Ulimpataje umpendae?

Bado sijabahatika kukutana na ubavu wangu. Naamini ipo siku wakati wa Mungu ni wakati mzuri sana. Hawai wala achelewi.
Bwana wa Majeshi,Mufalme wa Amani hakika ni Muweza wa yote!

Sasa na uamini wakati utayari na neno limetimia,
Karibu Kwangu MPENDWA.
 
Wa kwangu ni kicheko lakini nashukuru Mungu mpaka leo niko naye na sijawahi kuona kasoro zake. Nilipanda daradara asubuhi nikiwa tu nasogeza masaa sikuwa na muelekeo. Baada ya kilomita kama 2 nikamuona anapiga mkono kusimamisha gari. Kabla hajaingia mapigo ya moyo yakanienda mbio bila kutarajia. Lakini nikawa najisikia kumsemesha. Ndo ilikuwa mara yangu ya kwanza kumuona. Bahati nzuri tulishuka kituo kimoja. Konda akakosa change anirudishie huku naona yeye huyoooo anatembea. Nikasema simuachi bora niache hela. Nikamfata kwa nyuma na kumpiga picha. Kumuongelesha nikawa naogopa. Nikaamuwa tu nimfate mpaka nione wapi ataishia na nani ataongea nae ndo nipitie kwake. Mungu si Athumani bhana! Nikamuona mama mmoja mfanya usafi mazingira ya kazini kwao wakasalimiana na kujadili mawili matatu. Nikasema hapa umeisha. Jioni nikampigia simu mjomba wangu tuko sawa kiumri. Nikamueleza. Hapo hapo nikarusha picha whatsapp akamuone. Kumbe anamfahamu ! Akanipa na number yake nikamuona whatsapp ndo nikaanza na kumsoundisha. Mpaka leo hii niko nae,najiulizaga kwa mini sikumpata mapema! Na mwezi wa pili mwaka kesho ubwabwa tutakula na washikaji
 
Hongera sana kwakuopoa kitu cha kweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…