Ulimpataje umpendae?

karume kenge

JF-Expert Member
Mar 9, 2016
573
500
Binafsi niseme na kuanza kumshukuru Mungu kwa mke nilie nae mke bora na mama wa watoto wangu chipunga, helo na chipoku ukweli siku ya kwanza kumuona aliuchanganya sana moyo wangu mpaka kiasi kwamba nikasahau jinsia yangu kama ni mwanamke au mwanaume wakati nashangaa uumbaji wa manani ungeniita hadija ningeitika ungeniita juma ningeitika alikua kajaaliwa kwa kila kitu sura mpaka umbile nikaona isiwe tabu kwa kipindi kile nilikuwa rijali mwenye miaka 24.


Nilikua na ushawishi wa kila namna kwa mwanamke najua kuvaa vizuri na gari nzuri kifupi maisha yalikua mazuri bila kuchelewa ni katoa business card yangu na kumpa ikakataliwa duh kidume jasho likanitoka nikasema poa hakuna shida kwakuwa hakua anatokea mbali sana na kijiwe changu nikatafuta mtu wa karibu na kuhakikisha nakua karibu nae hatimae nikafanikiwa kumshawishi na kuwa nae karibu niseme tu ukweli.

Pamoja na uzuri wake wote sikuwa na mpango wa kumuoa sikuwa na muda wakati huo wa kuoa wala wazo nilimshawishi kwa muda wa mwaka mzima pasipo hata kuonja papuchi japo alikua anakuja kwangu kama kawaida mwisho nikajifikiria hivi kwa umri huu mwanamke wa kuoa si ndio huyu nahangaikia nini na dunia nimetumia ushawishi wangu wote na vizawadi nini lakini wapi mwisho nikaamua kutangaza ndoa na sasa tuna miaka 8 na watoto wawili asante Mungu.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom