Ulifundishwa Nini Uongo Shuleni?

Well said.
 
Hakuna kitu kinaniumiza kama kusema

""Education is better than money""

Niliikosea sana heshima pesa na namulaumu sana mwalimu wa English kuniaminisha hivyo, nilikuwa na propose kwa mbwembwe sana lakini leo pesa inaninyoosha hakuna mfano. Nilishaomba sana msamaha kwa pesa lakini ni kama imenifungia kioo kabisa.
 
Elimu ni ufunguo wa maisha🥴
Hii ni ukweli.
Elimu ndio inayokuwezesha kuishi. Na unaanza kuipata siku unazaliwa na kutambua ziwa la mama ili upate kuishi. Kuhisi kitu ni elimu ikuwezeshayo. Elimu inakupa ufahamu flani wa kuishi.
Elimu sio ile ya darasani tu, hata kujua namna ya kujitawaza ni elimu. Sasa ukimuondolea elimu binadamu anakuwa kama ng'ombe, yani hana maisha endelevu. Japo ng'ombe ana elimu kiasi ya kumudu mazingira yake.
Hata kujua jinsi ya kuvuka barabara ni elimu.
Hata kujua simba ni mnyama hatari ni elimu. sasa tukuondolee elimu ili ukamkumbatie simba ukimuoma.
 
Ivi wewe unajua tofauti ya elimu na akili???
 
Ivi wewe unajua tofauti ya elimu na akili???
Najua. Japo unaweza usikubali jibu langu.
Akili ni mfumo wenye uwezo wa kubeba elimu. Hivyo akili kwa mujibu wa maelezo yangu ni nyumba na elimu ni wakazi wa hiyo nyumba.
Nyumba ndogo (akili) hubeba wakazî kidogo (elimu), wengine hupotea na iliohadhîrika haiwezi kubeba wakazi kabisa.
Tupe uelewa wako
 
Watu wameenda mwezini.
ila watu wale wale walipoenda majini walivaa vile vile walivyo vaa mwezini.

Mic zinaelea wao wanaelea ila kuna maji yapo kwenye meza hayaelei.

Mwezi hakuna upepo bendera inapepea na zile alama za miguu zisingepotea.
Mwanga unapiga kutoka upande mmoja ila vivuli vinaposhana uelekeo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…