Ulaji wa mafuta Toyota IST

Ibanda1

JF-Expert Member
Jul 18, 2015
705
1,092
Habari wakuu

Naomba niende kwenye mada moja kwa moja,baada ya msoto wa kutembea kwa miguu kwa miaka mingi bas niksjichanga changa ili ni usafiri na kila nilipoomba ushauri kwa wengi wakaniambia TOYOTA IST ni nzuri ukizngatia ulaji wa mafuta na uimara waje

Sikuweza kuagiza kutoka japani bali niliinunua kwa mtu na kila nilipoiangalia ilikua imara na hata mafundi walinisihi kuwa ilikua sawa haswaa

Sasa ni mwezi ila jehanam nayoipata juu ya ulaji wa mafuta wa hili gari ni ngumu kuhimili inabugia litre1 kwa km 7-8,nikiweka mafuta ya 10,000 bado taa ya mafuta inacheza kwa dashboard

Jumamosi niliweka kiwese cha 45,000 kama litre 18 hadi leo nmesogeza km 87 inaniwashia taa ya mafuta tena,naombeni msaada wa kiufundi wakuu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
David grayson,
Hiyo gari ni mbovu unahatarisha maisha yako na uliowabeba..Peleka service ifanyiwe scan kwanzia engine,Ac na mifumo yote hiyo gari cubic capacity yake haizidi 2000. Au imetembea mile age Km 2,000,000:D
 
Mkuu haiwezekana IST ikala mafuta kiasi hicho there is something wrong nenda kwa fundi ukachek diagnostic! Finally nakushauri usije ukathubutu kununua gari iliyotumika TZ mi ilinicost sana nilinunua OPA Kwa mtu nilikula hasara sana! Kwa kuitengeneza matatizo yasiyoisha Finally niliuza kwa pesa ya kutupa hata jamaa aliniuzia na rafiki zake urafiki umeisha tukikutana bar sio lazima tusalimiane kila mtu na maisha yake nimeamua nijichange tu nikamilishe pesa ya kuagizia kutoka Japan direct maana hata showroom sitaki kusikia
 
pole sana mkuu, vipi kwa injini kubwa kama 2000cc zinakua na shida kama hizo ndogo? najichanga nichukue chuma cha kuwa kinanipeleka kijijini itakua poa nikimvua mtu au ni salama?
 
pole sana mkuu, vipi kwa injini kubwa kama 2000cc zinakua na shida kama hizo ndogo? najichanga nichukue chuma cha kuwa kinanipeleka kijijini itakua poa nikimvua mtu au ni salama?
Usimvue mtu unless uwe umekubali risk kwa ushaur wangu nunua gari used kutoka nje na si double used! Kama mfuko hauruhusu ni vzur kuendelea kujichanga otherwise wahuni hawa madalali na wauzaji wasio waaminifu watanywea henken hela yako yote
 
Hiyo gari ni mbovu unahatarisha maisha yako na uliowabeba..Peleka service ifanyiwe scan kwanzia engine,Ac na mifumo yote hiyo gari cubic capacity yake haizidi 2000.Au imetembea mile age Km 2,000,000:D
Hivi mkuu,km 2,000,000 unazifahamu lkn?tena kwa IST?

Ma landcruiser yenyewe na magari mengine yenye CC Kubwa(eg cc 4200/4600)yenyewe yakifika Km 1,000,000 mpk huko youtube yanawekwa maana ni miujiza saaaana,ije kua IST?

Haiwezekani hio.
 
Vits cc 990 na vitz rs cc 1290 zina tumia mafuta kiasi gani kwa kila 1 , lita 1 kwa km ngapi
 
Back
Top Bottom