ULEMAVU NA UMASIKINI, JE NI PANDE MBILI ZA SHILINGI??

Jul 2, 2016
15
17
Ndugu wapendwa watu wenye ulemavu na jamii yetu ya kitanzania, salamu....napenda kutumia nafsi hii kwa dhati ya moyo wangu kuwakaribisha kwenye ukurasa huu muhimu.

Pia namshukuru Mwenyezi Mungu kwa fadhila zake na wema wake kwa kutegemeza maisha yetu na Tanzania yetu kwa namna ya kupendeza. Amen.

Wapendwa walemavu karibuni sana katika makala hii upate habari, elimu, uchambuzi na hoja makini kwa ustawi wa maisha yako.
Kabla sijaanza kujadili hoja na uchambuzi zaidi, napenda nikukaribishe kwa kukupa maswali machache uweze kuyatafakari yawe utangulizi na msingi wa ufahamu pia ustahimilivu wa hoja makala haya.

Maswali haya ni muhimu kwako ili upate mwelekeo wa makala hii na mengineyo, tumedhamilia kushinda changamoto na kuondosha umasikini miongoni mwetu. Me pia ni kiziwi na mwalimu.

TITTLE: ULEMAVU NA UMASIKINI, JE NI PANDE MBILI ZA SARAFU???

Maswali:
1). Je, ulemavu ni nini??

2). Je, mlemavu ni nani??

3). Je, unaamini kwamba kupatwa na ulemavu wa aina yoyote moja kwa moja unapoteza wepesi wa kutekeleza majukumu fulani yenye uhusiano wa dhahiri na ulemavu wako??

4.) Una mtazamo gani kuhusu umuhimu wa elimu kwa mlemavu ili kuwa na maisha bora.

a.) Ni muhimu...kwanini?? Eleza kwa kifupi mtazamo wako.

b.) Si muhimu...kwanini?? Toa hoja zako kwa kifupi.

5.a) Je, unadhani ni maarifa na ujuzi gani utakufaa kulingana na aina ya ulemavu wako??

b) Je, utayatumiaje maarifa hayo endapo ukiyapata??

6.) Je, unakiri ulemavu licha ya kupunguza wepesi fulani ndani yako, kuna uwezekano wa kuibua njia mbadala ya kumudu jukumu husika endapo utajikubali na kutafakari upya fursa nyingine??

7.) Kuna falsafa inasisitiza umuhimu wa kubadili fikra zetu na imani dhaifu(hasi) juu ya matatizo na changamoto zetu kutoka kitu kinachoumiza na kufukarisha kwenda kuwa ni fursa za ushindi na neema maishani??

8.) Je, kwa falsafa hiyo, ni kwa namna gan changamoto za ulemavu zinaweza kubadilishwa kuwa fursa ya kupaata ushindi na mafanikio ya maisha bora kwa walemavu wa Tanzania yetu??

9.) Je, ni fursa gani unaziona katika eneo/jamii yako na unadhani ukishirikishwa utaboresha maisha yako??

10.) Mwisho, ungependelea msaada au aina gani ya uwezeshwaji ili uwe na maisha bora??

N.B. Kwa watakaoweza kujibu maswali haya, tutatambua uwezo wao na mahitaji yao kisha tutafikiria namna ya kutoa msaada wetu kwenu.

SHARE NA WENGINE,
KARIBU SANA.
 
Back
Top Bottom