Kibaso, mtunzi wa wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Afariki Dunia

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
13,731
21,132
Ni nani mtunzi wa wimbo wa EAC?

FB_IMG_1593601903359.jpg

PICHANI: Mwl. Samson Kibaso enzi za uhai wake.

Kuanzia 1999 hadi 2010 EAC ilikua ikitafuta wimbo rasmi wa Jumuiya hiyo. Aliyekua Katibu mkuu, Balozi Juma Mwapachu alikiita kipindi hicho "a decade-long search for a song that East Africans would call their own". Yani muongo mmoja mrefu wa kutafuta wimbo rasmi wa EAC. Watunzi zaidi ya 1,000 walipeleka nyimbo lakini hazikukidhi vigezo.

Kuna Mwalimu maharufu sana kwenye ufundishaji wa nyimbo za injiri anayetoka kanisa la waadvetista Wasabato anajulikana kama Mwalimu Kibaso, majina yake kamili ni Samson Kibaso mnamo mwaka 2010 alipeleka wimbo wake ambapo baada ya kupitiwa na jopo la wataalamu, ukaonekana unafaa.

Baadaye mapendekezo yakawasilishwa kwenye mkutano wa 12 wa wakuu wa nchi za jumuiya ya afrika mashariki ulioketi tarehe 03/12/2010 na wimbo huo ulipitishwa na kukubarika.

Kwa wale wadau wa njimbo za injili wa makanisa ya KKKT, Angrikan nk wanamfaham gwiji huyu katika ufundishaji wake, lakini hakuna mahali popote huyu Mwl. Kibaso anapokumbukwa kwa kazi hii kubwa, ukifuatilia hata serikali yetu ya Tanzania nadhani wamesahau au labda hawajui hili.

Kwenye website ya Jumuliya ya afrika Mashariki imeelezea historia ya wimbo huu lakini hawajataja mtunzi wa wimbo huo na haifahamiki ni kwa makusudi au bahati mbaya lakini wabunge wetu wa EALA walitakiwa wahoji na kutoa ufumbuzi.

Pamoja na yote gwiji huyu Mwalimu Samson Kibaso amefariki dunia wiki iliyopita jijini Dar es Salaam na jana amezikwa huko kwao Rorya Tarime mkoa Mara na serikali imeshindwa hata kutoa pole kwa familia.

Najaribu kuwaza angekua Mkenya ingekuaje? Nina uhakika serikali ingeubeba msiba wake na ingekua habari kubwa sana Afrika Mashariki.

Rais Kenyatta angeshiriki na viongozi wengine wa EAC wangeungana nae. Main stream media zingeifanya habari hiyo kuwa "lead story" na ingezaa "developing stories" nyingi. Zingeandaliwa makala kuhusu EAC kukosa wimbo na jinsi Kibaso alivyookoa jahazi baada ya miaka 10.

Lakini sisi tumechukulia kirahisi na kuona ni jambo la kawaida tu, serikali imeshindwa kumtambua late Mwl. Samson kibaso akiwa hai na bado imekataa kumtambua akiwa maiti, Eeh Mungu utusamehe kwaheri Mwalimu Kibaso, asante kwa utumishi wako kupitia uimbaji na umeacha alama isiyofutika!.

Appr: Mwl/Pr. Ezra Juma.

----

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa aliyekuwa Mwalimu na mwimbaji wa kwaya ya SDA Kurasini mwalimu Samson Kibaso kabla ya mazishi yaliyofanyika katika kijiji cha Ingrichini Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara.

mwalimu.jpg
 
Taarfa yake haijakamilika kama hakuweka wimbo huo
Nashanga mzalendo kama wewe humjui
Tatz mshazoea kuwasikia mondi harmonise
Nashangaa mpk muda huu viongozi kimya na hutawaona msibani cc:msiba wa meneja fulani

Ova
 
Nashanga mzalendo kama wewe humjui. Tanzania mshazoea kuwasikia Mondi, Harmonize.

Nashangaa mpk muda huu viongozi kimya na hutawaona msibani cc:msiba wa meneja fulani

Ova
Mkuu ina maana huujui wimbo wa Afrika Mashariki? Na kila siku unaimbwa kwenye halfa za kitaifa.!
We naye Kama hujui sema hujui. Sijui miccm ikoje jamani! Ptu
Mwanachama/shabiki wa chama tawala asiyejua wimbo wa Jumuia ya Afrika mashariki!!!!!!
Tatizo lenu mme base kwa kina mondi, harmonise, na juma lokole shilole, humjui huyu Samson alafu unasema ww mzalendo

Ova
Was hawazoea wavaa vikuku mguuni na wavaa pini puani

Ova
Nyote Ni vilaza kawe kamwambia mleta habari "weka huo wimbo" vilaza mmekurupuka,kwani yeye kaandika "siujui huo wimbo"? Mnakwama wapi bavicha? Mpaka aibu yaani!!!
 
Back
Top Bottom