Ule msimu umeanza tena....

Ule msimu umeanza tena....

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
371,617
Reaction score
860,794
Ni ule msimu wa hapa Jamii Forums... Msimu wa kuandika mada nyingi za kuwakandia wanawake kwenye mahusiano na hata ndoa
Wanawake wenye tafakuri ndogo wanaweza kukasirika na kuona kuwa kwanini wao ndio wanaandamwa kila siku.... Lakini ukilichukulia hili kwa undani wake utagundua kuwa ni tatizo kubwa zaidi la kijamii hasa kwa wanaume kuliko hao wanawake.... Ni tatizo kubwa linalotisha hasa na vijana wa kiume kwa kujifariji wanaamua kutoa nyongo zao kwenye mitandao kwa kuandika mada hasi dhidi ya wanawake, mahusiano na ndoa

Hawapaswi kulaumiwa... Bali sisi ndio tunapaswa na tuna jukumu kubwa la kuiponya na kuikoa hii jamii ya kizazi cha kiume kinachokaribia kusinyaa na kubaki jina tuu
Viainishi vya matatizo ya vijana wa kiume hivi hapa.... Na tusidhani ni kazi rahisi sana kuweza kutatua haya matatizo

1. USASA... vijana wengi sana siku hizi ni nyoro nyoro mno, laini na wenye kuchoka haraka na wasio na nguvu.... Teknolojia na usasa vinaharibu uimara na ujasiri wa kiumeni.. Ni ngumu mno kumtembeza kijana wa kiume km 5... Boda boda ndio kila kitu...
Simu janja, internet, tv, games nk ni vitu visivyohitaji nguvu... Tofauti kabisa na zama zetu... Tulicheza Michezo halisi ya kila aina na kujenga miili kakamavu

2.LISHE... Vyakula vingi vina kemikali na viko kwenye makopo na makasha na vinawekwa muda mrefu kabla havijatumika.... Wanakula vyakula mfu.... Vyakula vya nguvu kama Mihogo, viazi vitamu, viazi mbatata, ugali nk pamoja na vyakula vyote vya asili vyenye afya tele ukimpa kijana wa kileo anakuona how come kweli
Fasheni ni broiler, chips, burger etc... Imagine hata miwa mpaka wakamuliwe kama juice... Ukakamavu wa mwili utatoka wapi hapa?

3.BALEHE... balehe huja huku kijana akiwa keshafahamu mengi mno kupitia Internet na mitandaoni... Huko anachoona ni vijana wa kiume wasafi waliojipodoa sana... Hii inanasa akilini.. Anachoona ni porn za aina zote... Anatamani kuiga kuanzia ushoga mpaka ulawiti...
Mazoea haya humjengea Kutokujiamini na hivyo kuanza taratibu kujichua.. Vijana siku hizi wanajichua sana kwakuwa hawafanyi kazi za nguvu.... Zamani tulicheza michezo yetu nje huko na kule siku hizi ni simu janja kucheza game kitandani.... Akitoka kwenye game ataingia kuangalia porn na hatimaye kuishia kujichua....
Akishamaliza kujichua anakuwa hana hamu tena na haoni thamani ya mwanamke tena... Akizoea haya maisha siku akikutana na mwanamke ndio ile dakika keshamaliza...

Nina mengi ya kuandika lakini muda hautoshi.... Itoshe tu kusema kwa sisi tulio na watoto wa kiume tujitahidi kuwakuza katika njia ya ukakamavu, kuwaepusha na vyakula vya kisasa, matumizi makubwa ya Internet nknk
Unapoona kuna mada nyingi hasi juu ya wanawake, mahusiano na ndoa tambua kuwa hawa wanaoandika ni kiwakilishi cha wenzao wengi wenye tatizo kubwa kuliko inavyofikirika..... Tuwasamehe na kuwaombea sana lakini pia kila inapobidi tuwasaidie
 
 
 
Ungekuja na balanced review nadhani ingekuwa poa zaidi maana Naamini sio wanaume wa kisasa wote wapo hivyo na sio wanawake wote wa kileo wapo. Hivyo, kutengeneza maelezo ya kuonesha hali hali halisi ingekuwa ni bora zaidi kuliko kutoa counter attack.

Wanawake wanakasirika kusemwa kwa sababu inawaumiza fahari ya uanamke wao na wewe ulichokifanya ni kuumiza unaume wa vijana wa kileo. Kitakachofuatia ni endless arguments zisizo na maana . Kama watu wazima nategemea mtufundishe kuwa si vyema mambo ya chumbani kuletwa hadharani sababu tu ya mitandao na nyie kufanya kama tunayoyafanya vijana wa sasa inakuwa mnajidhalilisha.

NIMEMALIZA
 
Mkuu Unachosema ni kweli mfano mimi huwa napenda kula nafaka zisizonajisiwa, tetele za maboga + maboga yenyewe, mboga za kijani mbichi mbichi daily siruhusu ziive sana, matunda, kwa ujumla nakula vyakula natural sasa watu wanasemaga eti hivyo ni vyakula vya watu fukara mi huwa nawaangalia kisha nawaonea huruma.
 
Back
Top Bottom