Ulijuaje mpenzi wako anaku-cheat, na kwanini?

Ulijuaje mpenzi wako anaku-cheat, na kwanini?

Siku hiyo nilipigiwa simu na namba ngeni jamaa akajitambulisha kuwa amepata namba yangu kwenye simu ya demu wake amegundua tuna mawasiliano tata, nikamwambia ukweli kuwa huyo ni demu wangu!

Basi tukaongea sana, kumbe demu huwa anatupanga! Tukakubaliana tusimwambie kitu demu baada ya siku mbili demu akanitembelea room kwangu, mida ya saa nne nikamtumia text jamaa aibuke maana nilikuwa nishamuelekeza ninapoishi.

Jamaa alikuwa ni muajiriwa. Mimi na demu tulikuwa bado wanachuo. Basi mshkaji akaja hadi room na ndinga lake! Nikamfungulia akaingia, demu alipoteana balaa. Jamaa alikuwa muungwana akakaa kitandani, akamuuliza demu kwanini amekuwa akikubali mipango mingi anayompa kuhusu future yao wakati hapo hapo anapanga mambo hayo hayo ya future na Mimi?

Demu akaanza kumuomba msamaha mwana, Mimi hapo Sina langu nimekausha tu napiga zangu kiepe nilichonunua! Wakaongea pale ila jamaa akamwambia demu asijaribu kumtafuta hata kidogo, yaani amsahau, hataki hata kumuona! Demu akawa analia saaana, anaomba msamaha eti Mimi hanipendi anampenda yeye! Jamaa akawa na misimamo yake akaaga akatoka nje!

Na Mimi nikatoka nikamsindikiza jamaa kwenye ndinga yake, alichonishauri ni kuwa nimpige chini yule demu hafai, maana ananitosa kwa kuwa Sina hela na yeye anamng'ang'ania kwa kuwa ana hela so nipige chini! Nikamwambia poa! Jamaa akawasha ndinga akasepa!

Nikarudi ndani demu analia kichizi! Eti akaanza kunilaumu kwanini nimemuharibia sijui yule jamaa alikuwa anampa nini! Eti umbea wangu ndio umenipa kiherehere cha kupekua simu yake na kumpigia yule mchizi! Alinilaumu kichizi yaani hakutaka kuwa responsible kabisa, aliniona snitch!

Mimi nikamwambia jamaa alivyoondoka amenipa maagizo nikuache kama yeye alivyokuacha na kiukweli Mimi siwezi kubishana na wenye hela, wewe chukua vaa viatu vyako sepa! Siwezi kupingana na matajiri Mimi, ondoka! Demu hakuamini ila hatimaye alisepa! Jamaa akanipigia simu siku ya pili nikamueleza the whole story ilivyokuwa! Akawa bro wangu kabisa, nikienda town lazima nimtafute anitoe hata buku kumi ya kuunga chuoni! Demu aliendelea kugawa kwa washkaji na walimu Hadi tulipomaliza chuo, saa hizi yupo Moro hapo kachujuka hadi Ba wala Be! Mimi na jamaa still tuna mawasiliano na anataka kuoa mwaka huu mwezi wa tisa.. Kaniambia nijichange nichangie laki moja, siwezi kumuangusha bro! Nitachanga hiyo laki moja sasa nitakpokuwa Nataka kuoa Mimi nadhani atasimamia show!
Dahh. Nimecheka eti siwezi bishana na tajiri [emoji3][emoji3][emoji3] jf mnazingua
 
Sasaa mkuu huna helaa ya kugaramia mwanamke unategemea nini!nikwambie huku kitaa sisi mabrazaa wenu tunawala sana videmu vyenu vya chuo Tena hapo uwasibu ndo usisemeeee.soma utafte hela mapenzi tuachie wenye uwezo wa kumtunza binti na kuongaa.nyau weweeeee

Sent from my TECNO B1p using JamiiForums mobile app
 
Sitasahau X wangu alivyokua ananicheat mshenzi sana yule 😢😢 mpk leo sikupata ushahidi wa kimazingira ila dr alinithibitishia
Ushahidi wa kimazingira inabidi uambatane na physical evidence, La sivyo ni ngumu kushinda kesi
 
Ushahidi wa kimazingira inabidi uambatane na physical evidence, La sivyo ni ngumu kushinda kesi
Kesi nilishindwa kweli 😁😁
Ila nimeamini unaweza kupendwa na ukadekezwa na ukaamini upo peke yako
Kumbe mpk kama 10
 
[emoji3][emoji3]..Jamaa miyeyusho kinoma..alikuwa anakula kiepe huku anaskiliza manzi anavyozinguliwa.
[emoji16][emoji16][emoji16] ndio inavyotakiwa kwa kiasi fulani inatakiwa uwe na moyo wenye ganzi
 
Maisha haya sio poa nilidate na demu mmoja ananikubali mpaka na kesho siku hiyo niko naye out jamaa mmoja katokea kaanza muuliza huyu ni nani mimi nashangaa tu demu akadakia ni mtoto wa mam mdogo kizuri nilikuwa sijakaa naye bad position yeyote ikabidi nikubali sababu sipendagi ugomvi wa aina yeyote jamaa akaleta round za kutosha mezani siku iyo ikapita sikupenda kutengeneza scenario yeyote walichomoka wote ...kesho yake namuuliza anasema long story atakuja nielezea mimi nikapotezea ikapita kama siku tatu kaja kwenye biashara yangu na zawadi kibao namuangalia tu huku nacheka akaniletea blah blah nyingi kwamba yule lecturer mwenzake anaonesha nia ya dhati na yeye nikamwambia poa safari njema ....hakuolewa yule jamaa alikuja kufa na ajali ila bado napasha kiporo sidate naye tena akinikuta na dem yeyote ananiita mtoto wa mam mdogo kama kawa
 
Ungemchakata baada ya kesho yake kuondoka na yule msela.
 
Dahh. Nimecheka eti siwezi bishana na tajiri [emoji3][emoji3][emoji3] jf mnazingua
Matajiri wenye hela wamesema nikupige chini namm suwez kubishana na matajiri😂😂😂
 
Back
Top Bottom