Ulimbukeni wa ndoa

Ulimbukeni wa ndoa

brenda18

JF-Expert Member
Joined
Sep 17, 2013
Posts
5,687
Reaction score
5,297
Asilimia kubwa ya wanawake wanaopata kichaa cha ndoa ni wale ambao waume zao wana ulimbukeni wa ndoa kuanzia 5 ya kumi.

Mjue mwanaume limbukeni wa ndoa.
1.anaoa kwa heshima kabisa. Lakini bado atatafuta mwanamke wa nje wa kuzini naye.biblia inamuita hana akili kabisa.

2.Anaoa na ana mke lakini bado hawezi kujisimamia kila kitu anauliza mama yake mzazi ama kaka zake,biblia inasema aambatane na mke ila hataki.

3.Anarudi nyumbani kwake saa tisa za usiku,ama analala nje

4.Mke akiwa na pesa kumzidi haishi kusema anadharauliwa nk.

5.Hataki mke afanye kazi za kuingiza kipato.

6.Hajali wala kuwahudumia mke na watoto wake./ hataki kufanya kazi (marioo)

7.Hathamini mwanamke./anapiga mke.

8.Hataki wala kusikia kitu kinaitwa ibada. Ibada anazohudhuria kwa sana ni za mazishi tena wala sio kanisani ni makaburini.

9.Umri umeenda lakini bado utamkuta uvaaji wake, ishi yake,ongea yake,tembea yake kaa yake kama kijana anayebalehe

10.Hajali wazazi hasa wa mke.
*******************
Nakuja....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaume ndio chanzo kikuu cha kuvurugika kwa ndoa nyingi, huu ni ukweli ambao wengi wao wanaupinga. Ila kwa kiasi kikubwa wanawake wanapigania sana ndoa zao, lasivyo ndoa nyingi sana zingeshavunjika. Mwanamke na aheshimiwe daima.
 
Duh
 
Mwanaume hawezi kuwa chanzo cha kuvurugika kwa ndoa ikiwa atamwoa mwanamke anayejitambua, tatizo lenu mnataka kila mara ujue nyendo za mumeo, ujue mawasiliano yake, acheni hizo we angalia haki zako zinatimizwa hayo mengine muachie mwenyewe.
 
Ulichoandika yaani umepigilia msumari nilichokisema.
Kama unajijua bado una nyendo zako ulioa ili iweje? Subiri kwanza hadi utakapoelewa maana ya ndoa ndio uoe.
 
Mwanaume anaoa ili kuwa na mwenza wa kumlindia nyumba na kulea watoto, usije ukadhani tunapoamua kuoa basi umependwa sana hapana kuolewa kwako kuone kama bahati jiulize kawaacha wangapi wazuri wa haja akaamua akuweke wewe ndani kwae? Na nyie mkiolewa mnaanza kuleta amri zenu zisizo na kichw wala miguu, ndo maana tunaendeleza nyumba ndogo.
 
Hivi kwanza nazungumza na mvulana au mwanaume? How old are you?
 
Back
Top Bottom