Just Pray
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 2,142
- 4,779
Waziri wa Ujenzi na mgombea ubunge wa Jimbo la Mkuranga kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdallah Ulega amesema kuwa Watanzania wanapaswa kumchagua Samia Suluhu Hassan kama kiongozi wao wa Taifa ili kufanikisha ndoto ya kupata Katiba mpya.
Akizungumza leo Jumamosi Septemba 6, 2025 kwenye uzinduzi wa kampeni za ubunge katika viwanja vya Kongowe, Ulega amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2025 - 2030 inaahidi kufufua mchakato wa Katiba ya Tanzania, na Samia ndiye kiongozi pekee aliye na historia, maono na uwezo wa kuleta mabadiliko hayo.
“Watanzania wenzangu, uchaguzi huu ni fursa ya kihistoria. Huu ni wakati wetu kuchagua mgombea urais ambaye anaweza kutuachia zawadi isiyosahaulika ya Katiba mpya ya Tanzania,” amesema.
Ameeleza kuwa historia ya kisiasa ya Samia inamuonyesha kama mwanasiasa aliyechaguliwa kushirikiana kwenye kamati ya maridhiano iliyofanikisha mwafaka wa kisiasa wa Zanzibar, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bunge la Katiba, na kuanzisha falsafa ya 4R, ambayo mojawapo ya misingi yake ni ujenzi wa maridhiano ya kitaifa.